Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Badala ya kutoa kauli ya kuwapa faraja wahanga wa tetemeko anakuja na kauli iliyojaa kibri! Kulikuwa na haja gani basi ya Serikali kupitisha bakuli lao la umatonya!? Kuna haja gani basi ya kuwa na kitengo cha maafa!?

Halafu akitoka hapo, "Nawaombeni Watanzania mniombee" nani atakuwa tayari kumuombea mtu mwenye kutoa kauli kama hizi kwa wahanga waliopata maafa na hasara kubwa kufuatia tetemeko la ardhi!? Dah!
Mkuu kuna kauli zingine za kifedhuli kama hizi zinasababisha mtu awe hasira. Huyu kila anapoongea anatoa kauli tata zinazosababisha mijadala na hana tofauti na Mkuu wa mkoa wa Tanzania. Hata kama hataki kuwasaidia lakini hakupaswa kutoa kauli chafu hasa kipindi hiki cha majonzi
 
Huyu jamaa anajikinzani mwenyewe ama kwa makusudi au kwa kusahau haraka jana alizungumza nini.
Akiwa Pemba alijitapa sana kuwa hawezi kushirikisha mpinzani katika serikali yake, wakati siku chache zilizokuwa zimetangulia alikuwa amemteua Mwenyekiti wa TPL, Ndugu Augustino Mrema, kuwa mwenyekiti wa parole!
Wakati akiwa Unguja alimwakikishia Ndugu Shein kuwa akiletewa fyokofyoko yo yote amfahamishe na ata-respond katika muda wa dakika tano. Yanotokea maafa ya asili (ambayo hayakuletwa na serikali wala ccm) katika sehemu ya himaya yake (Kagera) analazimika kuahirisha ziara ya Zambia lakini anashindwa ku-deploy majeshi au kitengo cha maafa kusaidia wahanga si katika muda wa siku moja, bali hata baada ya siku saba za maafa!
Maafa ni fykofyoko? Lete fyokofyoko uone ya magu
 
Hivi ingetokea Chato kauli hizi zingetoka ?!
Ulitakiwa umuone wakati anasema ili uone body language yake na tone yake wakati anaongea, ungekuwa umemuelewa, ila mwenzangu naona unachukulia kama vile alikuwa anaongea kwa ukali, wenye akili na uelewa wamemuelewa rais.
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Tatizo tunafanya kazi na social media sana siku hizi hadi shida.. Tufanye reality sio SM..
 
Huyu rais ni wa ajabu kwelikweli. Ndiyo maana hata ameshindwa kutoa shukrani kwa mwenzie Kenyatta kwa msaada alioutoa kwa Tanzania! Anafedhehesha sana na kukatisha tamaa kwa kiwango cha hali ya juu kabisa.

Hayo maneno kutolewa na mkuu wa nchi bila hata kutoa shukrani kwa waliojitolea kuchangia misaada mbalimbali ni laana! Hivi haelewi ni yapi hasa majukumu yake?

Tanzania kwa sasa tuna janga!
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Ndio wapo wanaoamini hivyo maana wapo pia wanaoamini kupatwa kwa jua kuliletwa na serikali hivyo mkuu yupo sahihi kabisa. Nimeipenda sana hii maana lawama kwa serikali hazikomi utadhani serikali ni ya kinabii. Fanyeni kazi
 
Sasa kama ukuta umeanguka,ajengee kwa nini?,mate au tope,manake hapo anahitaji saruji ya kutumia,hela hana afanyeje au akaibe. Au kakusudia watu wajenge Nyumba zao za fito na tope, ndio tu arudi kule kuishi kama shetani,ulimbukeni mbaya sana.🙁
 
Ulitakiwa umuone wakati anasema ili uone body language yake na tone yake wakati anaongea, ungekuwa umemuelewa, ila mwenzangu naona unachukulia kama vile alikuwa anaongea kwa ukali, wenye akili na uelewa wamemuelewa rais.
Ndugu yangu kumbuka waathirka wengine kule Bkb ni majeruhi, wengine ni wazee wanahitaji faraja tena mapema si makavu na michakato

Mfuko wa maafa ni hewa ?! Mpaka michango ya wiki mbli na zaidi ?!
 
Nirudie kusoma? Mimi nimemsikiliza kwenye video, nirudie kusoma, nisome wapi?

Wewe uliyemwelewa Rais fafanua alichokisema basi.

Nirudie kusoma? Tanzania kuna mwandishi anaeweza ku replicate kinachosemwa na mtu?

Nimemsikiliza yeye Mwenyewe Rais kasema watu wasisubiri misaada. Majaliwa katoka kuongea hapo hapo anasema misaada ya vifaa vya ujenzi inakuja. Inakuja kwa nani?

Misaada ya ujenzi inakuja kwa watakaochelewa kujenga wenyewe?
Anachonishangaza ni kuwa misaada hii ilitolewa haraka na Nchi rafiki na aliowaita mashetani wakitegemea itawafikia haraka walengwa kutokana na madhara yaliyowapata. Badala ya kuipeleka haraka kupunguza majonzi anatoa kauli chafu. Huyu ni mtu asiye na huruma kwa watu wake cha msingi hapa wana kagera wanapaswa kuwa wavumilivu wasubiri 2020 ili wamtibu kupitia sanduku la kura
 
Duh???

Kwa kauli hii ya Mweshimiwa Rais kwangu Binafsi sijaipokea katika mtizamo chanya, alipaswa awatie moyo katika kipindi hiki kigumu walichopo na si kuwasimanga kwa maneno makali kiasi hiko.

Kwa hakika naanza kuona awamu hii itakuwa chungu sana juu ya wale wanaokaa jangwani endapo wakikumbwa na Mafuriko, ama wakazi wenzangu wa kule Kilosa, Mikoa ile yenye historia ya ukame kama Dodoma nao wajiandae kisaikolojia kwa maneno makali wakosapo chakula.

Nimeanza kukusoma Mkuu wa Kaya, Asanteeeeeee...!
 
Back
Top Bottom