Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Rais Magufuli: Sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani (Covid19), tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya. Akemea Chanjo

Shamba la miti oyeeee! Uchumi wa kati oyeee!! Dhuluma kwa wafanyakazi oyeee! Wizi wa kura oyeee!! Uminywaji wa demokrasia na uhuru wa habari huko nchini Puerto Rico, oyeee!!
Mfanyakazi yupi kadhulumiwa?? Ufipani kama vile mumevurugwaaa
 
Ila wakati huo mnapokea ARV za Wazungu? Hvi tuseme hao mabeberu waache kutupa dawa kwa cut-price ama bure tunaweza jilinda wenyewe? Ama Corona tu ndio tunajiona tupo invicible kisa kuwakejeli humu?

Btw kila chanjo au dawa ina side effects na margin of error lazima iwepo kwenye kila kitu hata tu dawa ya meno watumiaji wote lazima 0.5% wapate complications za meno mpaka kansa kabisa!! Ila je inahalalisha kuwa tusitumie dawa ya meno?

Hakuna chanjo isiyo na side effect hata dawa zote ukisoma makasha yake inakueleza madhara ya dawa husika..... Unless ww au Rais atuambie ni treatment ipi ya cancer ambayo haina side effect kuanzia chemotherapy mpka hizo radiology.... Ipi haina madhara kwenye mwili?
Kwani ma ARV nani kakwambia nimazuriii. Waulize watumiajiii.
 
Wakati mwingine ni vizuri kujifunza kuweka akiba ya maneno, msitake take sana kupotosha kauli za Dk.Magufuli mkisukumwa na itikadi zenu za vyama, yaani mnachukulia kila kitu kisiasa siasa tu.

Unambeza beza Dk.Magufuli kwa kuwa wewe si mwana sayansi, unachukulia kauli JPM anayo waonya Wizara ya afya pamoja na Watanzani, wewe onyo hilo unalichukulia kimzaa mzaa tu, lakini wana sayansi wenzake mbona tumemuelewa vizuri tu, sasa wewe puuzia ushauri wak, puuza kijifukizia na tahadhali nyingine kama za mwaka jana.Ukiona vipi,nenda Kenya au Afrika Kusini kadungwe chanjo za Oxford na washirika wake, halafu tuletee mlejesho baada ya wiki moja kupita.

Chunga sana,si kila king'aacho ni dhahabu/Almasi.
Kuna chanjo isiyo na side effect ewe mwanasayansi?

Rais anadai chanjo ya cervical cancer ilisababisha watu wasizae. Ssa nikuhoji wwe mwanasayansi ni tiba gani ya saratani isiyo na side effects kwa mwili? Je exception ya 0.2% inahalalisha kuwa chanjo fulani haifai?

Kma mnaona wazungu ni wauaji kataeni ARV zao za bure, kataeni misaada ya mashine za MRI au CT Scan or wateva mnayodhani wanataka kutumalizia alafu mje na mbadala tuone.

Sio unakejeli dawa ya ugonjwa A hku unakubali dawa ya ugonjwa B while supplier ni mmoja!!
 
Ni wapi wazungu wametangaza kuwa chanjo zitajaribiwa africa au kwetu?? kinyume kabisa chanjo wameanza kuchoma wao wakimaliza ndio tutakumbukwa huku. Ni wakati wa kuongea na facts sio opinion. Je watoto wadogo hawachomwi chanjo ya kifua kikuu? zamani ilikuwa hakuna siku hizi wanachomwa. Hao aliosema chanjo ya kizazi ni wapi lazima aweka facts tukianza kupeleka nchi kwa opinion sio facts basi na kuhakikishia huko mbele sio kuzuri tutakuwa blacklisted nchi zote. Kuna watu watakuja kusema hatuna shida ya kwenda huko bila kusahahu mahitaji yetu mengi ni huko. angalizi mwisho wetu sio mzuri na uhakika na hilo.
 
Kwa sasa kinachoendelea ni utambulisho wa viongozi ikiwemo wizara na idara za serikali. Waliokuwepo kwa uchache ni Dkt. Damass Ndumbaro, Medadi Kalemani ambae ni mbunge mwenyeji na waziri wa nishati, Dotto Biteko ambae ni waziri wa madini, Elias Kwandikwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Waziri wa maji, Jumaa Aweso na Marry Masanja Naibu waziri wa Utalii. Pia yupo Mwita Waitara naibu wa Mazingira.

Pia upo uongozi wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii, wapo wakurugenzi, wakuu wa taasisi ikiwemo Tawa, Tafori na DTI. Upo pia ungozi wa mkoa wa Geita ukiongozwa na mkuu wa mkoa, makatibu tawala na manaibu wao, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, kamati ya usalama wilaya ya Chato, viongozi wa chama cha Mapinduzi Geita, viongozi wa dini mkoa na wilaya pia wabunge wa mkoa wa Geita.

=========

Medard Kalemani: Mheshimiwa Rais wetu, sisi wananzengo na wananchi wa Chato kwa siku ya Leo ni siku ya furaha kubwa na kwetu sisi ni siku ya kihistoria, nichukue nafasi hii kwa niaba ya wananzengo na wananchi wa Jimbo letu na wilaya yetu ya Chato, kwanza kabisa kuwakaribisheni Chato.

Chato ndugu zangu ni nchi yetu sote, naomba wananchi wa Chato tuwapigie makofi wageni wote waliofika hapa.

Nimesikia huu ni msitu wa pili kwa ukubwa nchini kwetu, hongereni sana. Pia msitu ni wa kwanza kwa aina ya misitu mchanganyiko, misitu ya kupanda na misitu asili. Eneo hili limetoa ajira na watumishi na wafanyakazi ni wanaozunguka maeneo haya.

Mheshimiwa Rais na ndugu wananchi, kwa heshma ya pekee napenda nitoe shukrani ya moyoni, hawa wananchi walioko hapa kama kawaida ya misitu mmetupatia chakula, nawaomba wananchi tushangilie sana. Kitendo cha kutupatia ng'ombe wanne wakubwa madume yaliyonona kwa ajili ya wananchi hawa kula walau leo mchana na kilo 1,500 kwa ajili ya chakula cha mchana tunawashukuruni sana, wananchi tupige makofi na vigerere kwa ushirikiano huu mzuri. Mheshimiwa Rais na Waziri baada ya kusema hayo, niwashukuruni sana kwa kunisikiliza.

10:20 Asubuhi: Rais John Magufuli amewasili eneo la tukio na kupokewa na viongozi kadhaa kisha kuimbwa wimbo wa Taifa na wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Baada yahapo zimefata Dua na Sala kutoka kwa viongozi wa dini.

RAIS MAGUFULI: Nimeanzisha mashamba mengine manne ya misitu. Nina historia na eneo hili, wakati nikiwa mbunge ukifanya mkutano tu kwenye maeneo kutoka hapa Buseresere mpaka Bwanga.

Sikutegemea kama siku moja tutakuta miti mizuri shamba hili, mmefanya kazi kubwa sana, hongereni sana. Mimi nafikiri kwa kazi kubwa iliyofanywa na wizara ya maliasili na utalii lakini kwa kazi kubwa iliyofanywa na kamishna anaehusika na hifadhi ya misitu lakini kwa kumbukumbu kubwa ya vijana hawa maaskari wameendelea kulinda rasilimali hii

Katika kipindi hiki ambako kuna magonjwa gonjwa yanayojitokeza yasiyojulikana kama Korona, nchi nyingi wananchi wake watakuwa wamejifungia ndani, sisi watanzania hatujajifungia ndani na hatutegemei kujifungia ndani na wala sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yuko hai na ataendelea kutulinda watanzania lakini pia tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya ikiwa ni pamoja na kujifukizia. Unajifukizia huku unamuomba Mungu, unaswali huku unapiga zoezi la kufanya kazi la kulima mahindi, viazi ili ule vizuri ushibe Corona ishindwe kuingia kwenye mwili wako.

Mtatishwa sana ndugu zangu watanzania lakini simameni imara, ninajua wapo baadhi ya watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na walipochanjwa huko, wamekuja huku wametuletea Corona ambayo ni ya ajabu ajabu, simameni imara.

Chanjo hazifai, kama wazungu wangekuwa na uwezo wa kuleta chanjo, hata chanjo ya Ukimwi ingekuwa imeshaletwa, hata chanjo ya kifua kikuu, kifua kingekuwa kimeshaondoka, hata chanjo ya maleria ingekuwa imeshapatikana, hata chanjo ya kansa ingekuwa imeshapatikana.

Ni lazma watanzania tuwe waangalifu kwa mambo ya kuletewa letewa, msije mkafikiria mnapendwa sana. Taifa hili ni tajiri, Afrika ni tajiri, kila mmoja anaitamani, tuwe waangalifu na niiombe wizara ya afya isiwe inakimbilia mambo ya machanjo chanjo bila yenyewe kujiridhisha.

Ipo nchi fulani watoto wake walichanjwa wa kike umri wa miaka 14, wanaambiwa ni kwa ajili ya kuzuia kansa ya kizazi, imekuja kugundulika ile chanjo ni kwa ajili ya kuwazuia wasizae, kwa hiyo niiombe sana wizara ya afya, sio kila chanjo ni ya maana kwa Taifa letu.

Sio kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima watanzania tuwe macho, ni lazima watanzania tuwe waangalifu, tutafanyiziwa majaribio ya ajabu ambayo yataleta madhara makubwa, ninaomba tuendelee kusimama na kumuomba Mungu wetu, tuendelee kumtanguliza Mungu wetu huku tukichukua tahadhari za kiafya kadri tutakavyokuwa tunaambiwa na wataalam wetu lakini tujihadhari sana.

Tumeweza kukaa zaidi ya mwaka mzima na kitu, Tanzania tukiwa hatuna Corona hata hapa hakuna alievaa barakoa, Mungu wetu yuko mbele ya shetani.

Kwa hiyo niwaombe ndugu zangu watanzania na hasa wizara wa afya ambae ni kiongozi wetu ijitahidi sana kuangalia afya za watanzania bila kuingia kwenye papara za kuletewa kila jaribio linalofanyika linaletwa hapa, hii ni tahadhari na mimi naamini tutafanikiwa.
Kwa hiyo huyo "mungu" anatusikia zaidi Watanzania kuliko hata Waisraeli tunakokwendaga kuhiji?

Za kuambiwa....................................... 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️ 🏃‍♂️
 
Ukitawaliwa na chukia hisia za chuki hazikutoki
 

Attachments

  • IMG-20210127-WA0002.jpg
    IMG-20210127-WA0002.jpg
    79.6 KB · Views: 1
Anajibu vitu mabavyo hata hajaulizwa!

Anazungumzia Chanjo ambapo Africa inakuja mwaka 2030,kuzungumzia chanjo sasa ni ukichaa maana hata Ulaya inagombewa bado watu hawajapata

Kenya wajanja kuna namna wamepata kiasi fulani,kwa massive vaccination ni baada ya Ulaya kuchanjwa wote na sio Africa

Hilo swali la chanjo ni ukichaa kulizungumzia maana kwanza hajaulizwa

Kuhusu lockdown,hajaulizwa

Watu wakiumwa naturally wataanza kujificha na huwezi wapangia....

Mambo mengine nadhani yeye ndio kaanza kupaniki,tulidhani atakua sober atoe speech very sober ila tunaona anatoa maneno ya kurukia hiki mara kile kuonesha yeye ndio kapaniki kupita maelezo

Eti ndio commander in chief....aisee tuna matatizo kuliko hata Corona yenyewe!
Hahahha kawakomesha!

Mlifikiri kelele zenu sasa zitamfanya aanze kulia lia kwamba sasa tunafanyaje, au mara hooo tutaleta chanjo, for what?

Nyie endeleeni kupiga domo nchi inasonga
 
Kuna chanjo isiyo na side effect ewe mwanasayansi?

Rais anadai chanjo ya cervical cancer ilisababisha watu wasizae. Ssa nikuhoji wwe mwanasayansi ni tiba gani ya saratani isiyo na side effects kwa mwili? Je exception ya 0.2% inahalalisha kuwa chanjo fulani haifai?

Kma mnaona wazungu ni wauaji kataeni ARV zao za bure, kataeni misaada ya mashine za MRI au CT Scan or wateva mnayodhani wanataka kutumalizia alafu mje na mbadala tuone.

Sio unakejeli dawa ya ugonjwa A hku unakubali dawa ya ugonjwa B while supplier ni mmoja!!
Nchi hii inawatu wa ajabu eti wanasayansi wetu? kwa lipi walilofanya hata panadol hawajui ni copy paste. hiyo chanjo ingekuwa mbaya si wangetuletea sisi huku mbona wameanza wao kuchoma na hata jana EU walikuwa wakali kutopata chanjo kwa wakati. Hizi dhana kuona mtu mkubwa anaongea inatisha. Cancer yenyewe ukitibia utapata shida sana, akaone watu wenye figo ingekuwa sio machine zao tungekufa kama kuku. Kila dawa ina athari lakini faida kubwa. watoto wadogo wanachomwa chanjo na wanapata homa lakini faida ni kubwa sasa aende apige ban na chanjo za watoto, leo hii vifo vya watoto vimepungua sana kwa ajili ya chanjo hizi za bure. kwanini tunashindwa kushukuru.
 
Mimi ni CCM damu damu lakini lazima niseme ukweli kuwa huyu jamaa ni kichaa. Haiwezekani rais wa nchi anaongea mambo ya kipuuzi na mna hii tena ni Dr. ambaye nchi imetumia hela kumsomesha.
Swali lako ni fupi tu,

Tangu kelele za korona zianze duniani kote, sasa yapata mwaka na ushee, Je, kuna nchi ambayo imefanikiwa kukomesha korona nchini mwake??

Kama hakuna, mbona ni makelele Tu yasiyo na majibu halisi ya kukomesha huo ugonjwa?

Chanjo siyo?? Mbona kelele zimezidi huko Kwa wenye chanjo?
 
Kwa hiyo huyo "mungu" anatusikia zaidi Watanzania kuliko hata Waisraeli tunakokwendaga kuhiji?

Za kuambiwa....................................... [emoji2089] [emoji2089] [emoji2089] [emoji2089]
Mungu siyo amstwrdam kwamba kwa vile tulimnyima kura Lisu basi hatajibu maombi yetu
 
Wakati mwingine ni vizuri kujifunza kuweka akiba ya maneno, msitake take sana kupotosha kauli za Dk.Magufuli mkisukumwa na itikadi zenu za vyama, yaani mnachukulia kila kitu kisiasa siasa tu.

Unambeza beza Dk.Magufuli kwa kuwa wewe si mwana sayansi, unachukulia kauli JPM anayo waonya Wizara ya afya pamoja na Watanzani, wewe onyo hilo unalichukulia kimzaa mzaa tu, lakini wana sayansi wenzake mbona tumemuelewa vizuri tu, sasa wewe puuzia ushauri wake, puuza kijifukizia na tahadhali nyingine kama za mwaka jana.Ukiona vipi,nenda Kenya au Afrika Kusini kadungwe chanjo za Oxford na washirika wake, halafu tuletee mlejesho baada ya wiki moja kupita.

Chunga sana,si kila king'aacho ni dhahabu/Almasi.
Eti wanasayansi.

Hebu kajifunze kuanzika vizuri kwanza ndio uje tujadiliane.
 
Hv unadhan aliewaita haya kuwa ni mataga alikosea???
Kuna chanjo isiyo na side effect ewe mwanasayansi?

Rais anadai chanjo ya cervical cancer ilisababisha watu wasizae. Ssa nikuhoji wwe mwanasayansi ni tiba gani ya saratani isiyo na side effects kwa mwili? Je exception ya 0.2% inahalalisha kuwa chanjo fulani haifai?

Kma mnaona wazungu ni wauaji kataeni ARV zao za bure, kataeni misaada ya mashine za MRI au CT Scan or wateva mnayodhani wanataka kutumalizia alafu mje na mbadala tuone.

Sio unakejeli dawa ya ugonjwa A hku unakubali dawa ya ugonjwa B while supplier ni mmoja!!
 
Had it not been for their stringent precautions as you have put it, they would be dying in thousands or tens of thousands a day! That is the power of epidemiology (the branch of medicine which deals with the incidence, distribution, and possible control of diseases and other factors relating to health)!
Be honest bro!! Despite their best efforts, they are still infected! The best way to control Covd 19, has not existed since it entered the world
 
Back
Top Bottom