Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Hamasa ya upandaji wa miti huko Chato na Dodoma ihimizwe kufanyika nchi nzima hasa Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Singida, Pwani, Lindi, Mtwara, Kigoma, Morogoro, Rukwa, Katavi, Mara, Manyara, Arusha, Tanga, Ruvuma, Tabora, Njombe, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Dar Es Salaam.
Msitu wa kupandwa wa Mafinga Iringa, Morogoro, Tanga na Arusha zilianzishwa na Mwalimu Nyerere. Enzi za Mwalimu Nyerere mwaka 1977-1979 wananchi vijijini walikuwa wanaenda kupanda na kupalilia miti ya serikali na kupata ujira wa unga wa njano au ngano aina ya buruka. Miti lishamiri sana na hali ya hewa ilitamalaki mvua za kutosha lakini baada ya soko huru kufunguliwa na sera za serikali kutokuwa na mwelekeo unaotabirika wajanja wachache kutoka serikalini walihujumu rasilimali hizo kwa kukata miti kwa ajili ya mbao, kuni na mkaa; mfani kule Kibaha kulikuwa na mapori ya miti ya mikorosho kuanzia Kongowe ingia ndani kupita Chuo kikuu cha Open yalitelekezwa na watu binafsi wakahodhi kisha kuanza kuuzia mtu mmoja mmoja.
Miti ya vivuli, matunda na mbao inatija kama hamasa itazingatiwa kwa nchi nzima ambapo itasaidia sana kurekebisha uchafuzi wa mazingira, kulinda vyanzo vya maji, kulinda viumbe hai adimu kama vipepeo, vyura (Kihansi Morogoro, Ruhuji Njombe, Ziwa Ngozi kule Rungwe Tukuyu, Amboni Tanga, Mlima Mbeya, Milima Livingstone and Kipengele kule Njombe na Ruvuma, Kondoa Irangi, Uvinza Kigoma kwenye mto Malagarasi, Ilolangulu na Sikonge Tabora, Bonde la mto Simiyu kule Magu na Gamboshi, Ziwa Kindai an Singida kule mjini Singida nk