Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Hio ndio inapaswa kuwa kauli ya kiongozi...sio kuwapa watu matumaini hewa...

..huu ni wakati wa kuwafariji wahanga.

..siyo muda wa kutoa kauli za kukaripia.

..wengine wanaweza kumuona kama mtu asiyejali na aliyekosa huruma kwa waathirika.

..zaidi hakukuwa na haja ya kujibizana na wanasiasa waliokosoa namna serikali ilivyochelewa kuwasaidia wahanga.

..FOCUS yote iwe ktk kuwasaidia wananchi na siyo kulumbana na wanasiasa wenzake.

..Kwa kweli kauli hizi zinasikitisha na kushangaza.
 
Ni heri mwanasiasa anayetumia majanga Kama haya kujitafutia umaarufu kwa kutoa misaada maana atakufanya upate ahuweni kuliko mtu yule anayetoa maagizo matupu,wakati majanga yanapomkuta mtu yeyote Mara nyingi yanamkuta akiwa katika hali mbaya,huku ni sawa na kumwambia mfiwa abebe maiti yake akazike,sijui Kama mfiwa ana weza akawa hata na nguvu za kuchimba kaburi.
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Huyu jamaa ni janga kuliko tetemeko lenyewe
 
Maneno ya faraja bado yanahitajika zaidi katika jambo hili, watu wamepoteza familia zao, mali zao hivyo tuendelee kuwapa faraja.
Sipati picha watu wamekaa msibani ndugu kafa, nyumba imebomoka, pakulala ni Shida, watoto wameanza kupata maradhi kutokana mabadiliko ya aina ya maisha na mateso. Halafu wanasikia Rais kwa Mara ya kwanza atatoa neno hivyo wanahamu na matumaini ya kumsikia atasema nini lakini wanaishia kuambiwa "msibweteke fanyeni kazi kujinusuru serikali haiwezi kufanya yote. Tetemeko halikuletwa na Ccm"
Lol, kweli hilo ni janga juu ya janga.
 
Nimemsikia akisema waathirika wa tetemeko la ardhi wafanye kazi wasikae tu kusubiria Serikali iwasaidie, tetemeko halijaletwa na Serikali
Ndio baadhi yetu tulikuwa tunasema kukaa kwake kimya ilikuwa ni heri. Akifungua kinywa tu, basi kuna watu ikiwa ni pamoja na wahanga wa janga hili watakwazika. Kazi ya serikali ni nini? Kwa nini basi serikali inakusanya kodi? Ndio, watu wachangie na waliishaanza kuchangia lakini ilikuwa ni WAJIBU wa anayekusanya kodi kuwa wa kwanza ama kutangulia kutoa huduma ya kwanza na kutoa uelekeo wa kitaifa katika kipindi cha masaa 24. Itamchukua muda mtukufu kujua majukumu ya serikali.
 
Hilo la kusema watu wajiongeze wasisubir serikal ni ukwel fulan mchungu ambao hatuwez kuukubali.
Kwa maana kuna mtu anaweza kua na ufa tu Ila akakaa kusubir....
As long as una uwezo wa kufanya kitu fulan basi uanze nacho.
Hali mbaya na Mwenye uwezo hawezi ngoja serikali

Kuna mwenzetu mama yake anastaafu this December amepatwa na tetemeko!!

Nyumba yoteeee....imeondoka just imagine!

Ila wameshanza harakati za kumtafutia pa kukaa!

Ila kwa hali za wabongo watu wameunga mpk kupata kinyumba kimoja halafu ndo kimetetemeshwaa!!!

hatariii!
 
Ndiyo mkuu! Kama kuna walioamini kuwa kupatwa kwa jua kuliratibiwa na serikali tukufu ya Jpm na kuamuliwa kuwa tukio hilo lifanyike Mbeya wanashindwa vipi kuamini kuwa tetemeko ni kazi ya serikali? Kama ujinga Ni mtaji basi serikali ina 99% ya share zote.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwa nini Mungu anatuadhibu hivi jamani?
Yaani naamini hata Lubuva achilia mbali kikwete wanajuta laiti wangejua!!

Kwa maana ingeleta tetemeko ndio ingepaswa kusaidia (serikali)

Kohelethi hakukosea aliponena juu ya kumtumainia mwanadam.
 
Back
Top Bottom