Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Huyu jamaa aandikiwe hotuba, kumnyima mtu elimu ni kumkatalia haki yake ya kibinadamu yale maazimio tuliyosaini yatawabana watakaotekeleza huu ujinga.

Juzi kawaponza trafiki wawili.

ikiwa kapata mimba ajisomeshe mwenyewe...wazazi wampeleke shule za Kulipia ila si shule za hela za serikali...
 
Kukaa kimya ilikua bola zaidi kuliko alichokiongea hakuna anaesarpot wanafunz kuzalishwa wakiwa shule but somebody should not be subjected to life of misery because of such mistake
 
Kukaa kimya ilikua bola zaidi kuliko alichokiongea hakuna anaesarpot wanafunz kuzalishwa wakiwa shule but somebody should not be subjected to life of misery because of such mistake

Ukiona wanaotetea hivi ujue ni mabinti wanaopenda kuzini na wanaume wanaopenda kuzini...na kuzini na mabinti wadogo....Nyie mnatetea uzinifu sio ambao hata MUNGU atawahukumu na amewalaani kwa kitendo hicho sio...

Mmegeuka shetani..
 
Kuna potokea tatizo ni vizuri pande zote mbili zi elewa madhara ya hilo kosa/tatizo. Hivyo hawa watoto/wanafunzi bila kujilinda wao wenyewe au kujua madhara ya Hilo kosa basi hatutaweza kukabiliana na matatizo mengine Huko mbeleni.
Hatua za Raisi ni ku discourage Hiyo tabia kwa watoto/wanafunzi wenyewe pamoja na kwa hao ma bazazi na kwa wazazi pia.
Huko nyuma au tofauti na hapo tunakuwa Kama tuna wa encourage hao watoto kwani mwisho wa siku si atarudi shuleni, na mzazi si ndio atamuangalia mjukuu na aliyetenda naye si ndio atasepa Zake na kwenda kutendea wengine au Huyo Huyo siku nyingine.
Hizi kauli za Raisi tusizichukulie kijuu juu.
Maana elimu bila malipo ni sawa sawa na mtaji wa maisha yako ya baadae. Sasa serakali inabana shughuli zingine iliuweze kupata elimu ikusaidie na isaidie taifa wewe , unataka usaidiwe wewe tu bila kujua kuwa nawe sehemu fulani unatakiwa kutoa kwa jamii au serikali kile ulicho pewa Huko nyuma.
 
ikiwa kapata mimba ajisomeshe mwenyewe...wazazi wampeleke shule za Kulipia ila si shule za hela za serikali...
"Hela za serikali"
Hela ya serikali ni kodi iliyokusanywa kutoka hata kwa mzazi maskini wa huyo binti.

Haya nenda katrace alichoongea Samia Suluhu, Ummy Mwalimu na ilani ya ccm juu ya mwnafunzi atakayepata mimba.
 
Nimekuelewa mkuu, ila tatizo linabaki palepale kuukemea ushoga na usagaji bila kuwa na suluhisho na bila kutatua chanzo cha tatizo hilo bado tunakua tunatwanga maji kwenye kinu, swali la msingi ni kwamba je ushoga upo? then tukishakubali upo sasa tujiulize je chanzo chake ni kipi? napia ni kwanini unakua kwa kasi? hapo sasa ndio mbinu na njia za kuzuia au kutibu tatizo hilo zitumike...nadhani tumeelewana.
Pamoja mkuu!
 
Kuna potokea tatizo ni vizuri pande zote mbili zi elewa madhara ya hilo kosa/tatizo. Hivyo hawa watoto/wanafunzi bila kujilinda wao wenyewe au kujua madhara ya Hilo kosa basi hatutaweza kukabiliana na matatizo mengine Huko mbeleni.
Hatua za Raisi ni ku discourage Hiyo tabia kwa watoto/wanafunzi wenyewe pamoja na kwa hao ma bazazi na kwa wazazi pia.
Huko nyuma au tofauti na hapo tunakuwa Kama tuna wa encourage hao watoto kwani mwisho wa siku si atarudi shuleni, na mzazi si ndio atamuangalia mjukuu na aliyetenda naye si ndio atasepa Zake na kwenda kutendea wengine au Huyo Huyo siku nyingine.
Hizi kauli za Raisi tusizichukulie kijuu juu.
Maana elimu bila malipo ni sawa sawa na mtaji wa maisha yako ya baadae. Sasa serakali inabana shughuli zingine iliuweze kupata elimu ikusaidie na isaidie taifa wewe , unataka usaidiwe wewe tu bila kujua kuwa nawe sehemu fulani unatakiwa kutoa kwa jamii au serikali kile ulicho pewa Huko nyuma.

HAHAHAHAHA halafu ujue pia watu japo wanafanya ibada lakini washasahau makatazo ya mungu na kuona ni haki yao kutenda katazo...Ukitafakari kwa kina Rais pia hapo ni moja ya Ibada anaitetea...Mungu wa viumbe vyote amekataza UZINZI. bint ambaye anafanya mapenzi kabla ya umri wake/na mwanaume ambaye si wake ni UZINZI. Je nyie binadamu mnashabikia uzinzi?
Muacheni Rais atekeleze moja ya Ibada yake, nyie Mashetani endeleeni na laana zenu. Hayo ndiyo matokeo ya laana, Ukizini utapata Mimba au Ugonjwa (Ukimwi, Kaswende, Kisonono).
Me namkubali Rais.
 
Ukiona wanaotetea hivi ujue ni mabinti wanaopenda kuzini na wanaume wanaopenda kuzini...na kuzini na mabinti wadogo....Nyie mnatetea uzinifu sio ambao hata MUNGU atawahukumu na amewalaani kwa kitendo hicho sio...

Mmegeuka shetani..
What if ikimtokea Dada ako mwanao au pengine hata we ulivokua mdogo ungejiskiaje ???? Ndo maana nkakwambia kukaa kimya ilikua vizuri zaidi pia inatakiwa kuweka mikakat madhubuti ya kuzibiti watoto wadogo kutokutana na vishawishi kama shule za boarding na kutoa elimu ya jamii kuusu kumlinda mtoto Wa kike Over!!!
 
Kwa kauli hii Magufuli amekosea sana kwa sababu suala la wasichana kuendelea na masomo baada kupata mimba ni la kisera; tena sera ya chama chake!

Pia ni lazima ieleweke kuwa serikali inaendeshwa kwa kuzingatia matakwa ya kisera, kisheria na kikanuni; na siyo kwa matamko. Tanzania is not an autocracy.

Suala la kumpatia kila mtoto elimu, tena siyo elimu tu bali elimu bora, ni la kimkakati kwa maslahi mapana ya maendeleo ya taifa. Elimu ni uwekezaji katika rasilimali watu ya taifa.

Msichana asipopatiwa elimu, kwa kisingizio chochote kile, itamuathiri yeye mwenyewe, familia yake, jamii inayomzunguka pamoja na taifa kwa ujumla.

Katika kutoa tafsiri au matamko yenye utata ya kisera ni vyema Magufuli akawaachia wahusika ambao ni mawaziri.
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.

" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Mimi huwa najiuliza tuu hivi huyo mwanafunzi apewe mimba na nani? je mwanafunzi mwenzake au mwalim wake? Binafsi naona kwa kizazi cha siku hiz kuwalegezea utakuta shule inabadilika kuwa zahanati mana wako huru
 
What if ikimtokea Dada ako mwanao au pengine hata we ulivokua mdogo ungejiskiaje ???? Ndo maana nkakwambia kukaa kimya ilikua vizuri zaidi pia inatakiwa kuweka mikakat madhubuti ya kuzibiti watoto wadogo kutokutana na vishawishi kama shule za boarding na kutoa elimu ya jamii kuusu kumlinda mtoto Wa kike Over!!!

Bora alivyokataza ili watu waogope kuliko kuruhusu mtu anaona ni haki yake kushika mimba....
Kwa mwanangu haitokei sababu wkt wote yupo ndani, akitoka shule nyumbani, kucheza cheza nje ya geti mwiko...Unakuta mzazi mcharuko, mtoto hadi saa moja usiku yupo nje anang'aa macho, shule hajulikani anatoka saa ngapi, Wazazi hawawasiliani na mwalimu kujua muda wa mtoto kutoka shule...hakuna ufuatiliaji..kwanini mtoto asishike mimba?
 
Hata kama tunatenda dhambi tusiitetee hadharani kila mmoja akaona ni haki yake kuitenda...Hadharani tuungane na maandiko ya Mungu. Uzinzi haukubaliki..Wewe mwanaume unayezini na mtoto mdogo ujue ni dhambi na si ruhusa...
 
Hapo kapotoka sana na sikubaliani naye kabisa.

Mwanafunzi wa kike kupata ujauzito siyo kosa kubwa hivyo hadi anyimwe fursa ya kujiendeleza kielimu.

Hapo adhabu haiendani kabisa na kosa!
Mkuu Nyani Ngabu, Kwa namna jamii yetu ilipofikia kwa sasa, maamuzi ya Rais ni sahihi. Wazazi wamepwaya sana kwenye malezi ya watoto wao. Pengine tusema societal set up yetu iko vibaya sana kuliko wakati wowote. Watoto wanaanza mchezo wa mapenzi mapema sana hivyo ukiruhusu hata wanapozaa warudi shule, (kitu ambacho hajiwahi kutokea katika historia ya Tanzania ) tunajichimbia kaburi sisi wenyewe.
Binafsi nimeshuhudia watoto badala ya kwenda shule wanafanya huo mchezo live ziwa Victoria wakiwa na nguo za shule huku wenzao wamewazunguka kwa kufanya uzio. Tulimwita mwenyekiti wa mtaa na taarifa zikapelekwa kwenye shule wanazosoma. Kama watoto wa form one wanafanya, kuruhusu warudi shule baadaya kujifungua litakuwa janga!

Nampongeza sana Rais kwa uamuzi huu. Wazazi tusimamie maadili ya kitanzania kuliko kusubiri mtoto apate ujauzito tukiwa na matumaini ya yeye kurudishwa shule baada ya kujifungua.

Kama kupotea basi itakuwa ni ndani ya msitu mnene!
 
"Hela za serikali"
Hela ya serikali ni kodi iliyokusanywa kutoka hata kwa mzazi maskini wa huyo binti.

Haya nenda katrace alichoongea Samia Suluhu, Ummy Mwalimu na ilani ya ccm juu ya mwnafunzi atakayepata mimba.
Una uhakika hela yako ya kodi unayotoa inatosha kwa huduma zote za jamii unazopewa na serikali???
 
Back
Top Bottom