Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

I. Soldier,

Watu wengine hawaangalii side effects za tamko la wazi la kukubaliana na huo upoyoyo wa watoto wa kike wa shule.

Binafsi, tamko hilo hata wakiliwekea sheria kabisa itakuwa poa sana.
Mkuu, wakiruhusiwa kusoma hao wakiwa na mimba watafanyana sana. Tena wakikamatwa watasema rais aliruhusu.

Watu wengine translation inawasumbua kidogo.
 
Me Nakubaliana Sn Na Rais, Haki Lazma Iendane Na Wajibu. Umepewa Nafasi Ya Kusoma, Soma. Haiwezekan Sheria Iwekwe Kali Kwa Anaempa Mwanafunzi Ujauzito Af Wao Et Wanarudishwa Shule, No No Labda Wawapeleke Private. Hatuwez Kuipa Serikali Mzgo Wa Kulea Watoto Wetu Lazma Wazazi Tujipange. Maana Wazaz Tumewaachia Waalimu Kila Kitu. Bado Wale Wazaz Ambao Wanaweka Mtoto Mwali Wkt Anasoma, Wanapaswa Kufungwa, Huyu Binti Ndo Anakuja Kufundisha Wenzake Ushenzi Darasani. Wanafunz Ck Hz Wanamiliki Cm Hadharani, Wanavaa Nusu Uchi, Wanajipga Picha Chafu. Ndo Madem Wa Waendesha Boda Boda, Makonda Na Madereva Wa Madala Dala, Anaweza Mkubwa Panda Gar Hawampish Mzee Kwenye Siti Ukichunguza Ndo Vdem Vyao. Af Useme Warud Shule, Kufanya Nn? Cc Pia 2liptia Balehe Lkn Wapo Walioamua Kusoma, Wa Ckuhz Et Wamepnda. Wazaz Wawajue Wajibu Wa Kulea Kiumbe Ni Wao, Akipata Mimba Tafuta Kwa Kwenda Kusoma Full Stop. Hv Kwann Marais Wengine Hawakua Km Huyu? Nadhan Hata Enzi Za Beni, Ali Na Mwl Ilikua Hv Pia. Safi Sana.
 
Mkuu hilo ni swali au ushajijibu mwenyewe?Mazingira yasiyo rafiki ya kusomea haswa shule za kata za kutwa.
Na wazaz wanachangia watoto kuwa na tabia za kishenz....
.
.mzaz inabd umfatilie mwanao nyendo zake shulen na kumbana asipate mda wa kucheza michezo ya ajab ajab
.
.zaman ilikuwa haina shida sana coz utandawaz ulikuwa haujatanda bado ila saiv inabd wazaz wabadrike waongee na watoto wao kuhus kujtambua....
.
.mzaz wa kike asitegemee kumfundsha mwanae kupika tu katka nyakat hz , LAZIMA WAZAZ WABADIRIKE ILI KUPUNGUZA MIMBA MASHULENI
 
Naomba kuuliza hivi inakuwaje kama wote ni wa darasa moja na wana umri sawa?(mschana na mvulana )....
.
.sheria inasemaje?? , je mvlana amebaka au wamebakana??
 
Kama kweli kasema hivyo basi kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Kuruhusu hilo jambo ni kuhamasisha au kutoa upenyo wa watoto wa kike kujiingiza ktk ngono wakiwa wanafunzi tena wakiwa na umri mdogo, kitu ambacho ni distraction ya kufanya vizuri ktk elimu yao na pia hatari kwa afya yao. Labda waruhusu waliothibitika kubakwa pasipokuwa na shaka.
 
our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,

mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,

kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,

its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.
nani anayemwambia akubali amebakwa?
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.
mbona wengi mnakimbilia kubakwa mnadhani tuna taifa la wabakaji?
 
hata private wenyewe hawafundishi wamama labda mnipe mfano wa shule inayopokea wamama, tena hairuhusiwi kupata mimba wakigundua tu kuwa ni mjamzito wanakutimua siku hiyohiyo
 
NAMPONGEZA RAISI WANGU KWA KUWA NA MAAMUZI MADHUBUTI...

NAUNGA MKONO HOJA YAKE..SERIKALI HAIWEZI KUTOA PESA WATOTO WAKASOME HALAFU WAO WAKAJIFANYIE NGONO WAJAZANE MIMBA HALAFU WARUDI SHULE KUJAZA NAFASI ZA WANAFUNZI WENYE UHITAJI..MUDA WAKO UKIISHA SOGEA MBELE WAPISHE WATOTO WENYE NIA NAKUSOMA WASOME.

PIA KUNA SHULE BINAFSI WEWE KAMA MZAZI HUKULEA MTOTO KATIKA MISINGI BASI AKIPATA MIMBA KUBWA KAMLIPIE SHULE HIZO BINAFSI..NCHI HAIWEZI KUPOTEZA PESA KWA AJILI YA UTOVU WA NIDHAMU.

RAISI AMELENGA PIA KUTOKOMEZA NGONO ZEMBE WATOTO WETU NA WAELEKEZE NGUVU KATIKA MASOMO..WAKIKUA WATAFANYA TU HAKUNA MTU ATAWAFATILIA..SIO NCHI WALA SIO WAZAZI.
 
Eti anasema,"siwez nikatoa pesa za kusomesha wazaz" hizo pesa ni zake hata wanaopata mimba wanatka kodi hata ka si wao,lkn wazaz wao wanatoa, wana haki ya kupata elim..au kwa kuwa kashagundua kwamba kutawala wajinga ni simple sana ndo mana anaendelea kuminya elim,,
Note: this thing called change is a part of our nature,though others are reluctant to change..but one day they will change too.
 
Tatizo lake yeye, Ndalichako, Salma Kikwete na wengineo wanaotetea huo upuuzi ni kuwa misinformed.

Sera za dunia zinaandaliwa kisayansi sio moral view points labda kwenye nchi zilizo na misimamo mikali ya kidini.

Ni hivi kigezo cha afya bora kwa tafsiri ya WHO sio kukosekana kwa maradhi tu bali usalama wa mtu kwa ujumla wake ikimaanisha mazingira bora ya kila siku, kuwa na elimu ya kutosha kumwezesha kufanya maamuzi sahihi (saa zingine mtu anapata magonjwa ya maambukizi au anabeba kisa elimu tu ya kujua umuhimu kutumia kinga), ushirikiano wa mtu na familia na jamii (inawezekana kuna watoto wanapata hizo mimba kwa sababu wazazi awawezi kuwapa ata basic needs zao) etc.

Ndio maana kwenye afya kuna arguments za health inequality wenye mapato mazuri kawaida wanaweza ishi zaidi kwa sababu wanapesa za kupata access ya huduma bora ukienda muhimbili utakuta wazazi na watoto wanaokufa kwa uzazi ni wale wa chini kuliko matajiri, wanaelimu ya kuzuia magonjwa ambayo chanzo chake ni lifestyle, etc.

Kwa hivyo kwa jicho la NGO kupambana na elimu ya watoto wanaopata mimba sio kuleta agenda zao la hasha wao wanachoongalia ni 'social factors' zinazoleta health inequality ata makwao hilo ni tatizo sugu utakuta sehemu zinazopishana kilomita mbili tu kuna gap ya life expectancy ya zaidi ya miaka kumi uwezi kuzi ignore hizo kama causes.

Tatizo serikari yetu aifikirii kupambana na hizo changamoto wanachojua wao ni kwamba dawa ya kikoozi kata kimeo kama tiba kwenye kila kitu.

Ni hivi hii nchi kuendelea tunahitaji proper succession serikari imejaza watu wengi sana wasio na uwezo na wanaopanda madaraka kwa namna za kujipendeza lakini ubunifu ni zero na Ndalichako Phd yake inatakiwa ichunguzwe mama kwa kauli tu she is not technical mimi nakataa Ndalichako kama Phd yake ni halali.
 
Siongezi wala kupunguza ni C&P.

FB_IMG_1498163383462.jpg
 
Mkuu wa kaya aliyepita alisema watoto wa kike kubebeshwa mimba ni viherehere vyao,ila sametime naina yuko sahihi
 
Back
Top Bottom