Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Mbaaya sana hii. Poleni sana mliofikwa na kadhia hii.
Bora angendelea kukaa kimya tu!
 
Nawaambieni, Mungu hadhihakiwi hata kidogo, Majibu ya Maombi yenu kwa Mungu ndo yanaanza Jibiwa, Narudia tena Mungu wakat mwingne hugeuza Maombi kuwa laana
 
Nagazengele numba ami ng'wana?Onene yaya gete!yalinukuliwa maneno hayo na wakazi wa Mwakata Kahama iliponyesha mvua ya matofali ya mawe, yakisemwa na mtu mkubwa sana nchi hii
afadahali umeyanukuu kwa hiyo lugha
 
Hahahahahah



Unacheka nini mkubwa,kwani hukumbuki kusitasita kwa mama kipindi kile cha kampeni? Kusita kule kulikuwa ni ishara ya kutuonea huruma.Unakumbuka pia tetesi za juzi kuwa "Bi mkubwa alitaka kujiudhuru baada ya kuchoshwa na matumizi mabaya ya lugha na ubabe?" Alikomaa nimpe taraka lakini nilikataa ili kuilinda heshima yangu".
 
Sins uhakika sana kama magufuli anajua kuwa kuna uchaguzi 2020. Mtu amefiwa, mtu amedondokewa nyumba yake, yupo msiba anaufanyia kwa jirani kwa vile yeye hana nyumba imebomoka. Alafu unamwambia aache kubweteka tetemeko halikuletwa na serikali... Kweliii mh. Mh
 
Mbona unachokiandika wewe ni tofauti na kinachoelezwa kwenye hiyo habari? Maneno mazito yako wapi hapo?

Ni kweli, wananchi wanatakiwa wasibweteke kusubiri misaada ya serikali ili kuendelea na ukarabati sehemu zilizoharibika.

Kwa sababu serikali itachangai sehemu itakayoweza na siyo kuwaaminisha waathirika mambo ambayo hayawezekani kama ilivyotokea kule Kahama.
Habari za mwanzugi ngosha
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Si hao ukawa wameenda kujikusanya huko wakitaka kuwaamisha watu kama lile janga ni la ccm
 
naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Bwana wee.... hata mimi nachoka kabisa, hakuna kinachoeleweka hapo. Nani kasema mafuriko yameletwa na serikali?

Na wanaposema watu wajenge kuta zao wasisubiri misaada ya serikali they don't make any sense. Majaliwa katoa speech hapo hapo kasema msaada mkubwa wanaohitaji kwa sasa na wanaopokea kwa wingi ili waupeleke kwa wananchi ni vifaa vya ujenzi. Sasa hao wanaopelekewa ni kina nani, watakaochelewa kujijengea?

Kwa sababu kama serikali inatangaza inaleta misaada ( which means vinakuja bure) ya vifaa vya ujenzi kwa nini niwahi kuingia gharama za kujenga?

Okay, au ujumbe ni kwamba tusipende vya bure, okay, kwa hiyo vinavyokuja vitauzwa? Kama vitauzwa basi tusubiri bei yao lazima itakuwa bei ya kutupa kwa sababu wenyewe wamepewa bure! Nothing makes sense here!

ITV wanasema Majaliwa amesema serikali inawashukuru wahisani wa nchi mbali mbali. Misaada iliyotoka ndani je, ni uchafu?

Wanasema Museveni na Kenyatta wametoa misaada, sielewi, hivi hizi ni pesa zao binafsi ama za serikali zao? Ahsante tumwambie nani, Museveni ama Waganda? Maana haya ni madikteta na makabaila, Mu7 na Kenyata, yanaweza kuwa na hela zao mifukoni. Marekani inapotoa misaada hawasemi Barack Obama ametoa misaada, tunaambiwa "KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"!

Hakuna kinacho make sense hapa, hakuna kinachoeleweka.

Kwa nini nijenge na misaada wanasema inakuja, anakuja kupewa nani, atakaechelewa kujenga?
 
Ukweli upi alioongea wewe? Lini wahanga wa tetemeko la ardhi walilalamika kwamba tetemeko lililetwa na Serikali!? Kwanini wadhihakiwe katika kipindi kigumu kwao!? Acheni tabia ya kuunga mkono kauli za kuudhi kama hizi. Watu wamepoteza waume zao, watoto wao, wazazi wao etc badala ya kuambiwa maneno ya kuwaletea faraja wanakejeliwa!? Anaweza kutumia kauli kama hizi kwenye kuomba kura!? Mbona kwenye kuomba kura ni unyenyekevu wa hali ya juu!?
huwez jua labda amewafananisha na wale watu juzi juzi walishukuru serikali kuwapelekea lile tukio la kupatwa kwa jua kijijin kwao
 
Wataanzania tumekiingia cha kike, watu wanahitaji maneno ya faraja wanaenda kuambiwa hivyo kweli!
Mkuu... Kwanini tusitumie akili zetu wakati mwingine? Kuna ubaya gani kimwambia mtu fanya unapoweza serikali itafanya utapoishia? Ulitaka awape maneno ya kutia moyo kuwaridhisha tu!... Unafiki ndio umetufikisha hapa .... Asante Magu si mnafiki.
 
Back
Top Bottom