Ushawahi jiuliza kuwa tumuombee wa naniBadala ya kutoa kauli ya kuwapa faraja wahanga wa tetemeko anakuja na kauli iliyojaa kibri! Kulikuwa na haja gani basi ya Serikali kupitisha bakuli lao la umatonya!? Kuna haja gani basi ya kuwa na kitengo cha maafa!?
Halafu akitoka hapo, "Nawaombeni Watanzania mniombee" nani atakuwa tayari kumuombea mtu mwenye kutoa kauli kama hizi kwa wahanga waliopata maafa na hasara kubwa kufuatia tetemeko la ardhi!? Dah!
Nyie watu mna vituko sana !sasa ikiondolewa kodi ndio wale masikini ya mungu watajenga?wewe mtu kwa kujipangia tu kujenga unaanza unanyoa punk unakuja kumaliza nyumba una kipara cha uzee na mvi hadi kwenye nyusi!Serikali iwasaidie lakini si vizuri kuwapa ahadi hewa hasa kujenga nyumba zao. Labda serikali iwaondolee kodi kwenye vifaa vya ujenzi hasa cement, bati na nondo
Michango inapelekwa lkn haimaniishi wananchi wakae wabweteke kusubiri michango huo utakuwa ni upuuzi wa hali ya juu. Sio kosa ktk kauli ya raisSerikali inapaswa ipeleke mchango wote uliopatikana na ugawanywe kidogo kidogo kutokana na watu walivyo athirika.
Serikali itakua imetimiza wajibu wa kusimamia michango.
Mambo ya mfanye kazi na hamjapeleka michango ya watanzania iliyochangwa si maneno ya hekima, wapeleke michango, then ndo waambiwe wamalizie kwa kufanya kazi kwa wale ambao michango haitotosha , mfano mtu aliyebomokewa na nyumba apelekewe huo mchango ajenge msingi, ndo aambiwe afanye kazi amalizie nyumba.
Katika hizo familia pia kuna wahitimu wanaosubiri ajira, mfanye kazi, ajira mmebana , huu si upuuzi.
Hapa umenena mkuu kile kipindi serikali walirudishia miundo mbinu na kupiga X na kuzipa namba nyumba tu hakuna iliyojengwa licha ya kupewa ahadi, sasa serikali ya sasa haina ahadi za uwongo ,inachojua ni kukupa ukweli uliopohii ni kweli ajali haikusababishwa na serikali ya CCM,je
ile balaa iliyo sababishwa kwa wakazi wa Mbagala na Gongo la Mboto walilipwa nini?Mbona wanaendelea na maisha....na hata wengine wamekwishisha sahau..
Mambo ya sangoma hayo usizungumzie hilo jambo siku7
Serikali itafilisika na itashindwa kuhudumia jamii maana kazi yake itakuwa ni kujengea waathirika wa maafa nyumba.Huko sumbawanga kuna kaya 24 nyumba zao paa zimechukuliwa na upepo. nao tena wanasubiri serikali ikawajengee mbona kazi ipo
eeh si hapakazi tuMtu yuko nje..familia na watoto...amepoteza vitu vyake...hajapata hata hema bado afanye kazi..
mkuu unamchukia sana huyu mkuu wa kayaWatu wafanye kazi yeye amewapa ajira!? Au amewapa mikopo wafanye izo biashara...
Mbona unachokiandika wewe ni tofauti na kinachoelezwa kwenye hiyo habari? Maneno mazito yako wapi hapo?
Ni kweli, wananchi wanatakiwa wasibweteke kusubiri misaada ya serikali ili kuendelea na ukarabati sehemu zilizoharibika.
Kwa sababu serikali itachangai sehemu itakayoweza na siyo kuwaaminisha waathirika mambo ambayo hayawezekani kama ilivyotokea kule Kahama.
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.
Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.
Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.
Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.