Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Hii awamu hawajawahi kuwa na safu inayoonana. Kila mtu na lwake. Mwisho rais anatoa uamuzi unaoacha tahayari au anatumbua alieenda tofauti.

Kuna wakati humu ilisemwa mtu na makamu wake hawaelewani. Hili la mimba ni ushahidi tosha. Laiti kama inafaa kutumbua makamu!!
Inabidi walio chini yake wawe makini sana na kauli wanazotoa.
 
Inabidi walio chini yake wawe makini sana na kauli wanazotoa.
Na ameonyesha kukerwa sana na wanaotofautiana nae. Huenda waziri wa afya akaenda. Hakuna alietoa kauli tofauti nae akabaki salama. Labda kwa kua huyu alitoa kabla ya mkuu.
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Hujui unalolisema kwasababu wewe ni mtia mimba.
 
Mm namuunga mguu na mkono wasisome tena,kwani kitendo Cha serikali kuruhusu warudie masomo ni kuidhinisha ngono mashuleni
 
japo simkubali sizonje ila hili aliloliongea kuhusu ushoga ni ukweli mtupu hata wanyama hawaingiliani kinyume na maumbile
Hakuna anayekataa tatizo ni lugha ajaribu kutafuta maneno mazuri kufikisha ujumbe wake.
 
Hakika nimependa hii speech , safi mzee magu,

kwanza na mimi niliposikia habari za watoto wanaopata mimba waendee kusoma nikashangaa sana
 
Don’t be in a hurry to condemn because he doesn’t do what you do or think as you think or as fast. There was a time when you didn’t know what you know today.” — Malcolm X
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Kujiendeleza atajiendeleza lakini sio kwa mgngo wa serekali , kama hujamueeza mzee rais
 
Haya mambo huwaga hayana usawa

Mwanaume ukimpa mimba mwanafunz was kike unafungwa 30yrs

Ila mwanamke mkubwa akipewa mimba na mwanafunz wa kiume wala hakuna case..!!!

Hamshangai...!!!

Ni sawa na hapo msichana inakula kwake ila alie gawa km n dent wacha adunde tuu..ila km sio mwanafunz 30yrs inamuhusu
 
Labda mi nimemwelewa vibaya ila msingi wa mafanikio yoyote yale ni nidham
Swala la mwanafunzi kupata mimba an zen umsubiri ajifungue aje aendelee alipoishia itakua usumbufu sana zaidi ya tunavyofikiria af tutakuwa tunawafundisha nn watoto tusisahau akati si wenyew tunapinga mimba za utoton kutokana na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua
But rais sijaona aliposema mwatakuwaanafunz mjamzito hatapata nafasi ya kuendelea kusoma ila ka mzazi unauwezo unaeza mpeleka shule binafsi koz shule za serikal atakuwa amekosa sifa
Kwa kesi ya kubakwa sheria zipo
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Elimu ni haki ya kila raia wa Tanzania,awe na mimba au vinginevyo
 
Back
Top Bottom