Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Nilitegemea kusikia serikali imetenga kiasi gani kwa ajiri ya wahanga wa tetemeko badala yake anaongelea juu ya hela iliyochangwa na wasamaria wema wa ndani na nje ya nchi.
Ambazo serikali imeshindwa kuzipeleka Kagera kusaidia matatizo ya awali wakati rehabilitation ikifuatia baadae.
Kwenye taarifa hiyo hiyo ya saa mbili wahanga wamelalamika kwa mwandishi ya ITV Audax Mutiganzi kuwa siku 7 zimepita bado wanalala nje bila msaada wowote kila kukicha wanapita watu wa kutathimini madhara as if huo ndio msaada.
 
Ndiyo mkuu! Kama kuna walioamini kuwa kupatwa kwa jua kuliratibiwa na serikali tukufu ya Jpm na kuamuliwa kuwa tukio hilo lifanyike Mbeya wanashindwa vipi kuamini kuwa tetemeko ni kazi ya serikali? Kama ujinga Ni mtaji basi serikali ina 99% ya share zote.
Lakini la mbeya halikutolewa majibu ya ufafanuzi au kwakuwa lilijaa shukrani na si lawama?!
 
Tunammiss mzee zaifu kwakweli. Hata suala kama hili nilitegemea angeenda huko na kujulia hali na sio kupata taarifa ya mambo yanavyokwenda.
Maneno yake yana ukakasi sana
 
Lakini afadhali kawaeleza ukweli ingawaje mchungu. Nafikiri kipindi hiki watu watatia akili tu.
Tumezoea longolongo na kutiana moyo kwenye hakuna, bora awaandae kisaikolojia kuliko kufanya tulivyozoea
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kuna usahihi katika kauli ya Rais hasa kwa wale wanaoutumia haya Majanga kama njia ya kubweteka, maana majanga yameshatokea na maisha yatendelea na serikali haitaweza kusaidia kila mtu , mfano wale wanaotaka wajengewe Nyumba na serikali.

hata hivyo kuna ambao hawataweza kufanya shughuli zao za kila siku mpaka mambo yawe shwari.
Hakuna aliyewahi kupatwa na janga akaitegemea serikali maisha yake yote, kwani majanga mangapi tushashuhudia hapa Tanzania na watu si wanaishi?

Kinachotakiwa serikali ina rescue kwenye peak ya disaster ndio maana ina kitengo cha maafa chini ya mtendaji mkuu wa serikali na kinatengewa bajeti kila mwaka. Isitoshe serikali ina influence ya kuchangisha wahisani kama tulivyoona imefanya juzi.

Kusema eti wahanga wafanye kazi wasibweteke si sahihi achilia mbali msemaji wake ana nafasi gani kitaifa!

Mara ngapi tunaona kila mwenye tatizo iwe ni migogoro ya ardhi au hata ajari za barabarani watu wanakimbilia kusema tunamuomba rais aingilie kati, tunaomba atusaidie nk nk? Si ni kwa vile hiyo ni nafasi inayotegemewa na wengi kwa huruma na uwezo ndio maana wanaamini ina majibu ya shida zao au?
 
Unatia aibu.... Ni hasara kwa familia yako maana hawana mlezi!

Maneno ya faraja yanasaidia nini sasa ikiwa ukweli watu wanahitaji kukarabati makazi yao?

Yani familia yako haina msosi alafu unawapa maneno ya faraja kwamba msijali chakula mtapata tu! Badala ya kuwambia jishughulisheni wewe unawaambia watandike mikeka wakae wasubiri kuletewa?

Hovyo kabisa
Nadhani humu jukwaani kuna na wagonjwa wa fikra! Hili janga halikuletwa na serikali na wala hao walioathirika hawakuliita!

Mali zimeharibika, watu wamekufa na wengine kujeruhika wako hospitali na wengine wamepata vilema, kisha unawaambia wasibweteke saa hizi ndani ya siku saba za tukio kweli?!

Haya bwana ngoja tuone japo Tanzania si kura ya mpiga kura inayompa mtu madaraka au cheo, lakini japo utu ni muhimu jamani daah!!
 
It's me again Jah,as I fall on my knees today
Help them God I pray,don't wanna dem carried away
It's me again Jah,as I fall on my knees today
Help them God I pray,preserve their souls today..

Help them God I pray,preserve Kagera today and forever.

Ndugu zetu wote huko Kagera,pamoja sana.
Misaada yetu tunaileta huko sana tu,sio lazima kujulikana.
Pamoja sana.
Wanaoongea waendelee kuongea,wanaotenda waendelee kutenda,ila siku inakuja kila mtu ataitoa hesabu ya maneno na matendo yake mbele ya haki.
 
Si mlitaka aongee.. ? Haya kaongea sasa.... Na ndio maana hajaenda huko.. Akafanye nini na wakati hilo tetemeko hajalileta yeye?
 
Back
Top Bottom