Huyu jamaa anajikinzani mwenyewe ama kwa makusudi au kwa kusahau haraka jana alizungumza nini.
Akiwa Pemba alijitapa sana kuwa hawezi kushirikisha mpinzani katika serikali yake, wakati siku chache zilizokuwa zimetangulia alikuwa amemteua Mwenyekiti wa TPL, Ndugu Augustino Mrema, kuwa mwenyekiti wa parole!
Wakati akiwa Unguja alimwakikishia Ndugu Shein kuwa akiletewa fyokofyoko yo yote amfahamishe na ata-respond katika muda wa dakika tano. Yanotokea maafa ya asili (ambayo hayakuletwa na serikali wala ccm) katika sehemu ya himaya yake (Kagera) analazimika kuahirisha ziara ya Zambia lakini anashindwa ku-deploy majeshi au kitengo cha maafa kusaidia wahanga si katika muda wa siku moja, bali hata baada ya siku saba za maafa!