Bwana wee.... hata mimi nachoka kabisa, hakuna kinachoeleweka hapo. Nani kasema mafuriko yameletwa na serikali?
Na wanaposema watu wajenge kuta zao wasisubiri misaada ya serikali they don't make any sense. Majawali katoa speech hapo hapo kasema msaada mkubwa wanaohitaji kwa sasa na wanaopokea kwa wingi ili waupeleke kwa wananchi ni vifaa vya ujenzi. Sasa hao wanaopelekewa ni kina nani, watakaochelewa kujijengea?
Kwa sababu kama serikali inatangaza inaleta misaada ( which means vinakuja bure) ya vifaa vya ujenzi kwa nini niwahi kuingia gharama za kujenga?
Okay, au ujumbe ni kwamba tusipende vya bure, okay, kwa hiyo vinavyokuja vitauzwa? Kama vitauzwa basi tusubiri bei yao lazima itakuwa bei ya kutupa kwa sababu wenyewe wamepewa bure! Nothing makes sense here!
ITV wanasema Majaliwa amesema serikali inawashukuru wahisani wa nchi mbali mbali. Misaada iliyotoka ndani je, ni uchafu?
Wanasema Museveni na Kenyatta wametoa misaada, sielewi, hivi hizi ni pesa zao binafsi ama za serikali zao? Ahsante tumwambie nani, Museveni ama Waganda? Maana haya ni madikteta na makabaila, Mu7 na Kenyata, yanaweza kuwa na hela zao mifukoni. Marekani inapotoa misaada hawasemi Barack Obama ametoa misaada, tunaambiwa "KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"!
Hakuna kinacho make sense hapa, hakuna kinachoeleweka.
Kwa nini nijenge na misaada wanasema inakuja, anakuja kupewa nani, atakaechelewa kujenga?