Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Hamasa ya upandaji wa miti huko Chato na Dodoma ihimizwe kufanyika nchi nzima hasa Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Singida, Pwani, Lindi, Mtwara, Kigoma, Morogoro, Rukwa, Katavi, Mara, Manyara, Arusha, Tanga, Ruvuma, Tabora, Njombe, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Dar Es Salaam.

Msitu wa kupandwa wa Mafinga Iringa, Morogoro, Tanga na Arusha zilianzishwa na Mwalimu Nyerere. Enzi za Mwalimu Nyerere mwaka 1977-1979 wananchi vijijini walikuwa wanaenda kupanda na kupalilia miti ya serikali na kupata ujira wa unga wa njano au ngano aina ya buruka. Miti lishamiri sana na hali ya hewa ilitamalaki mvua za kutosha lakini baada ya soko huru kufunguliwa na sera za serikali kutokuwa na mwelekeo unaotabirika wajanja wachache kutoka serikalini walihujumu rasilimali hizo kwa kukata miti kwa ajili ya mbao, kuni na mkaa; mfani kule Kibaha kulikuwa na mapori ya miti ya mikorosho kuanzia Kongowe ingia ndani kupita Chuo kikuu cha Open yalitelekezwa na watu binafsi wakahodhi kisha kuanza kuuzia mtu mmoja mmoja.

Miti ya vivuli, matunda na mbao inatija kama hamasa itazingatiwa kwa nchi nzima ambapo itasaidia sana kurekebisha uchafuzi wa mazingira, kulinda vyanzo vya maji, kulinda viumbe hai adimu kama vipepeo, vyura (Kihansi Morogoro, Ruhuji Njombe, Ziwa Ngozi kule Rungwe Tukuyu, Amboni Tanga, Mlima Mbeya, Milima Livingstone and Kipengele kule Njombe na Ruvuma, Kondoa Irangi, Uvinza Kigoma kwenye mto Malagarasi, Ilolangulu na Sikonge Tabora, Bonde la mto Simiyu kule Magu na Gamboshi, Ziwa Kindai an Singida kule mjini Singida nk
 
Mwambieni mkuu huku kwetu TANGA - Lushoto, kuna mashamba ya miti makubwa zaidi ya hayo, waje wazindue kama vya kuzindua vimeisha .........
 
Magu ni denialist, kama hataki chanjo sisi tunaitaka. Sisi wengine hatutaki kufa.

Magu anakiri kua corona ipo kuna watu wameileta ila hataki hata kuhamasisha watu wachukue tahadhari, anapongeza watu wasiovaa barakoa.

Yeye anaamini corona imeletwa na wazungu ili waje kuichukua Afrika.

Kama chanjo mbaya tukatae chanjo zote, sio ya corona tu, tukatae za malaria, kifua kikuu, typhod, kichocho, kansa. Ikiwezekana tufute wizara ya afya na serikali isinunue madawa, tupambane na tiba za asili na maombi ili tuepuke wazungu wasije kuchukua nchi yetu.

Akili za viongozi wetu
 
sisi watanzania hatujajifungia ndani na hatutegemei kujifungia ndani na wala sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yuko hai
Yaani ktk hili niko na wewe JPM 100%. Japo sikupendi na wala sikukuchagua na hata sikubali ushindi wako ktk uchaguzi mkuu wa 2020.
 
Tatizo lake anajiona ni infinit
 
Nadhani wazungu wakitaka kuichukua Afrika hawashindwi, hata kwa mabomu ya maangamizi ya watu ..... weapons of mass destruction
 
Waoga saaana wa Corona inawasepesha!!

Inaonesha jinsi ulivyomuoga, Rais alivyosisitiza koote huko kuhusu kuchukua hatua na tahadhari juu Corona, wewe umeskia Neno la yeye kukataa kinga pekee??

Chukua tahadhari mpuuzi wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…