Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Alichoongea Rais ni sawa kabisa... huu ni ukweli unaouma..
Mtoto wa shule ya msingi mpaka sekondari anapata mimba maana yake nin?, maana yake kashakua mkubwa huyo aende akalee mtoto.. mwisho tuwe na watoto watakaokua wanaanza michezo ya ajabu mapema ambayo hata vitabu vya dini vimekataza kuzaa kabla ya kuoa au kuolewa....

tuachen kupinga kila kitu
 
Universal declaration of human rights:

Article 26.
(1) Everyone has the right to education. Education shall be free, at least in the elementary and fundamental stages. Elementary education shall be compulsory. Technical and professional education shall be made generally available and higher education shall be equally accessible to all on the basis of merit.

(2) Education shall be directed to the full development of the human personality and to the strengthening of respect for human rights and fundamental freedoms. It shall promote understanding, tolerance and friendship among all nations, racial or religious groups, and shall further the activities of the United Nations for the maintenance of peace.

(3) Parents have a prior right to choose the kind of education that shall be given to their children.

Article 27.
(1) Everyone has the right freely to participate in the cultural life of the community, to enjoy the arts and to share in scientific advancement and its benefits.

(2) Everyone has the right to the protection of the moral and material interests resulting from any scientific, literary or artistic production of which he is the author.

Article 28.
Everyone is entitled to a social and international order in which the rights and freedoms set forth in this Declaration can be fully realized.

Article 29.
(1) Everyone has duties to the community in which alone the free and full development of his personality is possible.

(2) In the exercise of his rights and freedoms, everyone shall be subject only to such limitations as are determined by law solely for the purpose of securing due recognition and respect for the rights and freedoms of others and of meeting the just requirements of morality, public order and the general welfare in a democratic society.

(3) These rights and freedoms may in no case be exercised contrary to the purposes and principles of the United Nations.

Article 30.
Nothing in this Declaration may be interpreted as implying for any State, group or person any right to engage in any activity or to perform any act aimed at the destruction of any of the rights and freedoms set forth herein.
Uko NGO gani...!??

Msituharibie maadili...
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Hivi vi-NGO uchwara vikatafute shimo la kuingia sasa.Vinapewa hela na wezi wa rasilimali zetu,halafu vinakuja kupotosha jamii zetu.Uharibifu double,hatukubali. Hata mjinga anajua kwamba ukiruhusu watoto wanaopata mimba waendelee na masomo, you are encouraging others to do the same.Hawa sijui akili za kijinga hizi wanazitoa wapi na sijui nani kawapandikizia.Nadhani ni roho za kipepo hizi, sio bure. Ku-encourage umalaya kwenye jamii!

Hongera Rais wangu kwa uamuzi huu wa busara mno.Jambo hili lilikuwa linanikera mno.
 
Bado naendelea kufanya utafiti , lakini mpaka dakika hii dalili zinaonyesha kwamba DR JOHN MAGUFULI anaweza kuwa ndiye raia wa Tanzania mwenye ROHO MBAYA ZAIDI KUWAHI KUWEPO TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI .

He is too aggressive !
 
our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,

mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,

kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,

its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.
hajasema aliempa Mimba aendelee na shule... kasema aliempa Mimba awe mwanafunzi au mtu wa mtaani nae aende jela miaka 30
 
Duh..
Kwa hekima za Raisi Ni wazo zuri..

Mimi Ni mwalimu,lakini kwa hili simuungi mkono hata kidogo..

Watoto wakike wanachangamoto nyingi sana,ikiwemo kutokukomaa kiakili, kubakwa,n.k

Hivyo tukiwaadhibu kwa kuwataka wafikiri kama watu wazima wakati wao Ni watoto tutakuwa hatuwatendei haki.

Ushauri wangu raisi atilie mkazo katika kudhibiti vyanzo vya mimba kwa wanafunzi.
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa. Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu. Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!

Wewe ndiyo umekosea. Ukisharuhusu huo ujinga bas ndo unahamasisha mapenzi shuleni na utapata matukio mengi sana ya watu kuzaa na kuomba kurudi shule. Mtu anayependa kuzaa azae na aendelee kuwa mama huko mtaani maana ndo alichochagua badala ya elimu.

Haya mambo ukwel tukiyakubali yatatuletea shida sana kwenye malezi hata wazazi. Ulaya binti analeta mwanaume ndani ya nyumba nyumbani kwao na analala naye eti ni haki yake, matokeo yake ni mimba na mwisho wa siku eti bahati mbaya aachwe arudi shule.

Ndo mchezo wanaoenda kutuletea. Kila kitu haki haki haki hata mijianaume kulalana eti haki. Hizi haki za kijinga zikizidi kuruhusiwa mwishowe itakuwa hapakaliki
Hao wa ulaya unaosema kuwa wamelichukulia busara wana maendeleo kuliko sisi.....sasa makosa ni yapi?
 
Hapo Rais bado hajafanya solution.....mimba kwani hazitoki?
 
Comment za page ya kwanza na kuendelea zinampiga juhudi za rais za kukemea ushoga, Raia wa Tanzania walisha data.... Kama upinzani ndiyo huu wa kutetea mashoga ni bora msajili wa vyama akavifutia usajili vyama vya upinzani vyote....
Sawa Mwanaccm washakusikia
 
Magufuli yuko sahihi. Tunapokea tu kila kitu kama makinda ya ndege, shwaiiin!
 
Mngekuwa walimu, wala msingemlaumu Mh Rais. Kwa kauli hiyo mm sijaona kosa lake hapo. Ni ukweli usiopingika kuwa lazima watoto wetu wazingatie maadili mema hasa wanapokuwa wanafunzi/shuleni. Mtoto akipata mimba in haki asirudi shuleni. Adha inayopatikana huko shule za serikali ni kubwa sana, kufundisha wazazi wenzio ni shida kubwa sana. Hongera mh Rais.
 
Duh..
Kwa hekima za Raisi Ni wazo zuri..

Mimi Ni mwalimu,lakini kwa hili simuungi mkono hata kidogo..

Watoto wakike wanachangamoto nyingi sana,ikiwemo kutokukomaa kiakili, kubakwa,n.k

Hivyo tukiwaadhibu kwa kuwataka wafikiri kama watu wazima wakati wao Ni watoto tutakuwa hatuwatendei haki.

Ushauri wangu raisi atilie mkazo katika kudhibiti vyanzo vya mimba kwa wanafunzi.
Hivi vi-NGO uchwara ndivyo vilivyo wapandikizia mawazo hayo potofu.Mkuu hata ukiwa mwalimu unaweza kupotoshwa.Mwalimu, wanafunzi waamue moja, kusoma au umalaya, hakuna jinsi.Ukiruhusu ujinga huo, utakuwa unahamasisha umalaya mashuleni,hatukubali.Mimi kama mzazi nasema uamuzi wa Rais ni wa busara mno.Hongera zake.Jamii yetu imepotoshwa vya kutosha,enough is enough.
 
Mngekuwa walimu, wala msingemlaumu Mh Rais. Kwa kauli hiyo mm sijaona kosa lake hapo. Ni ukweli usiopingika kuwa lazima watoto wetu wazingatie maadili mema hasa wanapokuwa wanafunzi/shuleni. Mtoto akipata mimba in haki asirudi shuleni. Adha inayopatikana huko shule za serikali ni kubwa sana, kufundisha wazazi wenzio ni shida kubwa sana. Hongera mh Rais.

kazi gani kubwa kusomesha wazazi wenzio?labda mkileta changamoto zenu tutawaelewa
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.

Sioni Rais alipokosea na sio kwamba namtetea..he is very right.Ndiyo maana kaweka exceptional waende private.Kupata mimba kwa mwanafunzi wa kike ni kosa.Kwanza kujihusisha katika mapenzi kwa wanafunzi ni kosa.Tusitake kufanya watu wazidi kukiuka maadili eti wakishusha engine warudishwe darasani..haitakuwa na maana na haimfundishi chochote yule mwingine ambaye hakupata mimba aachane na uzinzi.Kwa hali hii watasoma tuu na hawatawaza uzinzi.
 
Hata aliposema hatatoa chakula cha bure watu hamkumuelewa Rais,matokeo yake watu msimu huu wameingia shambani kwa wingi na hawatachezea tena chakula
 
Back
Top Bottom