Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Badala ya kutoa kauli ya kuwapa faraja wahanga wa tetemeko anakuja na kauli iliyojaa kibri! Kulikuwa na haja gani basi ya Serikali kupitisha bakuli lao la umatonya!? Kuna haja gani basi ya kuwa na kitengo cha maafa!?

Halafu akitoka hapo, "Nawaombeni Watanzania mniombee" nani atakuwa tayari kumuombea mtu mwenye kutoa kauli kama hizi kwa wahanga waliopata maafa na hasara kubwa kufuatia tetemeko la ardhi!? Dah!
Ushawahi jiuliza kuwa tumuombee wa nani
 
Serikali iwasaidie lakini si vizuri kuwapa ahadi hewa hasa kujenga nyumba zao. Labda serikali iwaondolee kodi kwenye vifaa vya ujenzi hasa cement, bati na nondo
Nyie watu mna vituko sana !sasa ikiondolewa kodi ndio wale masikini ya mungu watajenga?wewe mtu kwa kujipangia tu kujenga unaanza unanyoa punk unakuja kumaliza nyumba una kipara cha uzee na mvi hadi kwenye nyusi!
Serikali isikwepe iwasaidie au watu kwa asilimia tele tu,sio kusubiri washindwe maana hatujui watatumia kipimo gani kuhakiki kama mwananchi huyu kashindwa!
 
Serikali inapaswa ipeleke mchango wote uliopatikana na ugawanywe kidogo kidogo kutokana na watu walivyo athirika.

Serikali itakua imetimiza wajibu wa kusimamia michango.

Mambo ya mfanye kazi na hamjapeleka michango ya watanzania iliyochangwa si maneno ya hekima, wapeleke michango, then ndo waambiwe wamalizie kwa kufanya kazi kwa wale ambao michango haitotosha , mfano mtu aliyebomokewa na nyumba apelekewe huo mchango ajenge msingi, ndo aambiwe afanye kazi amalizie nyumba.


Katika hizo familia pia kuna wahitimu wanaosubiri ajira, mfanye kazi, ajira mmebana , huu si upuuzi.
Michango inapelekwa lkn haimaniishi wananchi wakae wabweteke kusubiri michango huo utakuwa ni upuuzi wa hali ya juu. Sio kosa ktk kauli ya rais
 
hii ni kweli ajali haikusababishwa na serikali ya CCM,je
ile balaa iliyo sababishwa kwa wakazi wa Mbagala na Gongo la Mboto walilipwa nini?Mbona wanaendelea na maisha....na hata wengine wamekwishisha sahau..
Hapa umenena mkuu kile kipindi serikali walirudishia miundo mbinu na kupiga X na kuzipa namba nyumba tu hakuna iliyojengwa licha ya kupewa ahadi, sasa serikali ya sasa haina ahadi za uwongo ,inachojua ni kukupa ukweli uliopo
 
Huko sumbawanga kuna kaya 24 nyumba zao paa zimechukuliwa na upepo. nao tena wanasubiri serikali ikawajengee mbona kazi ipo
Serikali itafilisika na itashindwa kuhudumia jamii maana kazi yake itakuwa ni kujengea waathirika wa maafa nyumba.
 
Kuwaambia wahanga wa tetemeko wafanye kazi na wasisubirie serikali hali ya kuwa wanatazama kwenye TV mapesa yao yanavyokusanywa ni kuwakosea kwa namna moja ama nyingine ,Ingawa kauli ilitawaliwa na upole ila naona kuna tatizo hapo huenda pesa hizi za wahanga hawa ZIKAELEKEZWA KATIKA JAMBO LINGINE hasa ukizingatia kauli kuwa tetemeko halikuletwa na serikali.
Inashangaza kuona mkuu huyu wa kaya anaonesha dhairi kuwa amegeuza tetemeko la Ardhi kagera kuwa source of Income katika taifa letu.
Sisi kma watanzania tunapaswa kujiuliza yale mapato yanayovuka malengo huwa yanakwenda wapi?
Iko wapi bajeti ya maafa na majanga kwa ujumla wake ili iweze kutumika katika wakati huu muafaka?
Kwanini serikali imeweza kutenga bajeti yake ya kuhamia dodoma kwa kipindi kifupi mno hali ya kuwa bajeti ya kuelekea huko haikuwepo wala kujadiliwa bungeni ?
Yapo mambo yanahitaji mwitikio wa haraka mno mfano hili la tetemeko kagera lakini serikali imetupa jukumu hilo kwa asasi za kiraia na mashirika mbalimbali ya kimataifa,hili swala halikuhitaji kujipanga zaidi ya siku tatu kwa wahanga hao.
Angalia misaada iliyotoka kwa watu wa sekta binafsi na wafanya biashara mbalimbali,hili linatosha kuonesha swala hilo halikuhitaji kujipanga kama serikali ya mkuu wa kaya inavyodai kutaka kufanya hivyo,sasa wafanyabiashara na asasi za kiraia zilizochangia zinajiuliza kama walichangia mbona watu wanasema misaada yetu haikuwafikia? Ndio maana leo ITV habari mbili za tetemeko kagera zinaonesha wanyonge wakilalamika kutofikiwa na misaada hiyo.
Tanzania sio nchi tajiri ni nchi masikini inayotaka kujikwamua.
Tanzania nchi yangu nitaipenda na kuitahamini kwa moyo wangu wote.
Magufuli rais wangu nitakusifia itakapobidi kwa furaha na shangwe.
 
Mbona hakuna baya aliloliongea hapo.....inawezekana kuna watu mna comment kabla hamkusikiliza hiyo clip.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Nakumbuka ule wa wimbo wa Abdul MIsambano na TOT 'masimango'
 
Ni bora anyamaze maana akiongea lzma alete mtafaruku
 
ni kushukuru kawambia kuhusu tetemeko kutoletwa na selikari. kama mbeza watu walidiriki kuishukuru serikal kwa kupeleka kupatwa kwa jua. hao kagera wangeshindwa kuilaani serikali kupeka tetemeko huko?
 
Mkuu waathirika wa ukimwi wanapewa dawa na serikali za kupunguza makali ya mashambulizi ya vinyemelezi sembuse Zilzala!!!
Hata kama huna akili lakini hapa umepitiliza.
Mbona unachokiandika wewe ni tofauti na kinachoelezwa kwenye hiyo habari? Maneno mazito yako wapi hapo?

Ni kweli, wananchi wanatakiwa wasibweteke kusubiri misaada ya serikali ili kuendelea na ukarabati sehemu zilizoharibika.

Kwa sababu serikali itachangai sehemu itakayoweza na siyo kuwaaminisha waathirika mambo ambayo hayawezekani kama ilivyotokea kule Kahama.
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.


OMUHAYA AKAGAMBA ATI: BAHAYA TWEMANYE!
 
Anapowaambia wajenge UKUTA nadhani anawatega tu ili wakamatwe na Polisiccm.
 
Back
Top Bottom