Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Nimefuatilia uzi nikagundua wanaoshabikia hili ni wale wale waliambiwa "Pesa si za umma" wakashangilia, baadae wakaambiwa "Pesa ni za umma" wakashangilia tena

Ndivyo walivyo!
 
Nadhani mtoto akipata mimba akaenda nyumbani kujifungua anaweza kurudi kuanza form one kwa private schools. Magufuli hajafunga njia kabisa.

Tunaweza kutofautiana kwenye mitizamo lakini msimamo wa Magu wa kuzuia wazazi kurudi shule hauna tatizo na inaweka discpline kidogo kwenye michezo yao ile.
 
Mtoto wa kike anapita changamoto nyingi Sana. Tuwaombee. Ikitokea bahati mbaya warudi shule. Raisi usitoe maamuzi kama mungu.
 
hongera JPM. kwa hapo nakuunga mkono. wakati wa shule iwe shule. wakati wa kutotoa iwe kutotoa tusichanganye mada. tusichanganye mada.mabinti wajitahidi kuweka kufuri
 
Watanzania saa nyingine tuwe wakweli, kuna mtu anasomesha wajawazito kweli? jiulize maswali haya kisha nipe majibu
1. Mwezi wa ngapi mtoto mzazi atakatisha masomo yake? (kumbuka ujauzito ni miezi 9)
2. Miezi atakayokuwa shuleni akilea ujauzito wake mchanga, je nini mahusiano yake kati ya walimu na wanafunzi wenzake darasani?

3. Ni mwezi wa ngapi baada ya kujifungua ataruhusiwa kuendelea na masomo yake? kama ni miezi 3 baada ya kujifungua - je atapewa muda wa kuondoka mapema shuleni na kwenda kunyonyesha mtoto? kumbuka kunyonyesha si chini yamiezi 6.

4. Je baada ya likizo ya uzazi, mtoto huyu Mzazi atakuwa na uwezo wa kuyakumbuka aliyofundishwa miaka iliyopita? hasa ukizingatia suala la uzazi si la mchezo - tena mtoto mzazi huyu bado alikuwa hajapevuka - i mean impact ya uzazi itakuwa imemwathiri vipi kisaikojia?

5. Uhusiano wa huyu mtoto mzazi na walimu wake utakuwaje baada ya ku-resume masomo yake; atakubali adhabu zote kama watoto wengine? kuna adhabu zingine hasitakubalika kutokana na uzazi - Wizara itatoa dokezo kwa watoto wa namna hii? Kwa mfano huwezi kumwambia mtu aliyetoka kujifungua miezi 6 ati aruke kichura, akimbie kuzunguka darasa sababu kachelewa nk


6. Je mapokeo kwa wanafunzi wenzake yatakuwaje? kumbukeni age kama hii kuna utani mkubwa - na nakumbuka kuna watoto huwa wanaacha shule sababu ya utani utani kwa mfano: we mama jitahidi darasani kama huwezi kalee mwanao nk

7. Je atakuwa na uwezo wa kuhimili mikiki ya masomo yake huku ana mtoto anahitaji attention yake akifika nyumbani? kuna H/W na kazi ambazo mtoto anahitaji muda kuzifanya akiwa nyumbani - Sitaki kusikia ati Bibi wa mtoto atamsaidia - si kazi yake.


Yapo mengi tu ambayo ukifikiri sana unaona kuruhusu kitu kama hiki hutakuwa umemsaidia huyu mtoto mzazi. Hao wanaharakati watafute njia nyingine ya kuwasaidia hawa watoto lakini si kwa kuwadanganya kwamba wakirudi shule wanaweza kuzikabili changamoto hizo hapo juu.

Kuruhusu jambo hili hamuoni litakuwa kama fungulia mbwa? watoto hawa hawa wanajua zipo kondom madukani tena zingine zinagawiwa bureee, lakini hawapendi kutumia - sasa kuruhusu kitu kama hiki ni kujaza wajawazito mashuleni.

Narudia tena, zile NGO zinazotaka watoto hawa wasome, zinaweza kuanzsiha program maalum nje ya ile ya kawaida ya kuwasaidia - wakija na write-up nzuri basi hata Serikali na sekata binafsi inaweza kusaidia pia.

JPM upo sahihi.
Mimi naona hili jambo liachwe kama lilivyo tusilipinge wala tusilikubali maana tulikikubali wazae halafu warudi ni janga na pia tukisema wasisome pia siyo vizuri tuliache kama lilivyo
 
Mkuu Malizia yote pia amesema watakaowapa mimba wanafunzi miaka therathini jela, mimi namuunga mkono kwa sababu nina watoto wengi wa kike
Zidi tu kumuunga mkono chizi anaekurupuka, mtu anaweza kumpa mtotowako mimba alaf akakimbia akatokomea kusikojulikana utabakia na hao watotowako ukiwa unaleawajukuu wasio na baba. Alaf bintizakopia watabakia nyumbani bila kwendashule utakaanao nyumbani as if ni wazako. Na je ataakifungwa si bado wewendio utagarimika kuwalea wajukuu kufungwa miaka 30 kwa mtuhumiwa weweitakusaidianini wakati bintizako pia hawatasoma?
 
Safi sana mheshimiwa ni upuuzi Kweli mwanafunzi hukufuata mapenzi Bali Elimu.Umepata mimba ukiwa shule hakuna kuendelea ni mawazo mfu .safi sana Raisi wetu Excellent.
 
Naunga mkono hoja ya Mkuu kupunguza baadhi ya wanafunzi kutumia fursa hiyo, yaani kuwa mama wa famikia huku anasoma, hii itapelekea wanafunzi wengi kutokuogopa kufanya ngono kiholela kwakuwa wanajua haitodhuru elimu yao.
 
kwa hiyo amechagua ujinga.. tafuta wapiga kura mzee.. ukiwasomesha imekula kwa ccm
Hapana,ukiliangalia suala hili kwa jicho la tatu ni sahihi kabisa alichosema Rais, hii ilikuwa inakatisha tamaa sana waalimu, pia maadili ya kijamii sio sahihi.Inawezekana vipi binti azae akiwa shuleni halafu tena arudi shuleni,hivi si atawadharau walimu kuwa hakuna kigeni asichokifahamu kuhusu mambo ya mapenzi? Si atawafanya wenzake waone ni sawa kujihusisha na ngono?Wakipata watoto si ruhusa kusoma tu? Kutakuwa na nidhamu kweli shuleni? Tunaimbishwa nyimbo za kijinga na wazungu nasi tunaimba na kuzifuata. Tumeletewa haya mafikirio ya wanaume kuoana wenyewe kwa wenyewe bado tunaona wapo sawa. Hivi kweli ambayo wanayapigia kelele tuyafuate na kuyafanya ambayo ni kinyume na utu anapotokea kiongozi kuyakemea bado tunalaamu tu na kuangalia kura? Viongozi wasifanye kazi eti kwa sababu kuogopa kutokosa kura? Za nani, zako au na za wengine wanaoona katazo hili ni sahihi kabisa? Tuwe na mishipa ya aibu kutotetea upuuzi tunaojazwa na hawa ngozi nyeupe. Yaliyo mazuri tuwakubalie, lakini ya udhalilishaji tuyakatae katu. Hizi NGO,s zinasapoti kwa sababu wanataka fedha, ila kwenye familia zao kimoyomoyo hawataki kusikia hicho kitu, waswahili walisema, pesa sabuni roho.Hivi huko majuu watoto waliozaa shuleni wanarudi tena shuleni kuendelea kusoma wakinyonyesha?Katazo hili litafanya watia mimba washughulikiwe hivyo kuleta woga wa mimba kwa watoto wa shule. Rais yupo sahihi kwa katazo hili.
 
kwa hiyo amechagua ujinga.. tafuta wapiga kura mzee.. ukiwasomesha imekula kwa ccm
Wajinga ni bora kuliko mafisadi sodoma na ghoroma. Anayesoma kikwelikweli hatapenda sera ya ushoga au sodoma; mtabaki hawo hawo na ajenda yenu ya ukabila mnaitafutia hoja za kila aina
 
Hivi vi-NGO uchwara ndivyo vilivyo wapandikizia mawazo hayo potofu.Mkuu hata ukiwa mwalimu unaweza kupotoshwa.Mwalimu, wanafunzi waamue moja, kusoma au umalaya, hakuna jinsi.Ukiruhusu ujinga huo, utakuwa unahamasisha umalaya mashuleni,hatukubali.Mimi kama mzazi nasema uamuzi wa Rais ni wa busara mno.Hongera zake.Jamii yetu imepotoshwa vya kutosha,enough is enough.
Sjapotoshwa niko makini sana!!
Sema tatizo langu mimi siyo muumini wa mawazo ya ghafla hasa ya kiongozi mkubwa kama raisi wa nchi.

Hakuna anae unga mkono ama kutetea wanafunzi kupata ujauzito wakiwa shuleni.Ama kutetea utovu wa nidhamu kwa wanafunzi.

Lakini Ni mhimu kutafakari kwa kina njia sahihi ya kunusuru hatima ya mabinti Na Dada zetu kabla ya kuwahukumu wakati sababu za wao kupata mimba wkiwa shuleni Ni nyingi mno.

Aidha,Kuhusisha NGO's kwenye hili na kubeza mchango wa NGO's Ni utovu wafikra chanya Na Ni uvivu wa kufikiri.

Mfano Leo hii utabeza mchango wa tafiti za haki elimu kwenye hili @kwasababu raisi kasema!!!?

Lengo la mwanafunzi aliyepata ujauzito kurudi shule bada ya kujifungua lilikuwa Ni kutaka kutoa nafasi ya pili kwa wanafunzi hasa wenye uwezo Na nia ya kurudi darasani kurekebisha makosa yao ama wale ambao walikuwa Ni wahanga wa matukio ya ubakaji ama kurubuniwa Na wanaume watu wazima au vinginevyo kupata hatima njema kielimu.

Hili lilikuwa Ni wazo zuri sawasawa Na kutoa frusa kwa waliofeli kidato cha pili kukariri darasa ama waliofeli kidato cha nne kurudia mitihani.

Wenye ufahamu wanajua fika Mazingira ya shule za serikali hasa za kata Ni hatarishi sana Na ndio chanzo kikubwa kikifuatiwa Na umasikini wa kipato katika familia pamoja na ukosefu wa maadili katika jamii.

Kuchukulia kigezo kimoja tuu cha utovu wa nidhamu Na kukosa maadili,kuwahukumu wanafunzi wa kike Na kuwanyima frusa ya pili kupata haki ya elimu Ni uvivu wa kufikiri narudia tena Ni uvivu wa kiwango cha juu sana!!!

Kwanza shule nyingi za serikali zinahamasisha sana mihemko na fikra za ngono kwa vijana wetu hatimae mimba kwa wasichana.

Mfano...
Shule nyingi hazina mabweni
Hazina maabara
Hazina makitaba
Zipo mbali Na makazi ya wanafunzi(hasa vijijini)mwanafunzi anatembea umbali mrefu Na njaa kali

Upande wa pili
Walimu hawatoshelezi hasa masomo ya sayansi
Hakuna nyumba za walimu
Mishahara duni n.k

Nyumbani kipato duni Na umaskini wa kipato n fikra hasa kwa wazazi waliowengi nayo Ni mimba nyingine.

Katika mazingira ya namana hii huwezi kuzalisha kizazi chenye fikra chanya hata kidogo mana wanafunzi na walimu woote wanawaza nje Na taaluma.

Wakati mtoto wa private yuko maabara akifanya mfunzo kwa vitendo ama makitaba akiwekeza ufahamu kwenye ubongo....

Mwanafunzi wa shule ya kata atakuwa anapiga kelele darasani ama akiwa Na msongo wa mawazo atarudije nyumbani Na akifika atakula Nini!!n.k

Alafu out of the blues mtoto anapata mimba unakrupka kaa ulee mtoto hapa hakuna shule bila kujiuliza sababu ama nini hatima ya binti yako Na mjukuu.!!

Namkubli JPM kwa mengi lkn pia sikubaliani nae kwa mengi hasa Hili la kuwanyiwa second chance wanafunzi Wangu ambao kimsingi Ni wahanga wa mfumo mbovu wa elimu nchini.

"I have the freedom to disagree with you just as you have the right to defend your mediocrity and ignorance"





Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Huo utaratibu bora maana watoto wa sasa hivi wamezidi ufuska, wana mambo mazito kuliko hata wakubwa zao. Watashika akili kidogo siyo kujiachia eti wakizaa watasoma tu, mna magonjwa pia jamani na hawa sijui kama wanakumbuka kuna kuambukizwa. Wakihofia mimba ngono zembe watazikimbia na wengine hata kuacha kabisa, hapa wataokoka watoto wengi kwenye mimba na maradhi.
Watajua kabisa wakishika mimba ndiyo basi. Hii itawafanya wawe makini mno.


Jamani kwa anayewajua watoto wa siku hizi hasa shule za kata walivyo na mambo ya ajabu, huwezi kumponda JPM.
 
our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,

mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,

kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,

its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.
Halalisheni zinaa tu iko siku yenu
 
Back
Top Bottom