Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Na ni kama kawaida yake, huwa akijitokeza kuzungumza tu, lazima azue mjadala usio hata na ulazima!

Sasa kwa mtazamo wake na waliomshauri kwa umoja wao anadhani kuna mtu aliyeathirika na janga hilo ambaye anaitegemea serikali imfanyie na kumpatia kila kitu kwa 100%!!!??

Mbona bado kuna watu na familia zao walioathiriwa na janga hilo, mpaka sasa hawajafikiwa hata na kiongozi yeyote wa serikali wala msaada wowote wa kibinadamu toka ktk serikali yanye kitengo maalumu cha maafa chenye bajeti tokana na kodi ya maskini haohao lakini wapo wanaendelea kuishi kwa "kujiongeza" wao wenyewe!!??

I think, Mr President could have said something sympathetic better than what he just said....kama hana kitu, watu wanaweza kumuelewa tu kwa kuongea kwa lugha njema especially kwa sasa ambao watu wamepoteza ndugu zao, mali na makazi yao!!

Bado engo ya matumizi ya lugha kwa kuzingatia situation inamsumbua sana bwana mkubwa huyu!!!
 
wakati Mr Kimya anaongea ,Mr Piko alikua anakunja kunja uso dizaini kama alikua anawasiwasi wa matamko
 
Wabongo mi nawajua sana kwa kupenda kuteleza,wengine nyufa tu,wanasubiri serikali ije iwajengee
mkuu watu hawakutaka kujengewa hayo
Watu wanataka angalau kupata chakula na hata kujisitiri kwa mudaa
hata kauli piai natosha kama huna chochotee......

Sio lazima kwenda kumtiza mamgonjwa au mfiwa na fedha,uwepo wako ni faraja tosha,kwamba tupo pamojaa
 
[emoji38] ninapo mkubali rais ni hapo tu,hakuna kumdanganya mtanzania eti nitakujengea nyumba halafu iwe historia, anachofanya anakwambia ukweli upate hasira ya maendeleo ujijenge usingoje serikali, Amen JPM
Braza, kwahiyo nyumba za Migomigo ni kanyanga?
 
Nchi hii tulizoea kauli za kinafiki zisizotekelezeka, sasa tumepata Raisi anayenyoosha maneno hata kwenye wakati mgumu ni kuongea ukweli tu kwa kwenda mbele.
Kwa wapinzani ni haki yao kikatiba kubeza ukweli ambao umesemwa na Mh raisi, wao walitaka Raisi atoe ahadi zisizotekelezeka ili ije kuwa mtaji wa kisiasa huko mbeleni.
Hizi ni zama za kunyoosha maneno, mh raisi ameanza na sisi huku kitaa tuige mfano wako maana tumekuwa jamii ya kinafiki kupindukia
Wakati mwingine maneno ya busara huhitajika sana.. Hasa mtu anapo pata dharura kama huko bukoba. Vijembe wakati kuna watu wamepoteza mali zao..
 
Niliandika kuwa serikali hii inakwepa majukumu , sasa serkali inatatua matatizo iliyoyaleta tu?
Hapana Mkuu kama ingekuwa hivyo ingewasaidia wananchi kwenye gharama kubwa ya sukari ambayo bila tsh. 3000 utalamba uji wa chumvi tu kama enzi zile maana malaika ndiye aliyesababisha janga hili
 
Badala ya kutoa kauli ya kuwapa faraja wahanga wa tetemeko anakuja na kauli iliyojaa kibri! Kulikuwa na haja gani basi ya Serikali kupitisha bakuli lao la umatonya!? Kuna haja gani basi ya kuwa na kitengo cha maafa!?

Halafu akitoka hapo, "Nawaombeni Watanzania mniombee" nani atakuwa tayari kumuombea mtu mwenye kutoa kauli kama hizi kwa wahanga waliopata maafa na hasara kubwa kufuatia tetemeko la ardhi!? Dah!

Mtu yuko nje..familia na watoto...amepoteza vitu vyake...hajapata hata hema bado afanye kazi..
 
Waanze kufyatua tofali, wachome mengne watasaidiwa ,walioumia sawa ila kama umetoka mzma nyanyua kuta,tulideka sana watz now tujue kujiongeza
Hivi unadhani watu wamenyoosha miguu na Ku relax kusubiri serikali? Kila familia hata zile masikini kiasi gani wanahangaika kwa uwezo wao. Hata ITV tumeona watu wanawajengea wasio jiweza bila msaada wa serikali. Hivyo maneno haya ya kukatisha tamaa hayafai, ni ya kikatili kupata kutolewa na serikali.
Nina uhakika sasa hivi hata michango itayumba kwa kukata tamaa.
Matembezi ya Leo ya Mwinyi kama yangekuwa ni kesho hakika hizo hela zisingepatikana namna hiyo.
 
..huu ni wakati wa kuwafariji wahanga.

..siyo muda wa kutoa kauli za kukaripia.

..wengine wanaweza kumuona kama mtu asiyejali na aliyekosa huruma kwa waathirika.

..zaidi hakukuwa na haja ya kujibizana na wanasiasa waliokosoa namna serikali ilivyochelewa kuwasaidia wahanga.

..FOCUS yote iwe ktk kuwasaidia wananchi na siyo kulumbana na wanasiasa wenzake.

..Kwa kweli kauli hizi zinasikitisha na kushangaza.

Kwahiyo wanasiasa wengine wanaruhusiwa kurusha madongo ktk wakati huu ila yeye tu ndo haruhusiwi kuwajibu wanasiasa wakati huu?
 
Hivi unadhani watu wamenyoosha miguu na Ku relax kusubiri serikali? Kila familia hata zile masikini kiasi gani wanahangaika kwa uwezo wao. Hata ITV tumeona watu wanawajengea wasio jiweza bila msaada wa serikali. Hivyo maneno haya ya kukatisha tamaa hayafai, ni ya kikatili kupata kutolewa na serikali.
Nina uhakika sasa hivi hata michango itayumba kwa kukata tamaa.
Matembezi ya Leo ya Mwinyi kama yangekuwa ni kesho hakika hizo hela zisingepatikana namna hiyo.
Kumbe wameanza? Basi vizuri...kwa maneno ya mkuu kasi itaongezeka zaidi
 
You can't fool all the people all the time! Stop fooling us! Hawajahitaji kupewa ahadi hewa, wapo tayari kupokea hata hicho kidogo, ilimradi kimetolewa kwa nia ya dhati! Labda utuambie hiyo nia haipo!

Mh. Raisi amesema watu wafanye kazi wasibweteke wasisubiri serikali kuyafanyia kila kitu. Tetemeko limeshatokea serikali itarekebisha miundombinu aliyoharibika na itwasaidia wananchi katika yale itakayoweza.
Sasa ahadi hewa ni kawaambia wananchi serikali itawajengea nyumba zenu zote, itawapatia mahitaji yenu yote wakati wakijua serikali haina uwezo huo, mwisho wa siku wakishindwa kutekeleza ndiyo inakuwa mtaji kwa wanasiasa wa Upinzani
 
[emoji38] ninapo mkubali rais ni hapo tu,hakuna kumdanganya mtanzania eti nitakujengea nyumba halafu iwe historia, anachofanya anakwambia ukweli upate hasira ya maendeleo ujijenge usingoje serikali, Amen JPM
Serikali imeshindwa kutimiza WAJIBU wake kama mkusanya kodi. Ningeamini kuwa ni 'msema kweli' kweli kama angeanza kwa kuuambia umma kuwa serikali ilishindwa kuwahisha huduma inayostahiki kama serikali. Sasa kwa nini asiwapelekee hiyo misaada inayoombwa na kusimamiwa na serikali na kuwaambia wao wandelee kwa juhudi zao pale misaada inapoishia. Aje aone kama kuna mtu atamlaumu au kulaumu serikali. Huyu mtukufu tukimwita majina mabaya mnaishia kutunyanyasa, lakini ni binadamu wa aina ya ajabu.
 
Back
Top Bottom