Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Wataanzania tumekiingia cha kike, watu wanahitaji maneno ya faraja wanaenda kuambiwa hivyo kweli!
Kazidiwa tayari. Wakati ule nakumbuka alikuwa akinadi pesa ipo lakini leo serikali haijatoa hata tone wala yeye kwenda, hajaenda nafikiri ni kwasababu anahisi haina uharaka kwa vile tetemeko hakulileta yeye. Namkumbuka dogo mmoja wa mkoa wa Mara aliyemchangia pesa mwezi wa 2 na yule jamaa aliyemnunulia baiskeli ya kusukuma. Kwani matatizo yale yaliletwa na yeye/chama chake? tuamini kwamba anareact haraka kwenye mambo yatokanayo na CCM/serikali pekee? Ama kuna matatizo anayaona ni ya kisiasa na mengine si ya kisiasa? na kwani ni nani aliyekwenda kumwambia watu wanadai tetemeko limesababishwa na wewe/CCM? Mh. alikuwa ana defend nini katika hili? any way, the means justify the end.
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Anatania bhana....nadhani tutegemee kauli ya waziri mmoja ...baba anatania tu
 
Unafikiri hatujui alifanyaje mpaka akaupata urais? 2020 sio mbali panapo uhai
Ila watanzia weng walikua hawajui kua kura zao ndiyo mustakabil wa maisha yao 2020 ndo wanatajua umuhim wakufanya maamuz sahii na kuzitetea kula zao maana jamaa anawafundisha umuhim wa kura zao
 
Magufuli is very RIGHT. Maisha yanaendelea. Tusitegemee serikali kutumia rasilimali zake kuwajengea nyumba wahanga. In fact to me, Magufuli angetumia hiyo hela ya michango kukarabati mashule, hospitali na barabara zilizo athirika. Na ndo inapashwa kuwa hivo.

Hili janga ni funzo kwetu sote. Jamani katieni bima nyumba zenu na other valuable properties (by the way bima ya nyumba iko chini mno). Tatizo waswahili kila kitu tunakifanyia mzaha tukitumia visingizio lukuki. Lakini kwa mwenye akili dunia ya leo huwezi kujenga nyumba yako kwa hizi hela za kuokoteleza...ukashindwa kuikatia bima.

Najua wengi tutapiga kelele tukisingizia umasikini (this is a popular excuse so far in our country).......lakini ukweli unabaki. Dunia ya leo...haina msaada tena! Ni jukumu lako kufanya uwezalo kujikinga na haya majanga yasiyotabilika (umeme, mafuriko, tetemeko nk). Ndo maana utakuta wazungu hata akizeeka hawi mzigo kwa ndugu au serikali. Au hata akifa...ana bima yake ya kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele. They always work hard and save for the rainy day!

Leo hii baadhi ya waTanzania wenzetu walioko mambelezz (au hata hapa nyumbani) wanatangulia mbele ya haki...tunaanza kupitisha bakuli! (kusafirisha mwili). This is bad and we should correct this culture. Kateni bima za maisha kwa uhai wenu, nyumba zenu na mali nyinginezo. Tuache hii tabia ya kuishi kwa kutaka kuonewa huruma na binadamu wenzetu. Undugu au urafiki haina maana kwamba tuwe mizigo kwa wenzetu.

Maisha yako. Jukumu lako.

Masanja
 
Ndug zangu wabongo mnawafaham vizur? Mkuu anawafaham vizur sanai wabongo, tathimin inaendelea na wap watakaoambula mfuko wa cement tu huko, mtu ana nyufa tu anasubir msaada wa serikal, na kama angekurupuka kepeleka pesa daaah ingeishia kupigwa yote na wajanja, angekuwa mzee wangu JK fasta angereka mbele angerud na misaada kibao na nyote ingeishia DSM wangeishia kupigwa sound wahanga, mzee wangu alikuwa anajitoa sana ila ss watendaj wake daah walikuw shida anatafuta akiwakabidhi wanapiga yote. Kwaiyo kawaeleza ukwel hakuna shida
 
Mtu kapoteza ndugu wawili kwa pamoja, majeruhi watatu wapo hospital, nyumba yake iliyokua na kiduka chake nje zimeanguka, alaf unamwambia majibu ya kunya kama hayo hivi nyie magamba mlituletea aina gani ya binadamu huyu.
 

Umeongea vema lakini unajikanyaga kiapproach. Kama pia una PhD pia basi una shida kwa kuwa huna approach sahihi ya kumaliza tatizo. Labda nikupe changamoto 2 au 3 za kuanzia siku.

1. Nini maana ya politiks?

2.How cheap are CHADEMAs politiks and probably how expensive are CCM politics.

3. Kwa nini siasa zinafanyika kwenye maafa na sio majukwaani.

4.kwa kupitia tukio hili tunajifunza nini kama taifa kutowachukia matajiri kama tunavyotambua uwepo wa masikini na kuchukua hatua mahususi kupromote wealth zao

5.tunajifunza nini kama taifa kujenga umoja upendo na mshikamano kwa dhati na sio kwa kutumia msuli? Je mshikamano na upendo wa dhati unajengwa vipi katika taifa?

6. Je ni nini nafasi ya viongozi wa dini na siasa katika taifa? Je wanapaswa kuheshimiwa au kupuuzwa?

7.je. tetemeko ni jaribu au sio jaribu?

Umeongea kitaalamu jinsi ya kukabili maafa...lakini je...bila kujibu maswali hayo hapo juu inawezekana kweli?

Ngoja niachie hapo wengine wataendelea.
 
Mtu kapoteza ndugu wawili kwa pamoja, majeruhi watatu wapo hospital, nyumba yake iliyokua na kiduka chake nje zimeanguka, alaf unamwambia majibu ya kunya kama hayo hivi nyie magamba mlituletea aina gani ya binadamu huyu.
Duh!
 
Hela zilizochangwa zinaenda wapi!?
 
Kufanya kazi siku hizi imekuwa fasheni.ni kazi gani ambazo wana kagera walikuwa hawazifanyi mnataka wazifanye ? Kauli zenye ukakasi namna hii kwa watu waliopata majanga hazivumiliki hata kidogo.watu wale wanahitaji kauli za faraja hakuna anayependa kulala nje wakati ana uwezo wa kuezeka kwa nyasi banda lake akajihifadhi na familia yake kwani hizo nyumba zilizopata madhara hapo mwanzo serikali ndiyo iliwajengea hao watu. Wana kagera na watanzania kwa ujumla tuna jambo la kujifunza hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…