Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Na bado mnajipinda kulipa kodi kwa hii serikali ya ajabu ajabu!
 
Mh. Raisi amesema watu wafanye kazi wasibweteke wasisubiri serikali kuyafanyia kila kitu. Tetemeko limeshatokea serikali itarekebisha miundombinu aliyoharibika na itwasaidia wananchi katika yale itakayoweza.
Sasa ahadi hewa ni kawaambia wananchi serikali itawajengea nyumba zenu zote, itawapatia mahitaji yenu yote wakati wakijua serikali haina uwezo huo, mwisho wa siku wakishindwa kutekeleza ndiyo inakuwa mtaji kwa wanasiasa wa Upinzani
We umeona mbali na tatizo letu tunapenda kubembelezwa hata pasipo na uwezekano, wajitahidi tu ndugu zetu hata hizo pesa zikichangwa kiasi gani haziwez kucover all their loses bora ujianzie serikali ikija umalizie ubaki na akiba walau
 
SERIKALI HAIJENGI UKUTA - wanasiasa msijinufaishe -mmmmh-
 
Kunywa uji wa chumvi hakuna na ukosefu wa sukari au kipimo cha shida
 
Mbona unachokiandika wewe ni tofauti na kinachoelezwa kwenye hiyo habari? Maneno mazito yako wapi hapo?

Ni kweli, wananchi wanatakiwa wasibweteke kusubiri misaada ya serikali ili kuendelea na ukarabati sehemu zilizoharibika.

Kwa sababu serikali itachangai sehemu itakayoweza na siyo kuwaaminisha waathirika mambo ambayo hayawezekani kama ilivyotokea kule Kahama.
Hayo ndio maneno mazito mkuu!!Kwani unafikiri tamko lolote au neno lolote toka kwa Rais wa nchi linakuwa jepesi?Haya ndio maneno mazito tuliyoyasubiri toka kwa Rais baada ya week nzima ya majanga...Au kwako maneno ya Rais ya aina hii ni maneno mepesi??
 
Waanze kufyatua tofali, wachome mengne watasaidiwa ,walioumia sawa ila kama umetoka mzma nyanyua kuta,tulideka sana watz now tujue kujiongeza
Bwana heee,hivi unajua kwa Tanzania kumiliki nyumba ni shughuli pevu sana,kwa halii ya kiuchumi watu washapatwa na majanga alafu ndo waanze pandisha nyumba inawezekana ila co kirahisi hvy,maana wengine ndo wachangishane ukoo mzima.
 
Yuko sawa ... Kujengea wananchi nyumba sio kazi ya serekali ... Kama ungekuwa hivo tusingejenga miaka yote tungesubiria tujengewe... Kazi ya serekali Ni kutengeneza miundo mbinu ya public kama barabara shule madaraja hospital maji UMEME tutimize wajibu wetu kama watanzania bana khaaaaa... Namkubali magufuli ...# raiskeshasema#
 
Waanze kufyatua tofali, wachome mengne watasaidiwa ,walioumia sawa ila kama umetoka mzma nyanyua kuta,tulideka sana watz now tujue kujiongeza

Ulaaniwe ufe uzame na wewe huko utakapokuwa unasafiri
 
Sasa si ni bora angeendelea tu kukaa kimya? Ningekuwa nimempigia kura ningechomelea mbali ID yangu ya kupigia kura.

Na kesho tutaambiwa kuwa ilikuwa ni utani kwa wakwe zake!
 
Bwana heee,hivi unajua kwa Tanzania kumiliki nyumba ni shughuli pevu sana,kwa halii ya kiuchumi watu washapatwa na majanga alafu ndo waanze pandisha nyumba inawezekana ila co kirahisi hvy,maana wengine ndo wachangishane ukoo mzima.
Hata kufyatua tofali la tope ni shughuli?
 
Serikali imeshindwa kutimiza WAJIBU wake kama mkusanya kodi. Ningeamini kuwa ni 'msema kweli' kweli kama angeanza kwa kuuambia umma kuwa serikali ilishindwa kuwahisha huduma inayostahiki kama serikali. Sasa kwa nini asiwapelekee hiyo misaada inayoombwa na kusimamiwa na serikali na kuwaambia wao wandelee kwa juhudi zao pale misaada inapoishia. Aje aone kama kuna mtu atamlaumu au kulaumu serikali. Huyu mtukufu tukimwita majina mabaya mnaishia kutunyanyasa, lakini ni binadamu wa aina ya ajabu.
michango itasaidia kuboresha miundo mbinu na kuwapa mahema ya kujisitiri ila wafanye kazi wanaanze wao serikali itawapa taff watakapo shindwa
 
Back
Top Bottom