Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kwa sasa kinachoendelea ni utambulisho wa viongozi ikiwemo wizara na idara za serikali. Waliokuwepo kwa uchache ni Dkt. Damass Ndumbaro, Medadi Kalemani ambae ni mbunge mwenyeji na waziri wa nishati, Dotto Biteko ambae ni waziri wa madini, Elias Kwandikwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Waziri wa maji, Jumaa Aweso na Marry Masanja Naibu waziri wa Utalii. Pia yupo Mwita Waitara naibu wa Mazingira.

Pia upo uongozi wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii, wapo wakurugenzi, wakuu wa taasisi ikiwemo Tawa, Tafori na DTI. Upo pia ungozi wa mkoa wa Geita ukiongozwa na mkuu wa mkoa, makatibu tawala na manaibu wao, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, kamati ya usalama wilaya ya Chato, viongozi wa chama cha Mapinduzi Geita, viongozi wa dini mkoa na wilaya pia wabunge wa mkoa wa Geita.

=========

Medard Kalemani: Mheshimiwa Rais wetu, sisi wananzengo na wananchi wa Chato kwa siku ya Leo ni siku ya furaha kubwa na kwetu sisi ni siku ya kihistoria, nichukue nafasi hii kwa niaba ya wananzengo na wananchi wa Jimbo letu na wilaya yetu ya Chato, kwanza kabisa kuwakaribisheni Chato.

Chato ndugu zangu ni nchi yetu sote, naomba wananchi wa Chato tuwapigie makofi wageni wote waliofika hapa.

Nimesikia huu ni msitu wa pili kwa ukubwa nchini kwetu, hongereni sana. Pia msitu ni wa kwanza kwa aina ya misitu mchanganyiko, misitu ya kupanda na misitu asili. Eneo hili limetoa ajira na watumishi na wafanyakazi ni wanaozunguka maeneo haya.

Mheshimiwa Rais na ndugu wananchi, kwa heshma ya pekee napenda nitoe shukrani ya moyoni, hawa wananchi walioko hapa kama kawaida ya misitu mmetupatia chakula, nawaomba wananchi tushangilie sana. Kitendo cha kutupatia ng'ombe wanne wakubwa madume yaliyonona kwa ajili ya wananchi hawa kula walau leo mchana na kilo 1,500 kwa ajili ya chakula cha mchana tunawashukuruni sana, wananchi tupige makofi na vigerere kwa ushirikiano huu mzuri. Mheshimiwa Rais na Waziri baada ya kusema hayo, niwashukuruni sana kwa kunisikiliza.

10:20 Asubuhi: Rais John Magufuli amewasili eneo la tukio na kupokewa na viongozi kadhaa kisha kuimbwa wimbo wa Taifa na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Baada yahapo zimefata Dua na Sala kutoka kwa viongozi wa dini.

RAIS MAGUFULI: Nimeanzisha mashamba mengine manne ya misitu. Nina historia na eneo hili, wakati nikiwa mbunge ukifanya mkutano tu kwenye maeneo kutoka hapa Buseresere mpaka Bwanga.

Sikutegemea kama siku moja tutakuta miti mizuri shamba hili, mmefanya kazi kubwa sana, hongereni sana. Mimi nafikiri kwa kazi kubwa iliyofanywa na wizara ya maliasili na utalii lakini kwa kazi kubwa iliyofanywa na kamishna anaehusika na hifadhi ya misitu lakini kwa kumbukumbu kubwa ya vijana hawa maaskari wameendelea kulinda rasilimali hii

Katika kipindi hiki ambako kuna magonjwa gonjwa yanayojitokeza yasiyojulikana kama Korona, nchi nyingi wananchi wake watakuwa wamejifungia ndani, sisi Watanzania hatujajifungia ndani na hatutegemei kujifungia ndani na wala sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yuko hai na ataendelea kutulinda Watanzania lakini pia tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya ikiwa ni pamoja na kujifukizia. Unajifukizia huku unamuomba Mungu, unaswali huku unapiga zoezi la kufanya kazi la kulima mahindi, viazi ili ule vizuri ushibe Corona ishindwe kuingia kwenye mwili wako.

Mtatishwa sana ndugu zangu Watanzania lakini simameni imara, ninajua wapo baadhi ya Watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na walipochanjwa huko, wamekuja huku wametuletea Corona ambayo ni ya ajabu ajabu, simameni imara.

Chanjo hazifai, kama wazungu wangekuwa na uwezo wa kuleta chanjo, hata chanjo ya Ukimwi ingekuwa imeshaletwa, hata chanjo ya kifua kikuu, kifua kingekuwa kimeshaondoka, hata chanjo ya maleria ingekuwa imeshapatikana, hata chanjo ya kansa ingekuwa imeshapatikana.

Ni lazma Watanzania tuwe waangalifu kwa mambo ya kuletewa letewa, msije mkafikiria mnapendwa sana. Taifa hili ni tajiri, Afrika ni tajiri, kila mmoja anaitamani, tuwe waangalifu na niiombe wizara ya afya isiwe inakimbilia mambo ya machanjo chanjo bila yenyewe kujiridhisha.

Ipo nchi fulani watoto wake walichanjwa wa kike umri wa miaka 14, wanaambiwa ni kwa ajili ya kuzuia kansa ya kizazi, imekuja kugundulika ile chanjo ni kwa ajili ya kuwazuia wasizae, kwa hiyo niiombe sana Wizara ya Afya, sio kila chanjo ni ya maana kwa Taifa letu.

Sio kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima Watanzania tuwe macho, ni lazima watanzania tuwe waangalifu, tutafanyiziwa majaribio ya ajabu ambayo yataleta madhara makubwa, ninaomba tuendelee kusimama na kumuomba Mungu wetu, tuendelee kumtanguliza Mungu wetu huku tukichukua tahadhari za kiafya kadri tutakavyokuwa tunaambiwa na wataalam wetu lakini tujihadhari sana.

Tumeweza kukaa zaidi ya mwaka mzima na kitu, Tanzania tukiwa hatuna Corona hata hapa hakuna alievaa barakoa, Mungu wetu yuko mbele ya shetani.

Kwa hiyo niwaombe ndugu zangu Watanzania na hasa Wizara wa Afya ambae ni kiongozi wetu ijitahidi sana kuangalia afya za Watanzania bila kuingia kwenye papara za kuletewa kila jaribio linalofanyika linaletwa hapa, hii ni tahadhari na mimi naamini tutafanikiwa.
 
Hongera TSF, huu ni mradi wa mkakati, mapori mengi yamebaki vichaka, mnaweza tafiti miti hardwood za kisasa za muda mfupi rafiki mazingira, pia tujipange kubadili sekondari za kata ziwe veta, twaweza kuwa exporter wa thamani duniani.
 
Back
Top Bottom