Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Kwa uelewa wake mkubwa wa kitukufu ikiwa ni juu ya phd, hiyo ilikuwa ni tafisda ya kusisitiza kuwa wahanga wasikae kusubiri wala kutarajia kuwa serikali ina jukumu la kuwasaidia (kwa sababu siyo iliyoleta tetemeko hili). Pengine limeletwa na UKAWA au UKUTA.
 
Nagazengele numba ami ng'wana?Onene yaya gete!yalinukuliwa maneno hayo na wakazi wa Mwakata Kahama iliponyesha mvua ya matofali ya mawe, yakisemwa na mtu mkubwa sana nchi hii
 
Wanawake ni viumbe wa ajabu sana,naamini Mungu aliwapa wanawake moyo wa kipekee sana,moyo wa uvumilivu na upendo.Wakati jamii inashangazwa na baadhi ya mienendo ya wanaume,mienendo ya ubabe na kutojali,wanaume hao wanaoonekana wa ajabu huku mitaani hutoka katika familia zao.

Pamoja na mitazamo hasi juu ya wababe hawa,nyuma yao kuna wanawake wavumilivu,waliowapenda jinsi walivyo na waliotayari hata kuhatarisha Maisha yao kwa kuwatetea.Laiti wanadamu wote wangeumbiwa moyo wa kike,naamini dunia ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.Hongereni Mama zetu,kwani wababe wote tunaowashangaa katika dunia hii,pamoja na ubabe wao bado mnamudu kuishi nao!!Kama haya ndiyo tunayashuhudia sisi tulio nje ya nyumba,Mama aliye ndani anashuhudia na kuona mangapi?Asanteni akina mama.
 
Nchi hii tulizoea kauli za kinafiki zisizotekelezeka, sasa tumepata Raisi anayenyoosha maneno hata kwenye wakati mgumu ni kuongea ukweli tu kwa kwenda mbele.
Kwa wapinzani ni haki yao kikatiba kubeza ukweli ambao umesemwa na Mh raisi, wao walitaka Raisi atoe ahadi zisizotekelezeka ili ije kuwa mtaji wa kisiasa huko mbeleni.
Hizi ni zama za kunyoosha maneno, mh raisi ameanza na sisi huku kitaa tuige mfano wako maana tumekuwa jamii ya kinafiki kupindukia
You can't fool all the people all the time! Stop fooling us! Hawajahitaji kupewa ahadi hewa, wapo tayari kupokea hata hicho kidogo, ilimradi kimetolewa kwa nia ya dhati! Labda utuambie hiyo nia haipo!
 
Siku za kwanza watu mitaani walikuwa wanasema limeletwa na yeye sasasijui ulikuwa ni utani au chuki binafsi, alipokaa kimyaa zaidi hayo maneno yakazidi kukolea,ila watu waache imani za ajabu hakuna binadamu awezaye kuleta tetemeko, Naamin mh.rais ni mtu makini na anafuatilia haya majanga.
 
Mlisema Rais aseme sasa kasema kazua wengine tena je angefika huko huko je c yangeongezeka wengine?
 
Jamani ndo maana nikasubiri video,Rais kaongea vizuri kabisa,na kweli yaliyotokea yametokea,lazima tusonge mbele na turekebishe tunapoweza,na serikali pia inatusaidia.
 
Tujifunze kukabiliana na changamoto ya mabadiliko,ni bora kuambiwa ukweli kuliko ahadi za kisiasa,mfano ni kipindi cha Mzee wa msonga alivyosemaga serikali haina uwezo wa kuleta mvua na wananchi walimwelewa.
 
Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.
Kwani kasema uongo? Mbona ni kweli tupu? Nimesikia mpaka viongozi wa makanisa wanataka wajengewe makqnisa yao. Hii ni aibu. Wekeni bima nyumba zenu japo hata bima hazihusiki na majanga ya asili. Serikali haijengi nyumba ya mtu kwa majanga asili. Utapata turubali na hema kwa muda wakati unahangaika ku settle na si kujengewa nyuma. Amkeni!
 
Watu wameficha pesa wanatarajia serikali itatoa wapi pesa?
 
[emoji38] ninapo mkubali rais ni hapo tu,hakuna kumdanganya mtanzania eti nitakujengea nyumba halafu iwe historia, anachofanya anakwambia ukweli upate hasira ya maendeleo ujijenge usingoje serikali, Amen JPM
 
Back
Top Bottom