Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Namuunga mkono raisi hatuwezi kushindwa kuwalea watoto wetu wa kike alafu tuachwe tu
Ukishika mimba olewa uliipenda ngono kakae kwa mwanaume siyo urudi darasani
 
Watanzania bwana kwa ujinga na kujifanya wajuaji ni namba moja...

Kwahiyo mlitaka Raisi aseme "mwanafunzi akipata mimba ni sawa tu, ataendelea na shule..." Big NO, haiwezekani...

Angeruhusu hilo uku mtaani ingekuwa machafuko, mazingira ya watoto wengi wa kitanzania tunayajua. Watoto wangeanza kupigana mimba uku mtaani. Yani mtoto anazaa mtoto. woga saa nyingine unasaidia...

Msilete mambo ya ajabu.... Msitetee mambo ya ajabu...
Ni kawaidaa yetu WTz kujitoa akili....

Ni sawa na Viongozi wa dini waruhusu na kuchampion matumizi ya Condoms au Utoaji mimba...

What do you expect kitatokea Mtaani..?!??
 
unatoa taarifa polisi within 24 hrs, unapatiwa tiba yavali na unakuwa na documentation, daktari atathibisha kuwa kweli umebakwa

lingine
Baada ya kutoa taarifa ya kubakwa na bahati mbaya akapata ujauzito na kuzaa, je Binti ataendelea na shule kama anahitaji au ndo basi tena? Maana huyo hakujitakia baali ni majanga tu yamemkuta
 
His Excellency The Head of State, si kuna wachungaji hapa.

Tunahitaji Elimu Elimu Elimu. Ushabiki baadae.
 
Nina visa viwili

#1. Kuna binti mmoja alipata ujauzito akiwa kidati cha nne mwanzoni..... Akaenda kufanya Mock kisha NECTA akafaulu kwa kiwango cha div 2...

Akaenda kidato cha Tano.... Huko mbele ya safari sijui aliishia wapi.


#2. Mwingine alirudi shule akafaulu akapangiwa kidato cha Tano Mawenzi Sec .. Akamaliza Kidato cha Sita kisha akaenza Mzumbe akachukua digrii yake lao hii ni mfanyakazi wa Umma.
 
Dah, inasikitisha sana kuwaona watu kama nyie mnashangalia suala la mtoto wa kike kunyimwa haki yake ya msingi "Elimu". Kuna msemo usemao "mtoto akiunyea mkono haukati", sasa kwanini mtoto wa kike akibeba mimba anyimwe haki yake. Mm nina mdogo wangu alibeba mimba akiwa shule ila alifanikiwa kuendelea na masomo yake na baada ya kujifungua alilea mtoto miezi mitatu akarudi shule kama kawaida. Mimba sio ulemavu na kupata mtoto sio mwisho wa maisha.
Alirudi shule hiyohiyo !?? Ilikuwa ya serikali!?
 
Inaonekana wanahumu wengi mlisoma/mnasoma mkiwa na u...ja...***t**o
Mhh jaman napita tuuu
 
Mnajitaidi kweli kutafuta anakosea mh mkosoe ila mtahangaika sana ndo mwaka na nusu bado miaka nane na nusu kazi mnayo,mbona kwenye mazuri hamsemi upuuzi upuuzi tu
 
Nina visa viwili

#1. Kuna binti mmoja alipata ujauzito akiwa kidati cha nne mwanzoni..... Akaenda kufanya Mock kisha NECTA akafaulu kwa kiwango cha div 2...

Akaenda kidato cha Tano.... Huko mbele ya safari sijui aliishia wapi.


#2. Mwingine alirudi shule akafaulu akapangiwa kidato cha Tano Mawenzi Sec .. Akamaliza Kidato cha Sita kisha akaenza Mzumbe akachukua digrii yake lao hii ni mfanyakazi wa Umma.
Kwahiyo unataka kusema nini!!??
 
Rais anapokuwa wakwanza kuwanyima watu wake haki yao yakupata elimu basi tupo pabaya sana kama taifa.
Haki ya Elimu ni haki ya Msingi..... Ndio maana ilipoonekana kuwa watu wengi wamekosa hiyo haki ilibidi ianzishwe Elimu ya Watu Wazima

Lengo ni ili nao wapate Elimu
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Hard science versus social science!!!!! Remmy aliimba "mambo kwa socks" na wimbo ukafungiwa lakini baada ya muda watu wakawa wanahimizwa kuchukua condom za bure!!!
Social science imsaidie Mzee wa Chemistry,wampe ushauri unaostahili.
 
Nataka niwaambie hawa ngo's Na taasisi nyenginezo... Katika utawala wangu mwanafunzi atakaye pata ujauzito akiwa shuleni ( kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ) Hakuna ruhusa kwa mwanafunzi huyo kuendelea na masomo baada ya kujifungua..

"NATAKA NISEME, KATIKA UTAWALA WANGU HAKUTAKUWA NA KITU KAMA HICHO "
Yani hapa analijibu lile tangazo la Haki Elimu
 
Back
Top Bottom