Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Uko sawa Amri jeshi wetu My.John Joseph Pombe Magufuli.
 
Nimemsikia akisema waathirika wa tetemeko la ardhi wafanye kazi wasikae tu kusubiria Serikali iwasaidie, tetemeko halijaletwa na Serikali
kama kiongoz hakupaswa kuzungumza hivyo. Nimekuja kugundua kitu flan the president is proud.

Ila angalau kaongea mioyo yetu imetulia. Ndiye baba yetu kichwa cha nyumba. Akitaamka ni amri tutafanyaje.
 
Hii yote shauri ya Pasco kung'ang'ania eti "sema neno moja tuu na roho yangu itapata ahueni"
Ona sasa neno gani hilo? Kwani nani kasema tetemeko limeletwa na Ccm?
Halafu hata hilo la kusema watu wafanye kazi wasibweteke hata kama ni ukweli sio wakati wake huu wakiwa msibani.
Mzee aendelee kukaa kimya inatosha
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Wengine tulisema bora akae kimya, akiongea tutapoteana humu.....na kweli yametokea. ...
 
Back
Top Bottom