Rais Magufuli, tafadhali mtumbue Harrison Mwakyembe, wizara upande wa michezo imemshinda

Rais Magufuli, tafadhali mtumbue Harrison Mwakyembe, wizara upande wa michezo imemshinda

Wizara zenye upekee kama hizi zinatakiwa ataeuliwe waziri mwenye uelewa mzr wa mpira wa miguu na michezo yote kwa ujumla wake, siasa inatakiwa ziwe kidogo sana anapodeal na mambo kama haya.

Katika kauli zote tatu au nne alizotoa katika nyakati tofauti tofauti, sijaelewa hata moja kwakweli, na sina hakika kama hata yeye mwenyewe anaelewa anachokiongea.
Na kibaya zaidi ana PhD.
 
wala sijaelewa msingi wa hoja zako.
TFF wapongezwe kwa kipi,kuweka rekodi ya timu kuwa na viporo vingi (wao wanaita hatukujua/amini simba atafika robo fainali) yaani watu wasio na imani na timu yao na ligi yao tuwapongeze

Amunike kafukuzwa kwa lipi? zaidi ya miaka 30 huko afcon tunapasikia leo tunafikishwa na amunike ila tff wanamuona hafai

basi wangefanya kama TFF ya Misri timua kocha na wao wajiuzuru (maana ni sehemu ya kushindwa kwa timu)

suala la wachezaji wa kigeni yuko sahihi pia uwepo wa wachezaji wengi wa kigeni unabana fursa kwa wachezaji wazawa kuonekana matokeo yake ni kuwa na timu dhaifu (kama yenu)
 
Huyu mwakyembe miongoni mwa mawaziri ambao wana ubunifu 0% ndani ya hii tz yeye ndo nambari 1
 
Kwa kitendo ulichofanya cha kutaka kuihujumu timu yetu ya simba tunasema hatuna imani na wewe tena kwenye mpira wa miguu. Hii timu ya simba sio timu ya serikali bali ina wanachama wake ambao wanafanya maamuzi juu ya klabu. Na sisi ndio wanachama ambao tumeamua kumpa timu Mo Dewji na ametusaidia kufika robo fainali africa mpaka kusaidia Tanzania kuingiza timu nne mashindano ya africa lakini hilo hulioni. Tunakuomba ujiuzulu mapema kabla hatujafanya maandamano ya kukupinga hadharani.
Nawasilisha.
Naunga mkono hoja.

Mpira wa kisasa huu, sio wa mikutano na mabishano na kesi zisizoisha.

Iwekwe sheria kwa ajili ya kusimamia wawekezaji, ila waruhusiwe kuwekeza kadri wanavyoweza..

Yeye na kujifanya ana mapenz na ligi, mbona mdhamin tu wa ligi ameshindwa kutupapatia?

Leo anatokea mtu, anaweka kila mwaka bilion 5 na bado analipa mishahara na kuiboresha simba ndani na nje ya uwanja, we unaleta vikwazo unataka lazma wawe wa tatu, njoo na wewe uwe mdhamini wetu, timu ikupasue kichwa ndo ujue kuthamini bidii za watu.
 
Naona Mh.Waziri anaona Klabu ya Simba imetulia sasa anataka kuianzishia Mgogoro juu ya kulazimisha wawekezaji wawe 3 ili wamiliki hisa 49 badala ya Mo Dewji pekee yake.Binafsi naamini huo utakuwa ni mgogoro kwa ni Katiba ya Simba ilirekebishwa na kupitishwa na BMT kwanini BMT haikusema kabla.Namshauri Waziri aache kuleta Migogoro Klabu ya Simba inajiandaa na Mashindano Makubwa ndani na nje ya Nchi asitake kuivuruga.
 
PhD za bongo darasa la saba wana nafuu.

Mwanangu ntamsomesha elimu ya muhimu ya Form 4 tu; ya kujitambua na kuondoa ujinga.
 
Nmemsikiliza Leo nikamshangaa Sana na Wala sijamuelewa bado sababu ya hayo maamuzi ni nini au ametumwa
 
Mkuu wewe,ungekuwa karibu maana kwenye jokofu kabaki bata Nusu ningekugongea mlango nikupe.Sijui tunachokisomea nini,mimi naona haina faida yeyote elimu yetu zaid ya kupata njia ya kupokelea mshahara
PhD za bongo darasa la saba wana nafuu.

Mwanangu ntamsomesha elimu ya muhimu ya Form 4 tu; ya kujitambua na kuondoa ujinga.
 
Ndugu zangu neno MAENDELEO tulisikie tu,kwa hali hii ya watu wenyew tukubali sijui tumekanyaga wapi ili tukapafute
 
Heri hata serikali isiingilie hizi timu,mzee kolomoni na Akilimali wanafaa wafukuzwe kabisa,waziri anatuharibia timu
 
Vile vile anaposema wachezaji wakigeni wawewanacheza timu za taifa, hajui kuwa simba tumechukua wauza mitumba Brazil? Huyu mzee anachochea mgogoro kabisaaa
Naona Mh.Waziri anaona Klabu ya Simba imetulia sasa anataka kuianzishia Mgogoro juu ya kulazimisha wawekezaji wawe 3 ili wamiliki hisa 49 badala ya Mo Dewji pekee yake.Binafsi naamini huo utakuwa ni mgogoro kwa ni Katiba ya Simba ilirekebishwa na kupitishwa na BMT kwanini BMT haikusema kabla.Namshauri Waziri aache kuleta Migogoro Klabu ya Simba inajiandaa na Mashindano Makubwa ndani na nje ya Nchi asitake kuivuruga.
 
Tumpe siku tatu arekebishe kauli yake.. asipofanya hivyo mechi ya kesho kutwa Stars dhidi ya Kenya tumuonyeshe nguvu yetu. Hizi ni hujuma dhidi ya Simba. Na kesho KILOMONI atajifanya anamuunga mkono Waziri ili watuletee mgogoro
 
Hiyo ni njama imepangwa,waziri kaongea kwanza halafu kolomoni ndo anapata nguvu
Tumpe siku tatu arekebishe kauli yake.. asipofanya hivyo mechi ya kesho kutwa Stars dhidi ya Kenya tumuonyeshe nguvu yetu. Hizi ni hujuma dhidi ya Simba. Na kesho KILOMONI atajifanya anamuunga mkono Waziri ili watuletee mgogoro
 
Waziri Mwakyembe, ameamua kuuzika mpira wa tanzania kwa kuungiza siasa michezoni.
TFF waliopo amua kumfukuza kocha huyu waziri aliingilia kuwa hakuhusishwa , tuna mwambia aache unafiki mbona wakati TFF wana mleta haku sema kuwa alipaswa kushirikishwa kumtafuta kocha.
Sasa ameingilia uwekezaji wa klabu ya Simba, wakati Mo alipotaka kuweka asilimia 51 ni huyu huyu Mwakyembe aliye sema kuwa haiwezekani akawekeza kwa 51℅ na badala yake awekeze 49℅ , Mwakyembe lazima utambue kuwa simba si mali ya serikali, bali ni ya wanachama, siasa kwenye michezo imesha sababisha mighogoro kwenye mataifa mengi sana , na nadhani huyu waziri kuna wakati anafanya maamuzi wakati amelewa , inabidi achunguzwe sana na ikibainika kuwa ni mlevi wa kiwango hicho basi ni bora aachie ngazi.
Ni majuzi tu hata Bashite ( Makonda ) alitoa madai kuwa Yanga ni mali ya CCM.
Dunia ya leo Mpira ni biashara , na kama anataka Serikali izichukue hizi timu basi waanze kuzitolea ruzuku mara moja.
MWAKYEMBE acha kuharibu kabisa michezo hapa nchini.
Kuna siku alidai kuwa bondia aliye pigwa kule Ulaya alikoenda kushiriki mchezo wa ngumi eti afungiwe, kwani nini maana ya mashindano.
Na ndiyo maana inadhaniwa kuwa huyu waziri ni mlevi.
Acha siasa kwenye michezo , tafuta sehemu nyingine ya kutafutia hiyo misifa yako.
 
Amtumbue kivip wakati Mwakyembe ametoa maoni yake tu!!
 
Simba na Yanga wamiliki ni Chama pendwa ikitokea mtu kawa na nguvu kwenye hizi timu anakua anatishia uhai wa uwepo wa chama pendwa ndio maana yanga ikiwa sawa jua simba kuna shida pia simba ikiwa poa upande wa pili kuna jambo hakuna mwaka zote zitakua sawa keep in your mind ndugu
Maybe Yanga lakin sio simba. Tokea simba inapoanza haikuwa team yenye relation na ccm.. yanga ndio ilikuwa na mfungamano huo.

Simba anachotaka kufanya ni kuchange soka la tanzania kwenda viwango vya juu kabisa. Means style ya uongozi wa vilab lazima ichange.. hata wachezaji nao.
Sasa threat inatoka wapi? Kila siku tunataka soka lipande viwango.. akitokwa mwekezaji wa kubadilisha team wanaanza kulalamika. Kuna tatizo mahali.
Sometimes naona kaa umaskin na maendeleo duni tumeyakombatia wenyewe.
 
C Ndo Huyu Huyu Alokuwa Kwenye Ile Wizara Akaja Na Masharti Ya Ndoa Eti Lazima Cheti Cha Kuzaliwa. Wakatumbua Wakaleta Huku.

Sasa Kama Madhahifu Yashaanza Kuonekana Toka Akiwa Kule Tu, Unadhan Huku Kutakuwa Na Jipya? C Ndo Yale Yale Tu.

Hii Wizara Wamepewa Watu Hewa Tu.
 
Back
Top Bottom