Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Huyo jamaa mduanzi sana

Suala la wanafunzi kupata mimba mashuleni kwa asilimia kubwa linachangiwa na ugumu wa maisha unaopelekea wazazi kushindwa kuwatimizia majukumu yao watoto wao

Ww jiulize kwa nini wanaopata mimba nyingi za utotoni ni watoto wa maskini na sio matajiri

Nadhani hapo utapata jibu sahihi na utaacha kusifia upuuzi wa hilo lijamaa lisizonje
 
Hapo suala la muhimu ni kuhakikisha ajra zinapatikana kwa wingi na mishahara inatosheleza

Hii itapelekea kupunguza vishawishi visivyo vya msingi kwa hao wanafunzi maana vitu vingi kwa asilimia kubwa vitatimizwa na wazazi wao kwa wakati

Pia suala jingine ambalo serikali inapaswa kulitilia nguvu ni mikopo ya uhakika na ya kujitosheleza kwa wanafunzi ,na ukitaka kuamini hivyo ,we angalia kwa nini watoto wa kike wengi wanajiuza boom likikata ?
 
Ndio alichosema magu akibeba mimba akiwa shule ya msingi au sec akishajifungua anaweza kwenda veta au sehemu nyingine kujiendeleza na si kurudi kule msingi au sec namuunga mkono mia kwa mia tusitafute sababu kufanya watoto wetu wakaona ni kitu cha kawaida kubeba mimba akiwa na umri mdogo watakufa wengi na uzazi pia ukimwi upo tusisahau hilo tukakimbilia kuklalamikia mimba tu, pia hawa watoto wamezidi jamani wanafanyana hadi darasani wanakaliana anasogeza kichupi kijana anaingia na anamkatikia huku wenzao wapo humo humo darasani hapana jamani tusiteteee mambo ya ajabu haya
 
Hapo suala la muhimu ni kuhakikisha ajra zinapatikana kwa wingi na mishahara inatosheleza

Hii itapelekea kupunguza vishawishi visivyo vya msingi kwa hao wanafunzi maana vitu vingi kwa asilimia kubwa vitatimizwa na wazazi wao kwa wakati

Pia suala jingine ambalo serikali inapaswa kulitilia nguvu ni mikopo ya uhakika na ya kujitosheleza kwa wanafunzi ,na ukitaka kuamini hivyo ,we angalia kwa nini watoto wa kike wengi wanajiuza boom likikata ?
Sio rahisi sana watanzania wote wakawa kama uniform za shule flani, hata siku moja maisha ya mwawanadamu hayawezi kuwa sawa. Tangu zama za manabii walikuwepo masikini na matajiri. Kikubwa ni wazazi kujua wajibu wao na kuwalea watoto wao kulingana na hali ya maisha waliyo nayo.
 
Kumpeleka private ni wewe mzazi ila yeye kasema shule za bure mbona wapo wanaopata na wakasoma anachosema isiwe ni sheria yaani isipitishwe ikishakuwa ni sheria watoto hawatasoma ni kuzaa tu
 
Ugumu wa maisha unachangiwa kwa kiasi kikubwa na serikali

Kwa hiyo hata hizi mimba za utotoni lawama zinabidi ziende kwa serikali kwa kushindwa kumtengenezea mazingira mazuri mwananchi kwa ajili ya kufanya kazi na kujiongezea kipato
 
Wewe sijui unaishi dunia gani? Nani kasema wahalalishe uzinzi? Inaonekana wewe hujazaa. Subiri uzae halafu ndo uongee
Ss km unauliza nani kasema wahalalishe uzinzi mbona humuungi mkono Magu...?? Unajichanganya...hueleweki unasupport watoto kuzaa ama kutozaa
Mi niko clear watoto wasizae, wasome,Over...
 
Mkuu kuna suala la maadili mema kwa wanafunzi wa kike. Ni kulea uhuni na umalaya shuleni ikiwa mwalimu ambaye ni mwanamama anafundisha ubaoni halafu huku kwenye madawati kuna wasichana watatu ambao wananyonyesha watoto nyumbani.

Hao wasichana watatu hawawezi kumpa heshima yule mwalimu mwanamama kwa sababu ya zile akili za kusema "huyu si ni mwanamke mzazi kama sisi?". Hakuna heshima katika mazingira ya aina hiyo, na pia hakuna utii wa mkubwa kwa mdogo.

Bila ya uwepo wa utii kutoka kwa hao watatu sidhani kama hao wasichana wengine watamheshimu huyo mwalimu mwanamama.

Waende wakasome VETA, waende shule za private, waende kokote kule, lengo ni lile lile, la kurudisha heshima ya elimu.
Kwa hiyo Veta Ni Taasisi ya Elimu isiyo na Heshima? Je Na Wavulana Watakaowapa Watoto wa Kike Magufuli Atawafukuza Pia? Au ni selective justice!
 
Huyo jamaa mduanzi sana

Suala la wanafunzi kupata mimba mashuleni kwa asilimia kubwa linachangiwa na ugumu wa maisha unaopelekea wazazi kushindwa kuwatimizia majukumu yao watoto wao

Ww jiulize kwa nini wanaopata mimba nyingi za utotoni ni watoto wa maskini na sio matajiri

Nadhani hapo utapata jibu sahihi na utaacha kusifia upuuzi wa hilo lijamaa lisizonje
Wengi wa waunga mkono wa mropoko ni mabungai. Hawajui kuwa hii nchi ni kubwa. Wanayoyaona kwenye mabanda ya chips walikotongozewa wao wanadhani ndio yanayotokea nchi nzima. Kati yao hakuna ajuaye kuwa kuna wabinti wadogo sana wanaingiliwa sio kwa kuona raha bali kwa kuwa victims of circumstances.
 
Kumpeleka private ni wewe mzazi ila yeye kasema shule za bure mbona wapo wanaopata na wakasoma anachosema isiwe ni sheria yaani isipitishwe ikishakuwa ni sheria watoto hawatasoma ni kuzaa tu
Kwa hiyo shule za Private ndio Zinaenzi Uzinzi? Kama dhana ni Kuzini na Mtoto wa Kiume akimpa mwanafunzi Wenzake mimba je aruhusiweje aendelee? Au kwa muwa yeye habebi mimba! Na kumwaribia Maisha ni Faida kwa Taifa au ni Mzigo?
 
Sio Kazi yake, hiyo ni Kazi ya Wazazi
Incharge wa nchi ktk issue zote ni nani...mda mwingine sijui kwanini hamjui mnachokitaka...hujui malezi ni shirikishi ma swala mtambuka??basi wazazi wajenge shule za watoto wao km unaona hii sio kazi ya Rais
 
Kwa hiyo unataka awe in charge mpaka chumbani kwako sio,
 
Sasa mfano mwanafunzi wa shule ya kata anayetembea kilomita 8 hadi 10 ndipo afike shuleni alafu akiwa njia akirudi nyumbani akabakwa.

Je huyu akipata mimba atanyimwa kusoma???
 
Anaweza kuja na ziara ya kushitukuza katika Taasisi fulani na kuamua kumsimamisha kazi CEO wa Taasisi husika.

Anaweza kuja na uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi na akatoa hotuba itakayolenga kufunikia hii kauli yake tena ukizingatia week-end ndio hiyo inaanza.

Anaweza pia kumpiga chini mtu anaetajwatajwa kwa kashifa yoyote ile ili tu aonekane ni mzalendo na afunike hii kauli.

Anaweza kutoa tamko lolote lile litakalo wafurahisha wananchi na kuwasahaulisha hii kauli yake

Hii ndio tabia yake pale anapokose bwana huyu.

Tuliomsoma wala hatupi shida bali inakuwa ni rahisi tu kwetu kutabiri atafanya nini katika mazingira fulani.

Time will tell.
 
Back
Top Bottom