Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Serikali iwasaidie lakini si vizuri kuwapa ahadi hewa hasa kujenga nyumba zao. Labda serikali iwaondolee kodi kwenye vifaa vya ujenzi hasa cement, bati na nondo

Hiyo ahadi ya kujengewa nyumba ilitolewa na nani, lini na wapi?
 
Kule kwetu wafiwa hawachimbi kaburi wala kupika na sio kuwa hizo kazi hawawezi ila ndo mila na desturi zetu watz sasa wapi tunakoelekea? Sio kila kitu ni cha kusema jamani ebu turudi nyuma wapi tulipokosea?
 
Si mlitaka aongee.. ? Haya kaongea sasa.... Na ndio maana hajaenda huko.. Akafanye nini na wakati hilo tetemeko hajalileta yeye?
Sawa.
Yule aliyeleta giza la mchana kule Mbeya na tetemeko Bukoba soon atajitokeza na kujibu hoja zote.Msijifiche tu siku hiyo.Huyo ndiye pekee ambaye HATANIWI wala KUJARIBIWA.
Subirini show.
 
Hawawezi kusema Mkuu haiwezekani apotee wiki nzima bila kutoa kauli yoyote kuhusu tetemeko, wiki moja baadaye ndiyo anatoa kauli lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu wiki nzima alifichwa wapi.
Mwishowe tutamuombea mabaya.
 
Akili, hekima na busara ni zawadi na neema kutoka kwa Mungu, si kila mmoja amepewa!
 
Ndio tufanye kazi tumekubali
Swali
Kwanini ulishindwa kwenda Zambia kufanya kazi?
Huyu jamaa anajikinzani mwenyewe ama kwa makusudi au kwa kusahau haraka jana alizungumza nini.
Akiwa Pemba alijitapa sana kuwa hawezi kushirikisha mpinzani katika serikali yake, wakati siku chache zilizokuwa zimetangulia alikuwa amemteua Mwenyekiti wa TPL, Ndugu Augustino Mrema, kuwa mwenyekiti wa parole!
Wakati akiwa Unguja alimwakikishia Ndugu Shein kuwa akiletewa fyokofyoko yo yote amfahamishe na ata-respond katika muda wa dakika tano. Yanotokea maafa ya asili (ambayo hayakuletwa na serikali wala ccm) katika sehemu ya himaya yake (Kagera) analazimika kuahirisha ziara ya Zambia lakini anashindwa ku-deploy majeshi au kitengo cha maafa kusaidia wahanga si katika muda wa siku moja, bali hata baada ya siku saba za maafa!
 
Magufuli ni fundisho kwa Watanzania kwamba nafasi ya urais sio ya kuchezea. Katika taifa lolote, the president is supposed to be the "symbol of unity", Magufuli hatoshi na iwapo tume ya uchaguzi itakuwa huru, atakuwa Rais wa kwanza wa CCM kutawala kwa muhula mmoja.

Uongozi wake ni wa ovyo na unaangamiza taifa lakini wale wale waliokuwa wanamtetea profesa JK kama Rais bora watakuja humu kumtetea Rais mwaribifu Pombe Magufuli.

Njaa na ignorance inatuangamiza!
 
Miaka mitano hii itakuwa kama century 🙂 🙂 lol! Wakagera hawakuomba tetemeko na wako kwenye shock. For God's sake haiwezekani hata wakati moja maneno sahihi yakatumika?
 
Hukumwelewa rais rudia kusoma


Nirudie kusoma? Mimi nimemsikiliza kwenye video, nirudie kusoma, nisome wapi?

Wewe uliyemwelewa Rais fafanua alichokisema basi.

Nirudie kusoma? Tanzania kuna mwandishi anaeweza ku replicate kinachosemwa na mtu?

Nimemsikiliza yeye Mwenyewe Rais kasema watu wasisubiri misaada. Majaliwa katoka kuongea hapo hapo anasema misaada ya vifaa vya ujenzi inakuja. Inakuja kwa nani?

Misaada ya ujenzi inakuja kwa watakaochelewa kujenga wenyewe?
 
Hata kwa mfano akiwa mgonjwa tukio likitokea lazima atokee, sasa Waziri mkuu na makamu wa nini?

Mimi ningekuwa mshauri wake, ningemshauri hivyo hivyo , fire kwa fire.

..Raisi akiwa mgonjwa lazima wananchi wapewe taarifa za ugonjwa wake na maendeleo ya afya yake kwa wakati.

..sasa hatujaambiwa kuwa Raisi alikuwa mgonjwa.

..kwamba unaona Raisi kulumbana na wanasiasa wakati taifa liko ktk maombolezo ni jambo la kawaida naomba kutofautiana na wewe. Naheshimu mawazo yako.
 
JANA NIKITIZAMA KITUO KIMOJA CHA TELEVISION, KIJANA MOJA KAPOTEZA FAMILIA NZIMA, MKE NA WATOTO, NA HANA MAKAZI YA KUISHI KUTOKANA NA TETEMEKO LENYEWE.
HIVI MTU KAMA HUYO AKIKUTANA NA KAULI KAMA HII ATAJISIKIAJE, NA HIYO KAZI ATAFANYAJE KWA MOLALI IPI KWA MFANO.??
Kwa kauli hii amefuta uzito wote wa ujumbe wa pole kutoka kwa Mr. Uhuru.
 
Kwani hizo pesa za misaada watu wanazichanga ni za serikali? Serikali haijatoa hata senti, pesa zote ni watu wamechanga
Kama hujui jambo ni bora kukaa kimya. Hakika usillolijua litakusumbua. Serikali ndiyo inayoratibu michango na lengo la michango hiyo ni kuwasaidia wananchi, wananchi huenda watasaidiwa vifaa vya ujenzi kama vile simenti, bati, mbao na misumari. Tusiwe na haraka ktk kukosoa, tukumbuke pia kuna miundombinu ya kijamii imeharibika ni pesa hizo hizo zitasaidia kuirejesha.
 
Ndugu zangu wana Kagera tujipange tu tujenge nyumba zetu..Serikali imeshasema haina msaada wowote kwetu...Mungu atatusaidia
 
..hajarushiwa madongo yoyote.

..ila naona kama yuko TOO SENSITIVE, anataka asifiwe hata pale alipokosea.

..kitendo chake cha kutoonekana akiwafariji waathirika ndiyo sababu ya kulaumiwa na wanasiasa wenzake.

..mimi ningekuwa mshauri wa Raisi ningemshauri asitumie kipindi hiki kulumbana na wanasiasa.

..huu ni muda wa KUWAFARIJI waathirika wa tetemeko la ardhi. We should focus on waathirika.

..Raisi akianza kujitetea ktk kipindi hiki cha MAOMBOLEZO kwa maneno kama "CCM haijasababisha tetemeko" inaoneka kama mtu anayejali maslahi ya chama na si maslahi ya waathirika.
Kila mara amesisitiza kuwa ni Rais wa wote. Hilo ni kweli kwasababu Rais ni kiongozi wa nchi
Kauli na matamko yanapaswa ku reflect maana hiyo ya Rais wa wote

Hata kama wapo watakaomtuhumu kichama, kazi ya kujibu kichama awaachie viongozi wenzake wa vyama. Yeye anatakiwa ajibu kama kiongozi wa wote

Kwahili tukio anaongea kama Rais wa wote na wanaomsikiliza ni wote
Ku insinuate tuhuma za uchama kunapoteza maana ya ujumbe.

Kwa mfano, hakukuwa na sababu za kusema tetemeko halikuletwa na CCM.
Mbona kila mtanzania anajua hilo!

Hili limekaribisha hoja nyingine kuwa, hajafika eneo la tukio licha ya kuahirisha safari.
Wapinzani waliokwenda wana haki ya kuzungumza na kufariji wahanga na wananchi

Sioni tatizo la kutoa misaada eti mpaka ipipitie ofisi ya waziri mkuu. Hii yote ni kuwa sensitive na wapinzani bila sababu. Lengo ni kuwasaidia watu, kama wahusika hawapo kuna tatizo gani watanzania wengine wakasaidia wenzao?

Kauli kama kubweteka inaondoa uzito wa ujumbe. JokaKuu alisema 'awe consoler in chief'
Si lazima ajibu kila tuhuma, lakini ni wajibu kuhakikisha hakuna anayeumia kwasababu tetemeko halitokei kwa waliobweteka, ni janga na hakuna aliyeomba ili asubiri msaada
 
Kenyata katoa mabati elfu 4, n.k.
Tukijenga nyumba za mgongo wa tembo zinazotumia bati 20, (chumba na sebule), tutajenga nyumba 200,
Kijazi na taasisi zake wametoa sh 1bn, ukigawa kwa 200, kila nyumba itajengwa kwa sh 5million.

Michango mingine itumike kusaidia yale mahitaji ya ghafla mfano chakula ,mahema, madawa,

Hayo ni mawazo yangu, ( nimechagua nyumba 200 ziwe kama mkono wa pole)
 
Back
Top Bottom