Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

our no 1,leo amegusia topic muhimu mno ambaye yeye kama kawaida kaiweka kimihemko,please wana JF tujaribu kuidadisi hapa,ni kweli kila mzazi anapenda mtoto wake aelimike shuleni,

mtoto wa kike inapotokea anapata mimba why anaathibiwa yeye tu,maana anafukuzwa shule hadi yule wa kiume aliyempa mimba anaachiwa aendelee na masomo,kwangu huu ni utaratibu dume na unaendeleza ukandamizaji wa watoto wa kike,halafu baadaye tunakuja kupiga kelele ohooo mbona hatuna wasomi wengi wa kike,

kumbe wengi wao wameathiriwa na mfumo dume,solutions watoto wa kike waruhusiwe kuendelea na shule baada ya kuzaa,iandaliwe kampeni nchi nzima ili watoto wa kike wanaopenda wapigwa sindano za kuzuia mimba,na hizi zinatofautiana kutoka mwezi mmoja hadi miezi sita,ila ni lazima kila mmoja kupimwa maana zina side effects kutegemeana na mhusika,condoms zigawiwe bure mashuleni na iandamane na elimu nzuri how to use it safely,

its time noe tabia hii ya kuwafukuza shule only girls ife maana ni ya kibaguzi.
Mkuu kaongelea pande mbili ambazo kwa bahati mbaya wewe umeiongelea pande moja tu.

Mja mzito hatakiwi kuendelea na shule na yule aliyempa uja uzito anafungwa miaka 30 jela.

Anayeharibu maisha ya mtoto wa kike, haachwi akaendelea kutanua mitaani, anakwenda kuzeekea jela.

Changamoto ipo kwa baadhi ya wazazi wenye kutoa ushirikiano kwa wale wanaowapa uja uzito wanafunzi.

Umasikini wa baadhi ya familia ndio huwa pona ya hawa washenzi wanaopenda kuzifuatilia vichochoroni, sketi za wanafunzi.
 
mmmh kinachofwata kutakuwa na ongezeko kubwa la watoaji mimba.
Kwani lini wanafunzi walikuwa wanaruhusiwa kuzaa na kurudi shule? Maana yake utoaji mimba upo hadi sasa. Kuna taasisi ambazo wazazi wanarhusiwa kusoma ila rais kasema serikali yake haiwezi kusomesha wazazi. Hivyo waendelee na masomo sehemu ambazo serikali haigharimii. Hajakataza wasome.
 
Sema wewe hujaona maana yake siyo sisi! Wewe unaona ni haki mtoto akipata ujauzito asirudi shule? Kwanini anyimwe haki yake ya kikatiba ya kupata elimu, kwanini apewe adhabu mara mbili. Halafu hujui tu hii ni kwa ajili ya watoto wa masikini wanaotegemea shule za serikali
Kumbe international schools huwa mnaenda mkiwa na mimba pamoja na vichanga?
Mimba anapata msichana yoyote popote pale. Kama rate kubwa iko vijijini basi ndio maana tunashauri hatua za kupunguza hiyo rate zichukuliwe.Au utaratibu utafutwe nje ya ule wa kawaida...
 
Je kama mwanafunzi alibakwa? Je mwanafunzi akipewa ujauzito na mwalimu? Matineja wengi hawajapevuka kiakili kiasi cha kujua madhara wanayofanya. Si haki kuwanyima fursa adhimu kama ya elimu.
Ndio maana pia amezungumzia adhabu ya miaka 30 kwa yule anayemharibia maisha mwanafunzi wa kike.

Tatizo tulilonalo ni ule muendelezo wa mfumo dume kwenye jamii, unakuta Baba wa msichana analainishwa na ushawishi wa fedha au hata maneno matamu tu ya familia ya kijana aliyempa mimba msichana.

Hapo ndipo kwenye changamoto ya kupunguza mimba mashuleni, ni kuwa wakali sana kwa vijana wenye kujifanya ni marijali kupindukia.
 
hata wamama ndio wa kwanza kuficha siri za mimba za binti zao baada ya kupata ngawira baba anastuka binti kesha jifungua
 
Ndio maana pia amezungumzia adhabu ya miaka 30 kwa yule anayemharibia maisha mwanafunzi wa kike.

Tatizo tulilonalo ni ule muendelezo wa mfumo dume kwenye jamii, unakuta Baba wa msichana analainishwa na ushawishi wa fedha au hata maneno matamu tu ya familia ya kijana aliyempa mimba msichana.

Hapo ndipo kwenye changamoto ya kupunguza mimba mashuleni, ni kuwa wakali sana kwa vijana wenye kujifanya ni marijali kupindukia.
Lakini adhabu kwa mtuhumiwa haimpatii msichana fursa ya kusoma. Watu naona mna-underestimate uzito wa kauli ya kiongozi mkubwa kama rais. Kama rais anawakomesha watoto kwa kuwanyima fursa ya kusoma, wazazi wa huko kijijini ambako mfumo dume umetawala watashawishika vip kuendelea kusomesha mtoto aliyepata ujauzito shuleni?

Kwa kifupi, rais kawapa kisingizio wale wote ambao wanasomesha mabinti kishingo upande na kwa kusuasua. Lazima tukiri, japo moyoni kuwa familia nyingi (tena baba na mama) wanaona fahari sana wakizaa watoto wa kiume tu, kuliko kuzaa wa kike tu. Kwa kauli ya rais, kasumba hii ya kishamba imepata mpiga debe mkuu.
 
Dah kweli leo nimesikitika. kwani Mh. Rais hajuwi kuwa mmoja wa mawaziri wake anaowaamini alishawah kupata mimba akiwa form two? wazazi wake wasingemrudisha shule leo angekuwa wazir? Kenya mbona wanarudi tu na maadili hajaharibika? dah, any way..
 
Taifa lazima Liwe na sheria tena zile ambazo kama Taifa litajuvunia. Mimba za utotoni sio maadili yetu .huku wazungu sio wanapata mimba hizo utotoni unadhani ni Serikali. Familia. Long lived traditions. Nk wee kazana kutetea ujinga

We ndiyo unatetea ujinga sababu hujui chochote, umeishi nje unakaa kupondea traditions za wazungu, nimeishi nje miaka zaidi ya minane, US, Japan, South Korea, UK. Ukilinganisha na watanzania kwa kuangalia ratio utagundua wabongo wanapata mimba za utotoni sana kuliko hao unaosema wana maadili mabaya, ratio ya ubakaji pia ipo juu sana kwa Tz tena ukijumlisha na kesi ambazo hua hata hazifiki polisi hiyo namba inaongezeka vibaya mno. Hao unaosema wana maadili mabovu pamoja na kutembea na vimini na vikaptula vifupi hamna mwenye muda, the majority wanafanya mambo yao, hayo mavazi wanachukulia tu ka mavazi mengine sababu ya joto.

Tanzania haya maadili mnayojivunia sijui ni yapi? Yamewafikisha wapi? Maana tunaongoza kwa umasikini, mimba, ubakaji na kupiga wanawake. Hizi chuki mlizonazo kwa wazungu inabidi mtoke mkaishi nao muone watu walivyo civilized. Bongo hata kupanga foleni tu kupanda bus hamuwezi watu wanapigana hadi kuruka madirishani alafu mnasema mna maadili? Hehehehe what a joke, endeleeni kulishana propaganda na huyu kilaza muone ka mtafika popote. Uliza watu walioishi hizo nchi mnazosema hawana maadili wawape story ya jinsi watu wanavyoishi kwa kutumia akili timamu sio mmekaa na vichaa 1 kati ya 4
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Ndugu, umesahau kuwa Mwenyezi Mungu amekataza zinaa ktk vitabu Vyake,?

Yeye Magu amesema hayo ili wadogo zetu waachane na mambo ya ngono shuleni waweke akili na fikra zao zote ktk masomo.

Unadhani ingekuaje km angesema atasomesha hao watakao pata ujauzito mashuleni ?? Bila shaka wangebweteka na kuendeleza ngono zembe na hatimaye kupata c mimba tu bali hata mgonjwa ya zinaa.

Utajisikia raha gani kusikia mwanao kipenzi ameziniwa na kupewa mimba na mwalimu !?

Utajisikiaje kuona mdogo wako anaenda shule huku anatapika njia nzima kwa sababu ya mimba changa ?

Kama hutajisikia vizuri, kwanini usimkanye mapema ili amalize masomo kwanza !?

Hawa wanaojiita watetezi wa haki za binadam mara nyingi mi naona ndio wabomoaji wa maadili yetu. Chunguzeni sana mtagundua hilo.

Magu yuko sawa kabisa !!
 
Na wazaz wanachangia watoto kuwa na tabia za kishenz....
.
.mzaz inabd umfatilie mwanao nyendo zake shulen na kumbana asipate mda wa kucheza michezo ya ajab ajab
.
.zaman ilikuwa haina shida sana coz utandawaz ulikuwa haujatanda bado ila saiv inabd wazaz wabadrike waongee na watoto wao kuhus kujtambua....
.
.mzaz wa kike asitegemee kumfundsha mwanae kupika tu katka nyakat hz , LAZIMA WAZAZ WABADIRIKE ILI KUPUNGUZA MIMBA MASHULENI
NA WAZAZI WAKIUME WASIKWEPE MAJUKUMU YAO KATIKA MALEZI YA WATOTO NA KUWAACHIA WANAWAKE PEKEYAO!
 
Lakini adhabu kwa mtuhumiwa haimpatii msichana fursa ya kusoma. Watu naona mna-underestimate uzito wa kauli ya kiongozi mkubwa kama rais. Kama rais anawakomesha watoto kwa kuwanyima fursa ya kusoma, wazazi wa huko kijijini ambako mfumo dume umetawala watashawishika vip kuendelea kusomesha mtoto aliyepata ujauzito shuleni?

Kwa kifupi, rais kawapa kisingizio wale wote ambao wanasomesha mabinti kishingo upande na kwa kusuasua. Lazima tukiri, japo moyoni kuwa familia nyingi (tena baba na mama) wanaona fahari sana wakizaa watoto wa kiume tu, kuliko kuzaa wa kike tu. Kwa kauli ya rais, kasumba hii ya kishamba imepata mpiga debe mkuu.
Anayeona fahari kuzaa mtoto wa kiume kuliko wa kike analo tatizo kubwa sana la kisaikolojia. Utampata vipi mtoto pasipo uhusika wa Mama?.

Umeongelea vizuri sana mtazamo wa kiafrika, lakini nadhani faida ya uamuzi huu ni kwamba hata yule mwanaume mwenye tabia ya kuwafuata watoto wa kike, itabidi ajishauri mara mbili juu ya kifungo kinachomsubiri iwapo atampa uja uzito mwanafunzi.
 
Kuna makabila ni sugu kwa kasumba za mfumo dume. Hata wasome mpaka Mars, lakini bado 'ushamba' na ujinga wa mfumo dume hauwatoki kichwani na moyoni.

Lazima tutambue, watoto wa kiume na kike wako tofauti, hivyo lazima tujenge mazingira sawa ya fursa. Mtoto wa kiume na wa kike wanapiga game pamoja kwa siku moja, raha wanapata pamoja, lakini mtoto wa kike anapata msalaba wa kubeba mimba miezi tisa baada ya siku ile ya utamu, na miaka mpaka 5 ya kulea mtoto. Lazima serikali inayojali haki imuwekee mazingira mazuri binti ya kuendelea na masomo hata akipata mimba, na wakufanya hivyo ni serikali. Rais asisakizie mzigo wake kwa private sekta. La sivyo tutakuwa tunaulisha chakula mfumo dume bila kujua.

Kauli ya rais ipingwe popote. Iko kinyume na sheria za EAC ambako Tanzania ni mwanachama. Iko kinyume na ustaarabu na muhimu zaidi, iko kinyume na haki za kijinsia. Rais wetu ana historia ya kuongea mambo ya msingi kimzaha. Mnakumbuka alivyosema fyatueni watoto serikali sasa inasomesha bure? Je ni sahihi kuzaa tu kwa kuwa serikali inasomesha? Je watoto hawahitaji chakula? Hawahitaji matibabu?
 
Anayeona fahari kuzaa mtoto wa kiume kuliko wa kike analo tatizo kubwa sana la kisaikolojia. Utampata vipi mtoto pasipo uhusika wa Mama?.

Umeongelea vizuri sana mtazamo wa kiafrika, lakini nadhani faida ya uamuzi huu ni kwamba hata yule mwanaume mwenye tabia ya kuwafuata watoto wa kike, itabidi ajishauri mara mbili juu ya kifungo kinachomsubiri iwapo atampa uja uzito mwanafunzi.
Tatizo watu mnaamini kila anachosema rais. Hiyo sheria ya miaka 30 bila parole ipo toka miaka ya mwishoni mwa 90 na haijazuia wanafunzi kupewa mimba wala kutiwa na watu wazima wenye akili zao. Sheria haijawahi kutatua tatizo. Hata ukisema anayeiba anyongwe, bado watu wataiba tu.
 
Ndugu, umesahau kuwa Mwenyezi Mungu amekataza zinaa ktk vitabu Vyake,?

Yeye Magu amesema hayo ili wadogo zetu waachane na mambo ya ngono shuleni waweke akili na fikra zao zote ktk masomo.

Unadhani ingekuaje km angesema atasomesha hao watakao pata ujauzito mashuleni ?? Bila shaka wangebweteka na kuendeleza ngono zembe na hatimaye kupata c mimba tu bali hata mgonjwa ya zinaa.

Utajisikia raha gani kusikia mwanao kipenzi ameziniwa na kupewa mimba na mwalimu !?

Utajisikiaje kuona mdogo wako anaenda shule huku anatapika njia nzima kwa sababu ya mimba changa ?

Kama hutajisikia vizuri, kwanini usimkanye mapema ili amalize masomo kwanza !?

Hawa wanaojiita watetezi wa haki za binadam mara nyingi mi naona ndio wabomoaji wa maadili yetu. Chunguzeni sana mtagundua hilo.

Magu yuko sawa kabisa !!
Mkuu hizi taasisi za haki za binadamu huwa na siri ya kutaka kutuingizia maadili yao kwa kutumia kigezo cha jamii huru (free society).

Hawa ndio watetezi wa haki za mwanamke katika mtazamo wa usagaji (lesbians), mara nyingi huwa ni taasisi zinazoongozwa na kinamama wa makamo ambao ndoa ziliwashinda sasa wanawasukumia wasichana ile roho (spirit) ya uasi.

Maisha ya kwao ambayo msisitizo huwa ni wa ubinafsi ni tofauti kabisa na maisha ya kwetu ambayo msisitizo huwa ni jamii pana ambapo kila mtu ni mzazi au mtoto wa jamii nzima (extended family).
 
Tatizo watu mnaamini kila anachosema rais. Hiyo sheria ya miaka 30 bila parole ipo toka miaka ya mwishoni mwa 90 na haijazuia wanafunzi kupewa mimba wala kutiwa na watu wazima wenye akili zao. Sheria haijawahi kutatua tatizo. Hata ukisema anayeiba anyongwe, bado watu wataiba tu.
Lakini kumbuka zila adha azipatazo mwanafunzi mja mzito, kumbuka aina ya mtazamo anaoweza kuuambukiza darasani kwa wale wenzake ambao hawajawahi kupata uja uzito.
Ni bora kukemea mitazamo inayowakuza wanafunzi kwenye mambo ya ngono na kuweka mkazo kwenye fikra za utafutaji wa elimu.
Starehe za kimaisha mtoto wa kike atazikuta tu huko mbeleni, tena atazichoka, kwanza akili itulizwe darasani.
 
Mbona kauli kuhusu suala la mimba zinachanganya?? Waziri wa afya, makamu wa rais na rais kauli zao zinatofautiana.
 
KWA KAULI YA MH.RAIS NATAMANI HATA NIMPE ZAWADI YA KUKU TU ILA SIJUI ITAMFIKIAJE. AMENIFURAHISHA SAAANA! WOTE TUNAJUA MAPENZI NA ELIMU NI SUMU NA MSHIKA MAWILI MOJA HUMPONYOKA! WAAMUE AMA SHULE AU MIMBA!
 
Back
Top Bottom