Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Pes yangu inayokusanywa inaendana na huduma ninazopata?

hela yako haitoshi hata theluthi yake....hiyo ni sawa na ile kumwambia mzazi ntakulipa gharama zako ulizonilea zote wkt huwezi hata chembe...
 
Ndio keshasema sasa, kilichobaki tusubiri akimaliza muda wake wa uongozi ndio tuwarudishe mashuleni waliopata ujauzito.
 
hela yako haitoshi hata theluthi yake....hiyo ni sawa na ile kumwambia mzazi ntakulipa gharama zako ulizonilea zote wkt huwezi hata chembe...
Mh upo serious? Una basic knowledge ya Public Finance?
 
Nimekuelewa mkuu, ila tatizo linabaki palepale kuukemea ushoga na usagaji bila kuwa na suluhisho na bila kutatua chanzo cha tatizo hilo bado tunakua tunatwanga maji kwenye kinu, swali la msingi ni kwamba je ushoga upo? then tukishakubali upo sasa tujiulize je chanzo chake ni kipi? napia ni kwanini unakua kwa kasi? hapo sasa ndio mbinu na njia za kuzuia au kutibu tatizo hilo zitumike...nadhani tumeelewana.
Kutatua ni kuwatia mbaroni mashoga wote....wao wanaokuza tabia hii chafu
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.



" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.

Tujifunze kutatua tatizo na siyo kukimbia tatizo Mwaka 1978 nilipokuwa form two Mwalimu wetu wa biology kwenye topic ya 'evolution of a man' alituambia itakapo fika mwaka 2000 mtoto wa kike atavunja ungo akiwa na miaka 10-12
Hapa ina maanisha mtoto wa kike anapevuka mapema sana Hili ni tatizo la jamii zetu kukosa maadili
 
Mh upo serious? Una basic knowledge ya Public Finance?
Madhara ya Zinaa na jinsi ya kujiepusha nayo:

UTANGULIZI

"Amrishaneni mema na katazaneni mabaya kwani hii ni dawa yenu; lakini pindi mtakapoacha kuamrishana mema na kukatazana mabaya itakujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni na wakati huo mtaomba nusra na hamtakubaliwa".

H adithi hii inaelekezwa kwa wanadamu wa aina yoyote duniani. Jambo hili la kuamrishana mema na kukatazana mabaya iwe ni kazi yao, kwani ni dawa kubwa kwa sababu kuamrishana mema na vilevile kukatazana mabaya kunaleta kheri kubwa sana, na kheri hizi zikipatikana, ulimwengu unakuwa salama. Na mambo haya mawili yakikosekana katika ulimwengu bila shaka itatujia balaa katika hii ardhi na ienee kila sehemu.

Kwa maana hiyo basi, ndugu zangu Waislamu kutokana na jamii zetu kuathirika vikubwa mno na ZINAA basi yatupasa sisi Waislam tukumbushane na kuelimishana kuwa swala hili la zinaa sio la kufanyia mchezo. Kwani Allah (S.W.) alishatuambia mapema katika surat - ISRAA aya ya 32:

"Na wala msikaribie (msifanye uchafu wa) zinaa, hakika huo ni uchafu (Mkubwa) na ni njia mbaya kabisa."

Hapa Mwenyezi Mungu (S.W.) anatukataza kuikaribia tu zinaa licha ya kufanya hicho kitendo chenyewe cha uchafu mkubwa auchukiao Allah (S.W). Na imeandikwa kuwa, mwanadamu kwa kila sehemu yake ya kuzini atapata (dhambi) na hizo hana budi nazo (ikiwa yeye ni mwenye tabia hii chafu). Kwani macho - kuzini kwake ni kutazama visivyokuwa halali kwake (ayanusuru Mwenyezi Mungu macho yetu kuangalia vya haramu). Masikio zinaa yake ni kusikiliza yasiyo halali. Ulimi zinaa yake ni kusema (maneno) machafu ayachukiayo Allah wetu (S.W). Mikono zinaa yake ni kutesa (kushika) visivyo halali yake. Miguu zinaa yake ni kwenda kwenye jambo chafu lisilo la halali; na moyo unaanguka na kutamani, na unasadikisha haya utupu au unamkadhibisha.
Juu

Haya ndio mambo au tabia inayomvutia mtu mpaka anaangukia katika kuzini, ndio maana Uislam unakataa kabisa kuchanganyika Wanaume na Wanawake pamoja ikiwa kama hawatazishinda nafsi zao. Na kuifuata nafsi inavyotaka ni hasara kubwa sana kwa Muislam na siku zote nafsi inaamrisha machafu, kwani Saydna Ali (r.a) alishatuambia kwamba "tukiitaka pepo lazima tuikandamize nafsi". Na Mtume Muhammad (S.A.W) anasema:
"Ikidhihirika zinaa na riba katika ardhi basi wamejihalalishia (wamejitakia) wenyewe nafsi zao adhabu ya Mwenyezi Mungu".

Tukilinganisha hadithi hii ya mtume wetu (S.A.W) na ulimwengu ulivyo sasa, tunaona wazi kabisa kwamba tumeshapata adhabu za Mwenyezi Mungu tukiwa hapa duniani kabla hatujafika popote pale. Na pia Mwenyezi Mungu anasema: "tutawapelekea maradhi huenda hawa watu watarudi nyuma (watatubia) na mimi nitawasamehe".

Leo hii Mwenyezi Mungu ameleta maradhi ya aina mbalimbali na misiba mingine mingi inayosababishwa na zinaa ili tupate kuzinduka na kuona kwamba zinaa sio swala la mchezo na ni lazima tujiepushe nalo kwa kila hali. Lakini kuna watu wasiojali maamrisho ya dini nao wameleta condom ili kujikinga na haya maradhi ya zinaa na vilevile kuzuia wanawake wasiweze kupata mimba na kuendelea kufanya zinaa. Msiba ulioje huu?
Mtume (S.A.W) anasema:

"Hakika hazini mwenye kuzini (mtu) ila wakati wa kufanya kitendo kile cha zinaa huwa hayupo katika Uislam"

Hii ni kwa sababu nafsi yake inakuwa haina raha kutokana na jambo analolifanya ambalo ni kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Mtume Muhammad (S.A.W) akaulizwa "Jee baada ya kumaliza unarudi Uislam wake?" Mtume (S.A.W) akajibu "Unarudi Uislam wake lakini kwa kazi kubwa" kwanza kwa kujijua yumkosa na kutubia toba ya kweli kweli.

Juu

Kwa kuzingatia hadithi hii, yatupasa kuchukua tahadhari kubwa kabisa. Uhai wa mwanadamu unaweza kukatika wakati wowote na mahali popote. Hivyo mwenye kuzini anaweza kufikwa na mauti wakati anatenda jambo hili chafu. Na mwenye kufa katika mazingira hayo atakuwa amekufa NJE YA UISLAM. Ni hasara iliyoje kwa mtu huyo?

Ndugu Muislam ikiwa wewe unayo hii tabia chafu, basi kabla hujaenda kufanya hivyo tena, jikumbushe kuwa wewe HUNA MKATABA NA ALLAH (S.W) JUU YA UHAI WAKO. JE UNA UHAKIKA GANI KWAMBA MAUTI HAYATAKUFIKA UKIWA KATIKA TENDO HILO OVU ?.

Hadithi hiyo inamaliza kwa kutufahamisha kuwa mtu (aliyemaliza kuzini) hurejea katika Uislam kwa kufanya TOBA YA KWELI.

Lakini toba ya kweli haipatikani ila kwa mtu.

Kujutia kosa lako
Kutia nia ya kutolirudia kabisa
Kuomba maghfira (msamaha) kwa mola wako.

Hivyo mtu akifanya toba ya kweli hawezi kuzini tena.

MAJANGA YATOKANAYO NA ZINAA

Mwenyezi Mungu ametukataza kukaribia zinaa kwa njia yoyote ile, kwani zinaa humtoa mtu katika imani na ni uchafu mkubwa kabisa. Kwani Mtume (S.A.W) alisema

"Haienei zinaa na uasherati katika jamii ila itaenea kwao vitu viwili (mauti na magonjwa yasiyojulikana)". Ukiangalia hadithi hii, utaona ni kweli kabisa kwani mara nyingi mtu mzinzi mambo haya yanamkuta mfano magonjwa yasiyokuwa na dawa wala kujulikana na vifo vya ghafla inakuwa ni kawaida. Miongoni mwa madhara ya zinaa ambayo leo hii yanaitaabisha jamii ya mwanadamu ni kama ifuatavyo:-

Hili ni gonjwa lenye mateso ya hali ya juu lenye kufedhehesha wagonjwa na kuidhikisha jamii. Wataalamu wa tiba katika kona zote za dunia wamekuwa wakihangaika bila ya mafanikio, katika kutafuta dawa za kutibu na/au kuukinga ugonjwa huu. Aidha kumekuwepo "Lundo" la kampeni za kuwaelimisha watu juu ya Ukimwi. Mambo yote haya yanagharimu mamilioni ya pesa. Lau kama mwanadam angeachana na uchafu huo wa zinaa, basi pesa zote hizo zingetumika katika mambo mengine ya kuufaa umma huu. Kwa upande mwingine watu wengi wanaopata AIDS hudhoofu sana kiasi cha kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali. Hali hii, inaelekea kupunguza pato la Taifa na pia kuongeza idadi ya wategemezi (dependants). Yote haya yanapelekea kuzidi kuporomoka kwa uchumi.

Juu

Zinaa inapelekea kupatikana kwa watoto wasiokuwa na baba rasmi. Mama za watoto hawa, huwatelekeza ama kwa kuona aibu au kwa kukosa uwezo wa kuwatunza, baada ya baba za watoto kukana kama sio wa kwake au kukosa kufahamika kwa baba za watoto ni yupi ikiwa huyo mama ni "Kiruka njia".

Hatimaye utaona watoto hawa wakishakuwa wakubwa, huwa hawajui baba zao na pia wanakosa nasaba (ukoo). Juu ya hayo, hatutegemei kheri yoyote kutokana na watoto hao toka kwa Mwenyezi Mungu kwa vile wamekuja katika njia ya haramu.

Watoto hao leo hii wamekuwa ni KERO kwa jamii, udokozi, ubakaji, ujambazi, ukibaka, uchafuzi wa maeneo (vinyesi) na kero nyingine zimekithiri.

Vilevile hivi sasa Ulimwengu mzima unapiga kelele kuhusu suala la ongezeko la watu duniani. Kwa kweli ni lazima tuwe wengi, kwa sababu zinaa imezidi mno kila pembe ya dunia, utakuta mwanamume mmoja ana wanawake wa nje ya ndoa wasiopungua sita na wote hawa wanamzalia watoto. Jee baada ya miaka kadhaa ijayo hatujawa wengi? Ongezeko hili la watu, linakuwa ni mzigo kwetu kwa vile halina baraka za Allah (S.W).

Mume mwenye tabia ya uzinifu, hupumbazika na kumezwa na hao vimada wake. Hivyo, huitelekeza familia yake akiwaacha mke na watoto wakitaabika. Baadhi ya watoto wameshindwa hata kumaliza masomo yao, na hao akina mama waliotelekezwa hujitumbukiza katika biashara chafu mfano uuzaji pombe na ukahaba.

Dada zetu kadhaa wamepoteza hadhi (murua) zao baada ya kubainika kuwa wamekuwa ni "Viruka Njia" (Wazinifu) kiasi cha kutopata waume wa kuwaoa. Zaidi ya hapo akina dada hao wamepoteza fursa za kuendeleza vipaji vyao na kuikosesha jamii wataalam wa kike na walezi NAMBA WANI wa familia.

Kadhalika akina dada waliowahi kuolewa wamepoteza ndoa zao baada ya kubainika kuwa hawakuwa waaminifu katika ndoa zao yaani walizini wakiwa ni wake za watu.

Ndugu Waislam, haya ni baadhi tu ya madhara ya zinaa katika jamii yetu ambayo kwayo sote tupate uchungu na kuipiga vita.TUSIIKARIBIE !!

Tunasema kuwa haya ni baadhi tu ya madhara kwa vile Allah (S.W) ndiye mjuzi zaidi.


MAMBO YENYE KUENDELEZA/KUCHOCHEA ZINAA.

Ndugu Waislam, haitoshi kabisa kusema tu kuwa zinaa mbaya pasi na kujaribu kubainisha mambo yenye kuifanya zinaa iendelee kuwa katika jamii yetu. Mambo hayo ni (Allah a'alam).

Juu

Mavazi kwa njia moja au nyingine hupelekea mtu kujikuta ameingia katika janga hili la zinaa.

Kwa kweli tukiangalia mavazi ya wanawake yanasikitisha mno; hasa wanawake wa Kiislam kwani ndio Mwenyezi Mungu aliowatolea amri kuwa wasidhihirishe viungo vyao (wajisitiri miili yao). Lakini sasa hufanya kinyume na amri yake Allah (S.W), kwani wanawake hawa wa kiislam huvaa mavazi yasiyo na stara wala heshima, hivyo basi mavazi yao huwa hayana tofauti kati yao na makafiri. Na Mtume (S.A.W.) kasema,

"Wanawake wamevaa mavazi ya uchi wameelemea (kupenda mavazi yasiyokuwa na stara), vichwa vyao vimeinama kama nundu ya ngamia, hawataingia peponi wala hawatapata (hata) harufu yake".

Na hivi leo wanawake wa Kiislam ndio wazivaazo nguo zisizo na stara, na hii ndio inayosabababisha watu kuangukia katika zinaa. Kwani pindi mwanamume akimuangalia mwanamke ambaye hana stara ya mwili wake, basi ni lazima mwanamume huyo ataingiwa na matamanio mabaya ya kuzini. Hivyo ni hasara kubwa mno iwapo mwanamke wa kiislam ataacha kuusitiri mwili wake kama alivyoamrisha Allah (S.W) katika Quran (Surat An-nur aya 031)

"Na waambie Waislam wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika. (Na ni uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao au wanawake wenziwao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume (watumwa wao) au wafuasi wanaume wasiokuwa na matamanio (kwa wanawake) au watoto ambao hawajajua mambo yaliyohusu uke. Wala wasipige miguu yao ili iwajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao. Na tubieni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waislam ili mpate kufaulu".

Juu

Kuchelewesha ndoa:-

Bahati mbaya leo hii kumekuwa na tabia ya kutowaozesha vijana mapema. Tabia hii inapingana na hadithi ya Mtume Muhammad (S.A.W) ambaye alisema kuwa vijana wanapobaleghe basi mipango ifanyike mapema (haraka) ya kuwaoza. Leo hii zipo sababu ambazo kisheria katika Uislam si za msingi kuchelewesha ndoa; miongoni mwa sababu hizo ni kama ifuatavyo:

Kutoza mahari kubwa.

Utakuta wazazi / walezi wa binti wanamzuia binti yao asiolewe na kijana fulani (Muungwana) kwa vile kijana huyo ameshindwa kulipa mahari (fedha) kubwa aliyotakiwa. Hebu tujiulize, hivi hiyo mahari kubwa kama ikilipwa ndiyo itamuwezesha binti yao aishi maisha yake yote ya ndoa bila kutindikiwa?

Baya zaidi ni kuwa wazazi hao wanashindwa kumzuia binti yao asizini na huyo mchumba au mtu mwingine yeyote.

Kumtaka kijana (Mwanamume) "ajijenge" kimaisha kwanza.

Wazazi au walezi wamekuwa wakimzuia kijana wao kuoa mapema wakidai "bado hajajijenga" lakini wazazi au walezi hao, hawana namna ya kumzuia kijana huyo "asirande rande" na wanawake

.

Kuwasubirisha vijana wamalize masomo

. Wazazi wamekuwa hawataki watoto wao wasichanganye masomo na mambo ya kuoa au kuolewa. Lakini wazazi hao, wanasahau kuwa watoto wao wamekwisha kua, na pia matamanio ya jimai (sexual appetite) ni sehemu ya maumbile yao. Leo hii, asilimia kubwa ya wanafunzi katika shule na vyuo wanaojishughulisha na ngono (sex) kabla ya ndoa inaongezeka. Serikali inatambua ukweli huu na ndio sababu imeruhusu kugawiwa kwa "Condom" mpaka mashuleni, na sasa hivi imekwishapitisha utaratibu wa kuwawezesha mabinti watakaopata ujauzito wakiwa mashuleni, kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Ni vipi basi kama mambo ndiyo hayo wanafunzi hao wasiruhusiwe kuoana ili ipatikane kheri toka kwa Allah (S.W)??.

Juu

Kutoenziana (kutojaliana) kati ya Mume na mke:-

Kumekuwa na tabia isiyopendeza na ni nje ya Uislam ya mume na mke kutoenziana. Kila mmoja anajifanya "Kutingwa" na mambo yake binafsi. Tabia hii, hupunguza sana mahaba baina ya mume na mke na hata kupunguza hamu ya jimai kati ya wawili hao. Huu ndio mwanzo wa "nyumba ndogo" kwa wote wawili yaani mume na mke.

Hebu turejee hadithi ya Mtume (S.A.W) aliposema:-

"Mwanamke anapoitwa na mumewe basi afanye upesi kwenda kumsikiliza (asijizungushe zungushe au kuuahirisha wito huo)".

Na katika hadithi nyingine Mtume (S.A.W) amewahimiza wanaume "kucheza cheza" (kufanya masikhara na kuwa karibu kabisa na wake zao).

Kutovumiliana katika maisha ya ndoa:-

Mume na mke, kama wanadamu, kila mmoja ana kasoro zake. Hivyo ni jambo la kawaida kwa mume au mke kumkosea mwenzi wake. Pakikosekana kuvumiliana na kusameheana, ndoa huwa mashakani na hata kuvunjika.

Ndoa inapovunjika ni hatari sana kwa mtu aliyezoea maisha ya ndoa kukaa bila ya mume au mke. Hivyo kuvunjika kwa ndoa, humweka mtu katika mtihani mkubwa wa kutumbukia katika uzinifu. Mtume Muhammad (S.A.W.) alipata kusema:

"Mwanamke atakayevumilia usumbufu wa mumewe (kwa ajili ya Allah) basi Mwenyezi Mungu atamlipa mwanamke huyo malipo sawa na yale aliyomuahidi Bi Asiyah mkewe Firauni".

Ama katika hadithi nyingine Mtume (S.A.W) alisema,

"Mwanamume atakaye vumilia usumbufu wa mkewe (kwa ajili ya Allah) basi Mwenyezi Mungu atamlipa mwanamume huyo malipo sawa na aliyomwahidi Nabii Ayub". Kadhalika katika hadithi nyingine yenye kuonyesha ubaya wa kutalikiana, Mtume (S.A.W.) amesema:

"Katika halali zote alizoziumba Allah (S.W) hakuna halali aichukiayo (yeye Allah S.W) kuliko talaka".

Juu

Watoto kukosa ukaribu wa wazazi wao:-

Ni katika hulka ya mwanadamu kutaka kuonyeshwa huruma, mapenzi na kipaumbele na wanadamu wengine. Na hivi ndivyo ilivyo kwa watoto ndani ya familia. Mtoto huyategemea hayo toka kwa wazazi wake.

Wanasaikolojia wamegundua kuwa mtoto anapoukosa "Ukaribu" huu toka kwa wazazi wake au ndugu zake wa karibu (mfano kaka na dada) basi nafsi yake humlazimisha kuutafuta "Ukaribu" huo toka kwa watu wa nje ya familia. Hatua hii ikifikiwa huwa ni jambo la hatari sana. Mabinti wengi "wameharibikiwa" pale walipolazimika kutafuta huruma, mapenzi na kipaumbele toka kwa watu wa mbali baada ya kukosa hayo toka kwa baba zao na kaka zao. Utakuta baba hana kabisa wasaa wa kukaa na kuzungumza na binti yake au kwenda matembezini pamoja naye.

Historia ya maisha Mtume (S.A.W) inatuonyesha ni jinsi gani Mtume (S.A.W) alikuwa akionyesha mapenzi ya hali ya juu kwa binti yake Bi. Fatma (r.a) tena ingawa Bi Fatma (r.a) alikuwa tayari amekwishaolewa. Na kuwa Mtume (S.A.W) alipokuwa akitembelewa na Bi Fatma (r.a) basi Mtume (S.A.W) alikuwa akisimama na kwenda kumlaki bintiye, akiuchukua mkono wake na kumbusu kumkaribisha nyumbani. Naye B i Fatma (r.a) ali kuw a akifany a hivyo hivyo alipotembelewa nyumbani kwake na Mtume (S.A.W.).

Mazungumzo na vitendo vya jimai kuonekana Hadharani.

Yapo magazeti, majarida na pia kanda za video ambapo kila kimoja huzungumzia na kuonyesha picha zenye kuhusiana na ngono (jimai). Aidha maduka ya pombe (Groceries) ambayo yamechipua kama uyoga katika maeneo ya makazi ya watu ni kichocheo kikubwa sana cha zinaa. Mtu anapolewa hutokwa na 'haya' na hivyo, kufanya lolote bila ya aibu. Wanywaji wake kwa waume katika maduka ya ulevi wakishalewa huanza kushikana shikana na kukumbatiana mbele ya wapita njia na wakazi wa sehemu hiyo wakiwemo watoto. Matendo hayo, huwafanya watoto wadogo (ambao kwa asili ni wadadisi) kutaka kujua 'kulikoni'. Katika huko kukumbatiana matokeo yake ni zinaa kukua mpaka kwa watoto, Mwenyezi Mungu atulinde sisi na vizazi vyetu.

Juu

Kuchanganyika wanawake na wanaume:-

Yapo matukio kadhaa ambayo hupelekea kuwepo michanganyiko hii ya wanaume na wanawake ama si mume na mke au hawana uhusiano wa damu (kwa kuzaliwa na/au kunyonya).

Matukio hayo ni kwa mfano sherehe na sehemu za kazi. Baya zaidi wanawake "hujiachia" kwa kuvaa nguo zisizofunika mwili wote na zenye kubana pia kwa kujitia manukato.

Labda tuweke wazi jambo moja ambalo huenda baadhi ya wanawake hawalifahamu. Ingawa matamanio ya jamii yapo kwa wote wanawake na wanaume, kasi ya kuyaamsha matamanio hayo inatofautiana. Mwanamume huchukua muda mfupi sana kupandwa na hayo matamanio kuliko mwanamke. Matamanio ya mwanaume huweza kuamshwa kwa kuliona tu umbile la mwanamke na hata kwa kunusa harufu (ya manukato) aliyojitia mwanamke huyo. Ndani ya dakika chake tu akili ya mwanamume huanza kuwaza "mengine".

Na ukweli huu makahaba wanaujua vizuri na wanaufanyia kazi. Anavaa nguo fupi, nyepesi na katika mkoba wake hakosi manukato ambayo hujupuliza kila baada ya muda kuhakikisha kuwa anaendelea "kunusika kimahaba" akipita mbele ya mwanamume.

Je tunategemea nini ikiwa mwanamke aliyevaa "uchi uchi" na kujifukiza marashi amekaa kando ya mwanamume au haishi kupita pita mbele ya macho ya wanaume huko maofisini au katika tafrija na sherehe za harusi? Bila shaka ni kuongezeka kwa zinaa.

Masheikh kushiriki zinaa.

Wapo watu ambao jamii huwaona kuwa ni wasomi wa Uislam, waswalihina na hivyo ni wacha- mungu, lakini wamekuwa washiriki zinaa kwa namna moja au nyingine. Watu hao ni kama vile Maimamu, Walimu wa madrasa, viongozi wa vikundi au taasisi za kiislam na Ma-Alhaji.

Hivyo watu huleta hoja kuwa "Ikiwa mcha-Mungu fulani ana kimada au anatembea na mke wa mtu fulani, Je mimi mtu wa kawaida tu nitaweza kuyaacha hayo mambo?"

Lakini ukweli ni kwamba tunasahau kuwa hao tunaowaona kuwa ni wacha- Mungu ni binadamu wenye udhaifu wa nafsi kama binadamu wengine. Pia sisi tunatakiwa kuiga mwenendo wa Mtume (S. A.W.) na siyo kumuiga Sheikh fulani na Sheikhat fulani, Ustaadh au Ustaadhat fulani. Allah (S.W) anatueleza katika Qur'an Tukufu:

"Bila shaka mnao mfano mwema (wa kuiga) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na kumtaja Mwenyezi Mungu sana" (33:2.)

Juu
KUJIKINGA NA (KUUTOKEMEZA) UCHAFU WA ZINAA

Ndugu Waislam yapo mambo kadhaa ambayo tunaweza kuyafanya ili kuzikinga nafsi zetu na pia nafsi za jamaa zetu, dhidi ya uchafu wa zinaa. Kwa ujumla yatupasa KUKUZA IMANI ZETU NA KUINGIA KATIKA UISLAM WOTE.

Yafuatayo yanaweza kukuza imani iwapo tutayafanya kwa dhati.

Unyenyekevu katika sala.

Tuzidishe unyenyekevu (utulivu wa fikra na mazingatio ya juu) katika sala zetu za kila siku kwani Allah (s.w.) alikwisha sema kuwa hakika sala ikisaliwa vilivyo (kwa mazingatio) humzuilia mtu (huyo mwenye kusali) na maovu na machafu.

Tuzidishe sala za Sunnah.

Jambo hili litatuongezea fursa ya kumkumbuka Allah (S.W.) mara nyingi zaidi katika siku na hivyo kusaidia "kufuta" fikra chafu mara zinapotuingia.

Kufunga funga za Sunnah.

Kwa mtu ambaye hajaoa au kuolewa, au kwa yule aliyeoa au kuolewa lakini yuko mbali na mwenzi wake ajiwekee utaratibu wa kufunga saumu za Sunnah mfano kila Jumatatu ma Alhamisi. Mtu mwenye saumu humkumbuka Allah kwa karibu zaidi . Aidha saumu huulegeza mwili wa mtu aliyefunga na hivyo kupunguza nguvu ya matamanio ya ngono.

Mwanamke na Mwanamume Ajnabi wasikae Faragha.

Mwanamke na Mwanamume ambao sheria inawaruhusu kuoana waepuke kukaa faragha wakiwa wawili tu. Mtume (S.A.W.) alitutanabaisha juu ya mwendo huu wa hatari aliposema:

"Hawakai faragha watu wawili mwanamke na mwanamume wasio maharimu isipokuwa watatu wao ni shetani (ambaye yupo tayari kuwashawishi wazini)".

Tahadhari kubwa zaidi iwepo ikiwa wawili hao wamekwishafunga uchumba kwa vile:

Juu

Kila mmoja anapomuona huyo "mtarajiwa" wake mbele yake hamu yake ya ngono huchemka zaidi.

Ni rahisi kwa kila mmoja wao kujifanya "laini" kwa mwenzie kama dalili ya kuonyesha anampenda.

Stara ya mavazi kwa akina dada:-

Mtume (s.a.w.) ametufundisha kuwa mwili mzima wa Mwanamke ni "kitamanisho" (Kivutio cha jimai) kwa mwanamume. Kadhalika sauti yake akiitoa kwa ulegevu, mapambo aliyojikwatua na manukato vyote ni vyenye kumtamanisha mwanamume.

Hivyo akina dada mnapotoka au kuwa mbele ya wanaume wasio maharimu kwenu sharti mjifunike mwili wote isipokuwa uso na viganja vya mikono, msiyadhihirishe mapambo mlioyachukua na msijitie manukato.

Jifikirie Utajisikiaje wewe ukifanyiwa ubaya:-

Unapokusudia kuzini kwanza tafakari utajisikiaje iwapo tendo hilo atafanyiwa jamaa yako wa karibu mfano mkeo, binti yako, dada, mama, na wengineo

. Allah (S.W.) anatuasa kuwa tunapoazimia kufanya jambo tuzingatie akilini mwetu jinsi tutakavyojisikia iwapo jambo hilo watafanyiwa jamaa zetu. Mfano: Katika Qur'an (4:9) Allah anamuusia yule aliyeachiwa dhamana ya mali ya urithi, kuwa awatendee haki watoto yatima (wenye haki na mali hiyo). Kwa vile bila ya shaka yeye mwenyewe (msimamizi wa hiyo mali) iwapo angekuwa amefariki na kuacha watoto, angependa waliobaki wawatendee haki wanae aliowaacha duniani

Malezi ya Watoto:-

Wazazi walezi wawafundishe watoto wao kumjua na kumuogopa Mwenyezi Mungu katika mambo mbalimbali kulingana na umri wao:

Watoto wasipewe fursa ya kucheza (kushiriki) makundi yasiyoeleweka (japo ni ya watoto wenzao).

Watoto wajengewe mazoea ya kutulizana nyumbani na kujisomea/kudurusu.

Watoto washirikishwe katika shughuli za nyumbani, mfano:- Usafi wa mazingira, Utunzaji wa bustani, upishi/mapishi n.k. Mambo haya yataishughulisha akili ya mtoto na hivyo akili yake haitopitiwa na "fikra chafu chafu".

Juu

Uwepo utaratibu wa kutoka (kwenda matembezini) na watoto wenu, kutembelea sehemu za asili na pia familia zenye maadili mazuri. Kwa vile mwanadamu hujenga mapenzi miongoni mwa wale anaowafahamu, watoto wenu Inshallah watatokea kujenga mapenzi kwa watoto wenziwao wa familia hizo zenye maadili mazuri. Utaratibu huu, utapelekea hata mwanenu kupata mchumba mwema (mcha-Mungu) kutoka miongoni mwa watoto wa familia hizo.

Watoto wakifikia umri wa kubaleghe ambapo hutokewa na mabadiliko ya kimaumbile na kupata matamanio ya jimai, basi wafundishwe namna na umuhimu wa kujizuilia mpaka pale mtu atakapooa au kuolewa.

Wafundishwe:-

Umuhimu wa ndoa
Wajibu wa mume na mke katika ndoa
Hadhi kubwa ambayo Uislam umeipa ndoa.
Njia za kisheria za kukabiliana na matamanio
Hasara anazoweza kupata mtu hapa duniani kwa kushiriki zinaa
Adhabu hali ambazo amewaandalia wazinifu.

Wakati huu ni wa hatari sana na kijana anatakiwa kupata mtu sahihi wa kumfunza na kumuongoza. MZAZI ndiye hasa anastahili kufanya kazi hiyo. Mama amfunze binti yake, na baba amnfunze kijana wake wa kiume. Wakikosekana hao basi mwalimu wa kike ambaye ni Muislamu na mwadilifu, apewe jukumu la kumfunza binti yako.Aidha mwalimu wa kiume Muislam na mwadilifu amfunze mtoto wako wa kiume.

Ifahamike kuwa sasa hivi kumejaa fikra potofu nyingi, mfano watoto wetu wanadanganywa kuwa kijana asipokuwa na rafiki (mpenzi) ambaye watajaribiana na kuzoeshana ngono, basi kijana huyo, atapata tabu atakapooa au kuolewa, na hivyo kuhatarisha ndoa yake. Hivyo, wazazi au waalimu hao ni sharti kuwa wazi zaidi juu ya masuala haya kwa vile vijana wengi huwa wanaghilibiwa.

Juu Watoto wakumbushwe kuwa:-

Allah anayajua yote tuyafanyayo dhahiri na yale tunayoyaficha.
Haiwezekani Mwenyezi Mungu ambaye ndiye aliyetuumba na hivyo anatufahamu vilivyo atuzuie jambo (uzinifu) ikiwa kweli jambo hili lina manufaa kwetu.

Ili jambo hili la kuwafunza watoto (wa umri wote) lifanikiwe, lazima wazazi/walezi waonyeshe mfano wa utii wa hali ya juu kabisa kwa sheria za Mwenyezi Mungu. Mfano watoto wawaone wazazi wao wanachunga nyakati za swala na wanaswali kwa unyenyekevu, hawatumii lugha chafu (hata kama wamekasirika) kumkemea mtoto au mtu mwingine yeyote aliyekosa, na wazazi hao wanasoma (durusu) Qur'an mara kwa mara.

Kwa mujibu wa yale yote yaliyotajwa awali kuwa ni yenye kuchochea zinaa katika jamii yetu, mambo yafuatayo yanafaa kuzingatiwa kama njia za kupambana na zinaa.

Ndoa zihimizwe na ziharakishwe.

Visingizio vya kuchelewesha ndoa kama vile kutoza mahari kubwa, au, eti vijana wangali shuleni havina msingi. Wapo wanafunzi wengi waliofunga ndoa wangali wakiwa masomoni na wamemaliza masomo yao salama salimini. Hakika ndoa iliwapa utulivu.

Ikiwa wanafunzi hao hawajawa na nguvu ya kiuchumi, basi familia ya mume na ile ya mke kwa pamoja zinaweza kufanya utaratibu wa kuwakimu wawili hao mpaka hapo watakapoweza kujitegemea wenyewe. Na kufanya hivi, ni sadaqa iliyo bora kwani Mtume ametufundisha kuwa katika kutoa sadaqa kwanza tuwakumbuke ndugu zetu wa karibu (hasa familia) kuwapa sadaqa hiyo.

Kuhusu uuzaji na unywaji pombe hadharani:-

Kwetu sisi Waislamu kuuza na au kunywa pombe ni haramu. Hivyo yeyote anayejihusisha na biashara hiyo, hana budi kukoma kabisa mara moja. Lakini kwa vile jamii yetu ya kitanzania ni mchanganyiko wa dini mbali mbali ambazo baadhi yake zinaruhusu unywaji pombe, hatuwezi kulizuia jambo hili kwa kila mtu. Hata hivyo tuipigie kelele serikali ipige marufuku unywaji pombe katika maduka yaliyo mtaani (groceries).

Kadhalika tuzidishe kuzungumza na watoto wetu, tuwakumbushe madhara ya pombe na uzinifu na pia adhabu kali za Mwenyezi Mungu alizowaandalia watu wenye tabia hizo. Pia jamaa zetu walio walevi, tuwakemee na tusiwakaribishe majumbani mwetu wakiwa wamelewa.

Hii itampa mtoto picha kuwa pombe ni kitu kisichofaa kabisa.

Juu

Maelewano kati ya Mume na mke.

Mume na mke kila mmoja aonyeshe kumjali mwenzi wake. Katika maisha ya ndoa mtu ajitahidi kuacha ubinafsi, yaani asijikumbuke (asijitangulize nafsi yake) yeye tu zaidi ya mwenzi wake; apunguze "mimi" na aongeze kwa wingi "sisi". Kila mmoja "amuenzi" mwenzi wake kiasi cha kumfanya huyo mwenziwe ajione kama ni yeye tu kwa huyo mwenzi wake. Hebu tujikumbushe hadithi ya Mtume (S. A. W) alipowaambia maswahaba:

"Mbora miongoni mwenu ni yule aliye mwema kwa mkewe na mimi ni mbora kuliko ninyi nyote [kwa vile mimi ni mwema sana kwa wake zangu]"

Mtume (S. A. W) alionyesha mapenzi ya hali ya juu kwa kwa wake zake: alicheza nao na alifanya kazi za nyumbani. Mke wa kwanza wa Mtume (S. A. W) Bi. Khadija (r.a) aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri alitoa mali yake nyingi kwa ajili ya Mtume (S. A. W) na baada ya mumewe kupata utume Bi. Khadija aliendelea kutoa mali yake kuuendeleza Uislam.

Kwa kweli maisha ya ndoa hayataki ushindani kati ya mume na mke hata kidogo, bali iwe ni ya kuhurumiana. Ni kwa sababu hii M/Mungu anatufahamisha katika Qur'an kuwa:

"Na katika alama zake (za kuonyesha Ihsani yake juu yenu) ni kuwa amekuumbieni wake zenu kwa jinsi yenu ili mpate utulivu (wa maisha) kwao, naye amejaalia mapenzi na (kuoneana) huruma baina yenu, bila shaka katika haya zimo alama kwa watu wanaofikiri". (30:21).

Ukaribu wa baba na binti yake.

Ni vema kuwepo uhuru mkubwa kabisa wa kuonana na kuzungumza kati ya baba na binti zake; wale chakula pamoja na watoke (watembee) pamoja.

Kadhalika akina kaka nao wawe karibu na dada zao, wajumuike na kuzungumza, wasaidiane kazi za shuleni na nyumbani, pia na matembezi ya pamoja. Katika hili wazazi wanalo jukumu la kuwahimiza watoto wao (wa kike na wa kiume) kushirikiana.

Utazamaji wa TV na Video.

Kwa familia zenye TV majumbani, wazazi/walezi wahakikishe kuwa TV inawashwa kwa vipindi vyenye kufaa kimaadili tu. Hata vile vipindi vya kuchekeshachekesha yaani "Comedy" ni hatari. Wazazi wawe wanaufahamu utaratibu (ratiba) wa vipindi kwa kila kituo cha TV ili kuweza kudhibiti utazamaji. Aidha kanda za Video zinazokuja nyumbani ziwe tayari zimehakikishwa na wazazi kuwa hazina mambo ya "kipuuzi".

Tukazanie stara ya mwanamke na tukomeshe michanganyiko ya wanawake na wanaume.

Mwanamke wa Kiislamu anapotoka kwenda shuleni, sokoni, kazini na pengine popote sharti ajihifadhi kisheria-ajifunike mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mkono. Hata mwanamke huyo anapokuwa nyumbani lakini akalazimika kuonekana mbele ya wanaume wasio maharimu kwake.

Mfano: nyumbani kuna wageni wa kiume nae anakwenda kuwasabahi au kuwaandalia chakula au hapo anapokaa anaishi na shemeji zake au rafiki wa kaka zake au mwanamume mwingine yeyote wa mbali (aliye ajnabi kwake) basi mwanamke huyo analazimika kujihifadhi muda wote.

Juu

Walio na jukumu kuhakikisha kuwa amri hii inatekelezwa ni ama baba, mume, kaka au mtoto wa kiume wa mwanamke huyo. Wajibu huu wa mwanamume juu ya mwanamke unapatikana katika Qur'an pale Mwenyezi Mungu aliposema:

"Wanaume (wawe) walinzi wa wanawake kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine… (Qur'an 4:34)

Pia katika hadithi moja Mtume (S. A. W) alisema kuwa mwanamke mmoja ataweza kuwazuia wanaume wanne wasiingie peponi kwa vile hawakufanya juhudi yoyote ya kumdhibiti yeye (huyo mwanamke) alipokuwa chini ya uangalizi wa kila mmoja wao. Mtume ( S. W. A) aliwataja wanaume hao kuwa ni baba, mume, kaka na hatimaye mtoto wa kiume wa mwanamke huyo.

Kuhusu michanganyiko ya wanawake na wanaume; tunapokusanyika kufanya sherehe basi tujitahidi kuepuka michanganyiko hiyo. Ikiwa ni harusi, mahafali au shughuli nyingine (ya halali) basi wanaume wakusanyike katika sehemu tofauti na ile ya wanawake.

Ikiwa imelazimu kwamba wanawake na wanaume wakutane sehemu moja (Uwanja au ukumbi mmoja) basi wanaume wakae safu za mbele na wanawake wafuate nyuma lakini wasichanganyike. Ikiwa kuna yeyote anayeona kwamba sherehe haitafana pasi na wanawake na wanaume kuchanganyika pamoja bila shaka mtu huyo ana "damu ya uzinifu".

Ee dada wa kiislamu, jitahidi kujiweka katika hali ya kuvutia (ili kumvutia mumeo na ni mumeo tu). Pia mazingira ya nyumbani nayo yawekwe katika hali ya unadhifu na katika mtindo unaoujua kuwa unampendeza mumeo. Haya yote, Insha'Allah, yatamfanya mumeo muda wote awe na hamu ya kurudi nyumbani na kukaa nawe. Bahati mbaya leo mambo ni tofauti: mume anaporudi nyumbani anakuta mkewe "kachakarika" kisa eti kazi za nyumbani huwa zinamtinga. Lakini mwanadada huyohuyo akit ok a kwenda shughulini , sokoni na k adhalika muone jinsi "anavyomeremeta" kwa mavazi na manukato. Aidha utaku ta ndani ya nyumba vitu vimekaa "shaghalabaghala" eti mpaka asikie kuwa leo kuna wageni ndio nyumba ipambwe! Je haya yote yanapokosekana haitoshi kumfanya mume aone kuwa "huko nje" ni bora kuliko ndani kwake?!. Hata hivyo ikiwa mke anaonyesha uzembe huo, haimaanishi kuwa sasa huyo mume anayo ruhusa ya kuwa baradhuli. Mwenyezi Mungu atuepushe na yote hayo.

Juu
NENO LA MWISHO

Ndugu Waislamu tutambue kuwa kila jambo (kitu) alichojaaliwa mtu kuwa nacho ni mtihani kwake. Mali , watoto, madaraka, vipaji, maradhi, afya n.k yote haya ni mtihani kwa yule aliyejaaliwa nayo. MATAMANIO YA JIMAI NI MTIHANI KWA MTU. Mtu anapopatwa na matamanio hayo, Allah (S.W) anangalia ni vipi mtu huyu ataikidhi haja yake. Na utaratibu wa Mwenyezi Mungu kwa mtu aliyepatwa na matamanio hayo ni huu:

kwa aliyeoa au kuolewa basi AMGEUKIE MKEWE AU MUMEWE.

Kwa ambaye hajaoa/kuolewa huyo AJIZUILIE mpaka hapo Allah (S.W) atakapomjaalia kupata mke au mume.

Waislamu tukumbuke na kuzingatia kwa ukamilifu amri ya Allah (S.W):Reply

"Wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu (mkubwa) na ni njia iliyo mbaya kabisa" (Qur'an 17:32).

Baada ya kuutambua ujumbe katika aya hii basi tudumu katika kuomba kama tulivyofundishwa na Allah (S.W):

"(Hao wenye akili husema) 'Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza, na utupe rehema itokayo kwako; hakika wewe ndiye Mpaji mkuu' " (Qur'an 3:8).
Source: Na Ukhti Zuleikha Ally Rashid
 
Mwambie binti yako basi azae akiwa na 12 years ehh...Utamkuza binti vipi ukihalalisha uzinzi at a very young age??hivi maadili yenu yako wapi na hata makanisani ama miskitini mnajifunza kweli mnayoambiwa???

Kwani hao wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni huwa wanaambiwa wakazae wakiwa na miaka 12? How people can be so ignorant is beyond me. Kwani unafikiri makanisa na misikiti imeanza leo? And who do you think is interested in your religious commitments? Na wengine wanaowapa watoto wa shule mimba ni wachungaji na mashehe. Au hujasikia makasisi wakilawiti vijana wadogo? Hayo maadili?

The problem of teen pregnancy will always be there. Usifikiri utapunguza tatizo kwa kusema eti msichana akipata mimba anafukuzwa shule (Akili hizi za kung'ang'ana na majawabu bila kulielewa tatizo ni cancer katika jamii yetu). Kama huna ufahamu wa kujadili jambo, huna haja ya kulijadili.

Wewe una maadili gani if all you can do is to suggest denying access to education to victims of teen pregnancy? Yaani maadalili ni kuwanyima wasichana fursa za kupata elimu? I am sorry but you don't know anything mom. Badala ya kuhangaika kuwanyima wasichana fursa za kusoma, kwanini usihangaike na kutoa adhabu kwa viongozi uchwara na wezi wanaoliangamiza taifa?
 
Madhara ya Zinaa na jinsi ya kujiepusha nayo:

UTANGULIZI

"Amrishaneni mema na katazaneni mabaya kwani hii ni dawa yenu; lakini pindi mtakapoacha kuamrishana mema na kukatazana mabaya itakujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni na wakati huo mtaomba nusra na hamtakubaliwa".

...

Mkuu public finance na hili somo vipi tena? Jitahidi kuwa serious basi.

Ishu za mimba nimekuonyesha tamko lilivyopingana na ilani na matamko mengine.
Ishu ya kodi nakuuliza kitu kingine unaniletea ishu nyingine.
 
Kaka pole sana naona mapovu matupu badala ya hoja za msingi. Wameambiwa wakipata mimba waende VETA wajifunze kushona, waende shule za private.

Nyinyi ndio wanafiki wenyewe, watu wanafukuzwa shule kwa utoro, kwa kupiga waalimu, na kwa makosa mengi tu mbona hao hawatetewi?, ina maana hawana faida kwa taifa lao?.

Hatuwezi kukubaliana na mawazo ya kuzigeuza korido za shule zikawa sawa na zile za zahanati, lazima tulinde maadili ya kitanzania. Wewe unaweza usiwe na uwezo wa kuelewa maana ya maadili lakini wapo wengi wanaonielewa.

Your thinking is flawed.

1/ Kwa kuwa sikutetea wanafunzi watoro wasifukuzwe shule hakuninyimi haki ya kutetea wahanga wa mimba za utotoni kupata fursa za elimu. Philosophically speaking, you do not justify a wrong by citing another wrong. That said, mambo ya mwanafunzi kumpiga mwalimu na msichana kupata mimba akiwa shuleni hayafanani. It shows that unajaribu kujadili tatizo ambalo hata hulielewi. Unasukumwa na mihemko. Kama una hoja ya kutetea mwanafunzi anayempiga mwalimu iweke mezani, badala ya kulazimisha wanaopinga kauli ya Rais inayokandamiza wasichana wa nchi hii wawatete wanafunzi waliompiga mwalimu.

2/ You are claiming causality simply based on gut feeling. Hoja kwamba kuruhusu wasichana wanaopata mimba kuendelea na masomo ni "kuzigeuza korido za shule sawa na zile za zahanati" is empty, hollow, and populistic. You are simply reproducing your religious biases in the name of maadili.

3/ Ni maadili gani ya nchi hii unayozungumza? Kuiba mali za umma? Ubabaishaji?
 
Wa kike akikubali kumtaja wa kiume ni jela miaka 30 hiyo ipo wazi siku zote sasa kama ni mwanafunzi atasoma saa ngapi wakati yuko magereza, na huko private ni wazazi huwapeleka kwa siri hawezi kusema alishazaa
 
Kubakwa ni swala lingine jamani na akiwa muwazi kuwa kabakwa akipelekwa hosp atapewa dawa za kuzuia lile yai lisiweze kukomaa na kutunga mimba ili mradi iwe ndani ya masaa 48
 
Sikutegemea nchi hii kuna ambae angepingana na hili la waliozaa primary wasiendelee shule wazazi tuna akili za kutofautiana mimi namuunga magu mkono mia mia kwa sababu tutahamisha hawa watoto wadogo waone ni jambo la kawaida watazaa sana mtalea ujukuu na kuwa na watoto wenye virus vya ukimwi wengi matendo ya watoto wetu wa sasa ni machafu mno jamani
 
Lakini huo mtazamo wa Magu ni mtazamo wa watu wengi pia.

Wewe subiri tu uone maoni ya watu humu....utashangaa!!
IMG-20170624-WA0011.jpg
 
Ndio alichosema magu akibeba mimba akiwa shule ya msingi au sec akishajifungua anaweza kwenda veta au sehemu nyingine kujiendeleza na si kurudi kule msingi au sec namuunga mkono mia kwa mia tusitafute sababu kufanya watoto wetu wakaona ni kitu cha kawaida kubeba mimba akiwa na umri mdogo watakufa wengi na uzazi pia ukimwi upo tusisahau hilo tukakimbilia kuklalamikia mimba tu, pia hawa watoto wamezidi jamani wanafanyana hadi darasani wanakaliana anasogeza kichupi kijana anaingia na anamkatikia huku wenzao wapo humo humo darasani hapana jamani tusiteteee mambo ya ajabu haya
salome peter , uko sahihi...hata mimi nimeona huyo binti anayekenua chupi kumkatikia mvulana shuleni. Hiyo ni picha ya mjini, je unafahamu wa kijijini wanapataje mimba?

Nakuhakikishia, yule uliyemuona anakatika darasani kamwe hutasikia anakatisha masomo sababu ya mimba. Pale alipo anafahamu a to z ya mimba, anajua hata pa kwenda kuitoa. Anaenjoy yule, na nafikiri unamuona alivyofurahi. Lakini Salome, kuna wengine huko kijijini, ambao hadi mbegu zinawaingia hawajui raha yeyote ya ngono.

Wakati huyu uliyemuona wewe kwenye whatsapp anakenua chupi yake, kijijini yupo ambaye hana hata hiyo chupi. Huyu hulazwa chini kichakani akaingiliwa akiwa analia, akishamwagiwa hizo mbegu anapewa 1000 na kuambiwa asiseme. Kwa kukosa kwake kujiamini, anaogopa kusema. Kinachokuja kuyaibua haya ni tumbo kubwa...huyu naye ahukumiwe sawa na huyu anayehongwa chips?

Kapewa mimba njiani akizikata kilometa 6 kati ya kijiji na shule, atamudu kuifikia VETA iliyo makao makuu ya mkoa? Huko VETA anasoma kwa gharama za nani?
 
Mmmm hii njia nina mashaka nayo kama kweli inafaa kukomesha tatizo hili. Tusije tukaanza kukomoa tukadhani tunakomesha. Haya ni mambo mawili tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom