Waziri Mwakyembe, ameamua kuuzika mpira wa tanzania kwa kuungiza siasa michezoni.
TFF waliopo amua kumfukuza kocha huyu waziri aliingilia kuwa hakuhusishwa , tuna mwambia aache unafiki mbona wakati TFF wana mleta haku sema kuwa alipaswa kushirikishwa kumtafuta kocha.
Sasa ameingilia uwekezaji wa klabu ya Simba, wakati Mo alipotaka kuweka asilimia 51 ni huyu huyu Mwakyembe aliye sema kuwa haiwezekani akawekeza kwa 51℅ na badala yake awekeze 49℅ , Mwakyembe lazima utambue kuwa simba si mali ya serikali, bali ni ya wanachama, siasa kwenye michezo imesha sababisha mighogoro kwenye mataifa mengi sana , na nadhani huyu waziri kuna wakati anafanya maamuzi wakati amelewa , inabidi achunguzwe sana na ikibainika kuwa ni mlevi wa kiwango hicho basi ni bora aachie ngazi.
Ni majuzi tu hata Bashite ( Makonda ) alitoa madai kuwa Yanga ni mali ya CCM.
Dunia ya leo Mpira ni biashara , na kama anataka Serikali izichukue hizi timu basi waanze kuzitolea ruzuku mara moja.
MWAKYEMBE acha kuharibu kabisa michezo hapa nchini.
Kuna siku alidai kuwa bondia aliye pigwa kule Ulaya alikoenda kushiriki mchezo wa ngumi eti afungiwe, kwani nini maana ya mashindano.
Na ndiyo maana inadhaniwa kuwa huyu waziri ni mlevi.
Acha siasa kwenye michezo , tafuta sehemu nyingine ya kutafutia hiyo misifa yako.