Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Nakumbuka siku moja nilikula pili pili kwenye mtori wa moto, kwa akili zangu za hovyo nikajiwahi na maji ya baridi kupoza pili pili, kumbe ndio nilikuwa nazidisha maumivu kooni.

Ukiuvagaa wa pilipili dawa ni kutulia
 
A
Mkuu bila adhabu tulizopewa utotoni pengine tusingekuwa ni watu tuliokuja kuwa na heshima utu uzimani.

Ukiondoa zile cases za binti kubakwa ambazo ni chache, nyingine zote ni zile za msichana au mvulana kwa utashi wao wenyewe kuingia kwenye mapenzi wakiwa mashuleni.



Hawa ni lazima watishwe kwa kuambiwa kwamba wanafanya starehe na wapenzi wao kwa gharama ya kuwa tayari kupoteza nafasi ya elimu bure.

Huwezi kuwa na elimu bure halafu yule anayepewa bure aamue kutoiheshimu kwa kuendekeza umalaya shuleni.

..nakuelewa.

..sijui umri wako, lakini enzi zangu shule za sekondari zilikuwa tofauti kwa wavulana na wasichana.

..naamini mazingira hayo yalitusaidia kutuepusha na vishawishi vya ngono.

..lingine lilikuwa ni marafiki niliokua nao. Wengi walikuwa makini sana ktk masomo na hawakuendekeza starehe.

..mazingira sasa hivi yamebadilika. Shule ni za mchanganyiko.
 
Nakumbuka siku moja nilikula pili pili kwenye mtori wa moto, kwa akili zangu za hovyo nikajiwahi na maji ya baridi kupoza pili pili, kumbe ndio nilikuwa nazidisha maumivu kooni.

Ukiuvagaa wa pilipili dawa ni kutulia
Huyu ni mtu wa kucheza na matukio tu soon utajionea hasa hii week-end/week hii sidhani kama itapita bila jambo kubwa kuibuliwa la kujitafutia maujiko.
 
Politics ni ngumu sana Salary Slip .

Ukimsoma Niccolo Machiavelli katika "The Prince" utaelewa kuwa sometimes wanasiasa wanatengeneza matatizo kisha wanayatatua wenyewe.This is what happening now in Tanzania.

Haya yote yanafanywa ili kuwafanya kina holoi-poloi kuwa attentive kwa Mwana sihasa na si vinginevyo.

Kwa Tanzania hiki ndicho kinachofanyika almost Mwaka mzima sasa.Yaani tunachezewa abra kadabra kibao then kazi yetu ni kushangilia tu.

Lets wake up.Twende extra mile na Tifikiri nje ya box.Politicians are always echo our minds.
 
Anaweza kuja na ziara ya kushitukuza katika Taasisi fulani na kuamua kumsimamisha kazi CEO wa Taasisi husika.

Anaweza kuja na uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi na akatoa hotuba itakayolenga kufunikia hii kauli yake tena ukizingatia week-end ndio hiyo inaanza.

Anaweza pia kumpiga chini mtu anaetajwatajwa kwa kashifa yoyote ile ili tu aonekane ni mzalendo na afunike hii kauli.

Anaweza kutoa tamko lolote lile litakalo wafurahisha wananchi na kuwasahaulisha hii kauli yake

Hii ndio tabia yake pale anapokose bwana huyu.

Tuliomsoma wala hatupi shida bali inakuwa ni rahisi tu kwetu kutabiri atafanya nini katika mazingira fulani.

Time will tell.
Na nyie mlivyokuwa watu wa kuishi kwa matukio mtatekwa kirahisi. Tayarisheni matamko tu.
 
Don't take the statement too serious. Mzee hakumaanisha kiuhalisia bali kuonyesha upande wa pili wa mjadala especially kwa wale wenye conservative ideas, as most of times hili linabebwa na liberals.

Litawekwa wazi (litafafanuliwa vizuri) ili kuondoa ukakasi, na maisha yaendelee.

Haya tuendelee na kazi ....
 
Lazima kuwe na somo mahususi.
Waalimu watoe darasa kwa wasichana kila wakati na kuwatahadharisha na mahusiano.
Watoto walindwe kwa hali ya juu kwani paedophile ni wengi na hao ndio wakutahadharishwa nao.
Na ikiwezekana waalimu wapewe majukumu ya kuwalinda kama wanao
 
Magufuli kakosea na ukumbuke yeye ni mwalimu nilitarajia ayajue hayo ya mimba nyingine za kubakwa, nyingine kulaghaiwa na wanaume sasa kachemka.
 
Kupewa madaraka ni mzigo. Ni vema akalitambua hilo. Si vema kujiona you are each and everything! Weye ndiyo weye and the only one. Uongozi ni pamoja na kuyajua matatizo ya watu. Si ubabeubabe kwa wananchi. Noooooo! Ukifanya hivyo maana yake ni kuwa hata hujui hapo ulipo umefikaje. Hafai.
 
Mbona katika hii mada sijaona mdau akizungumzia utumiaji wa condom au dawa za kuzuia mimba,si muwafundishe watoto wenu ili wasipate mimba kama mnaona raisi anawanyima haki ya mtoto wako kugegedwa? Acheni ujinga.
 
Sasa mfano mwanafunzi wa shule ya kata anayetembea kilomita 8 hadi 10 ndipo afike shuleni alafu akiwa njia akirudi nyumbani akabakwa.

Je huyu akipata mimba atanyimwa kusoma???
Ukizungumzia shule za kata kwa sasa ni nyingi labda kwa zile kata ambazo vijiji viko mbali kutoka kimoja hadi kingine, ukweli ni kwamba wanafunzi wanafanya mapenzi kwa hiari yao suala sio umaskini na sio umbali mtoto wa sister angu tulipata nae shida sana kila siku usiku yeye lazima atoroke alikanywa sana lakini wapi nikaletewa mimi na hatukumuweza na yeye alipata kila alichohitaji ili asome mwisho wa siku aliacha shule kutokana na ujauzito na hapo ni baada ya kutoa mimba mbili kwa siri akishirikiana na mama ake
 
Chips Mayai INA nguvu sana kuliko hata makatazo ya dini, maagizo ya wazazi na hotuba Kali ya Rais. Chips Mayai na fanta sijui vina nini jamani, wasichana hawasikii wala hawaambiwi kitu Mbele ya chips Mayai na fanta.
 
Chips Mayai INA nguvu sana kuliko hata makatazo ya dini, maagizo ya wazazi na hotuba Kali ya Rais. Chips Mayai na fanta sijui vina nini jamani, wasichana hawasikii wala hawaambiwi kitu Mbele ya chips Mayai na fanta.
Duh umetisha chips yai ni hatar kumbe
 
Huyo jamaa mduanzi sana

Suala la wanafunzi kupata mimba mashuleni kwa asilimia kubwa linachangiwa na ugumu wa maisha unaopelekea wazazi kushindwa kuwatimizia majukumu yao watoto wao

Ww jiulize kwa nini wanaopata mimba nyingi za utotoni ni watoto wa maskini na sio matajiri

Nadhani hapo utapata jibu sahihi na utaacha kusifia upuuzi wa hilo lijamaa lisizonje
Wewwww nani kakwambia ni ugumu wa maisha......tamaa tu za mabinti wa siku hizi hakuna lolote

Sent from my H8501 using JamiiForums mobile app
 
Assalam alaykum wanajukwaa, habari za maandalizi ya sikukuu naamini yako poa sasa twende kwenye mada

Swala la watoto wa kike kupata mimba mashule, tusilichukulie juu juu tu.

Swala la watoto kujiingiza kwenye maswala ya ngono, ni janga kwenye familia jamii zetu.

Rais aliposema kuwa wasikubaliwe kurudia masomo yaliokatizwa na mimba za kujitakia, yupo sahihi kabisa.

Na waume walioshiriki kwenye ilo tatizo adhabu zao zipo wazi na zinatumika tayari...

Kama ikitokea mtoto wa kike kubakwa, ilo linaeleweka na muanga wa kubakwa anapaswa kutoa taarifa ya huo ubakaji ili ikitokea kusababisha ujauzito, kuwe tayari na taarifa kwenye vyombo husika.

Tusipo kuwa makini na malezi na tabia za watoto zetu, watatuletea wajukuu ilihali wapo shule za msingi au sekondari, na hizi mimba si sifa nzuri kwa watoto ambao bado hawajamaliza elimu ya msingi na sekondari.

Watanzania tuna maadili yetu na dini zetu, hakuna dini hata moja yenye kukubali kuzaa nje ya ndoa, sembuse swala la kufanya ngono wakati bado watoto wanasoma.

Kwanza hili swala litamfanya mtoto wa kike kuwa makini na masomo yake na kuzuiya tamaa za kimwili na kupelekea yeye kuwa makini na masomo yake.

Kulitetea hili swala ni kutetea mzigo kwenye familia, cha muhimu ni kukaa na kuzungumza na watoto zetu, awe wa kike au wakiume na tuache siasa siasa zisizo na maana, zitatuharibia.
 
Back
Top Bottom