Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

kwani alikua Bagamoyo kufanya nini?
au ndo ile one mistake 3 goals
 
Duh watakaopata mimba itabidi waende nchi jirani kuomba hifafhi na kusoma. Inasikitisha sana maamuzi ambayo sio tu yanauma lakini katika karne ya 21 yana madhara makubwa unatengeneza taifa la kesho litakalo tegemezi wasioweza kujikomboa.
 
Wazungu hawajafundisha watoto kupata mimba shuleni, wala hawatulelei watoto wetu, mzazi anamwacha mtoto na house girl, baba mlevi, familia hazina maadili, hali ngumu ya uchumi hairuhusu wazazi kuwapatia watoto mahitaji muhimu, wazazi wenyewe hawana elimu ya kutosha kwa hiyo kwa hiyo hawawezi kuwapa elimu ya uzazi watoto wao, jamii nzima imevurugika kwa umaskini...leo hii tuna mzuia mtoto wa kike kurudi shule, hapo aliyemtia uja uzito ama yupo shule pia ama hana kipato cha kueleweka ama kakataa ujauzito ule. Mtoto ambaye hana kosa lolote anazaliwa kwenye umaskini , hapo tutakuwa tume tatua matatizo au kuyaongeza?

Sio kila kitu tusingizie wazungu, hili tatizo ni ishara ya mapungufu mengi serikalini na kwenye jamii
kwanza wako wangapi. alafu statistics zinasemaje? maana wengine tumesoma mjini na watu wanakila kitu na mimba walipata. Binafsi bila kujali ni bahati mbaya au makusudi wanaweza kutafutiwa utaratibu mwingine nje ya ule ambao wengine wanaendelea nao.
 
Kuna msemo umezoeleka kusemwa pale jambo geni linapotokea au kutaka kufanyika nchi kwetu. Utasikia mtu anasema kwamba, "sio utamaduni wetu", nakusahau kuwa tamaduni zetu hazifanani (hapa hapa Tanzania) kuna makabila kukaa matiti wazi ni jambo la kawaida ila mjini waweza onekana muhuni, chizi au malaya.
Dini za kuja zimechukua nafasi ya mila, desturi na tamaduni za mtanzania kwa kiasi kikubwa leo, mfano leo hii ukisema unaabudu mti jamii itakutenga na hata ndoa yako inaweza kutofanyika. Pia baadhi ya dini Mungu ni neno tu na sio sheria tafauti na huko nyuma. Hivyo basi hapa ni kuangalia uwezekano wa kutunga sheria kuruhusu utoaji mimba nchini Tanzania.
 
Kuna watu mna vichwa vikubwa kumbe kazi yake ni kutenganisha masikio tu.mnapinga kila kitu rais kaongea ukweli mtupu
 
Da!mepitia comment karb zote kuhusu hii mada,na nimechoka kwel kwel. Lakin megundua haya hapa:
1, watu pamoja na vichwa vyao kuwa vikubwa lakin vimejaa mifupa tu akili kdogo.
2, Watanzania tumebalikiwa tu macho ya kuona mbele,lakn tumenyimwa peo za kutazama mbali..bnafs sintakaa nimuunge mkono huyu mtukufu kipenzi cha zero brain kwa hili
Kwanza najiuliza maswali haya;kwa nn kla ktu haamue yy?, bunge ni LA kaz gani..mijadala ka hii ambayo inagusa taifa zima maamuz yatoke bungen baada ya majadiriano na kupima nguvu ya hoja za pande zote.
Lakin hili suala la kukurupuka na kuja na conclusion ni kuelendelea kulichimbia taifa kaburi la hatari,..this is a blind decission,education is the right for every individual..naamni kwa asilimia nying kuwa hata bungen wapo walobeba mimba wakiwa shulen,wengne ni mawazr na wengne wana nyazifa kubwa serikalin na taasis bnafs,Mr president think critically and decide logically
Pendekezo lang,katiba ibadilishwe mpiga kura atleast awe na elim ya form four,..
Usitukane watu bila kufikiri kwa makini.
(1) Rais haanzishi kitu kipya,ndio utaratibu uliopo toka nchi hii ianze
(2) Rais ni Mkuu wa Nchi, yes jambo lolote alilolikataa Rais haliwezi kuwa sheria hata kama Wabunge wote wakitaka.Na hii ni kwa mujibu wa katiba, nchi karibu zote duniani ndivyo ilivyo.
(3) Kama Mkuu wa Nchi,Rais ndiye mzazi mkuu mwenye wajibu wa kusimamia maadili ya taifa, hii ni chachu ya kuwaogopesha wanafunzi kupata mimba na wakipata wasiwafanye wanafunzi wengine waone hilo ni jambo sahihi tu.Anaonyesha dira.
 
Kwa kua Mimi ninaamini katika misimamo mikali

Nitamuunga mkono endapo suala hilo na lamakinikia litakua kwa vitendo
 
Labda tujiulize elimu inatolewa kwa ubaguzi?
Ni haki kwa watu kupata elimu?
Kupata mimba kunazuia mtu kuelimika?

Serikali iweke shule maalumu kwa wote watakao kumbwa na hilo jambo. Hiyo tu itawafanya waone pia ni kosa.
Kuruhusu pia haina maana ndio itaruhusu mimba kwa watoto,maadili yetu bado yapo vilev ile.
Nchi yetu bado ni ya dunia ya tatu,hiyo luxury ya shule maalum za waliojifungua tunaitoa wapi?kama taifa tayari tuna mifumo ya elimu ya watu wazima ambayo elimu yake ni bei ndogo.
 
Huyu jamaa aandikiwe hotuba, kumnyima mtu elimu ni kumkatalia haki yake ya kibinadamu yale maazimio tuliyosaini yatawabana watakaotekeleza huu ujinga.

Juzi kawaponza trafiki wawili.

Hii ni sasa atakapo shinda kwa kishindo 2020 (wakurugenzi washaambiwa hakuna mpinzani kutangazwa mshindi) ... haki ni neno litakalofutika Tanzania.... hizi fedha anazojidai nazo ni kodi ya Watanzania hazijawaji kuwa zake kwanini kila siku huzitamka km zake ?? Juzi bungeni Ndugai nae kazungumza hivyo hivyo kwamba mbunge asiyeunga mkono bajeti basi asipelekewe maji au fedha za maendeleo eneo lake hivi kodi kumbe siyo yetu kwani mbunge akikataa kuunga mkono bajeti ndio kodi yao haihitajiki? Mbona wasisamehe kodi kule ambako mwakilishi haja unga mkono bajeti?
 
Tema mate chini wewe.... na wale watoto wa miaka miwili wanabakwaga gulioni??? Wanaobakwa na baba zao ni gulioni huko... fikiria kabla hujaropoka
Ninazungumzia wanafunzi. Baba kumbaka mwanaye ni USHETANI.
MTU Mzima kumbaka mtoto wa miaka miwili ni ufirauni. Adhabu zao zinajulikana.
Mjadala hapa ni wanafunzi wanaojitambua.
 
Huu mfano wa kuonesha kuwa ushoga ni kinyume na uasilia wa viumbe hai hauna tatizo na hamna njia ya kiungwana ya kuelezea tabia chafu kama hii.
Hata hivyo lakini inatakiwa lugha ya staha,

kuna maneno ya kutumia mfano kujamiiana badala ya kuto*****, sehemu za siri badala ya ku*a n.k.
 
Back
Top Bottom