Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Wataanzania tumekiingia cha kike, watu wanahitaji maneno ya faraja wanaenda kuambiwa hivyo kweli!
Kazidiwa tayari. Wakati ule nakumbuka alikuwa akinadi pesa ipo lakini leo serikali haijatoa hata tone wala yeye kwenda, hajaenda nafikiri ni kwasababu anahisi haina uharaka kwa vile tetemeko hakulileta yeye. Namkumbuka dogo mmoja wa mkoa wa Mara aliyemchangia pesa mwezi wa 2 na yule jamaa aliyemnunulia baiskeli ya kusukuma. Kwani matatizo yale yaliletwa na yeye/chama chake? tuamini kwamba anareact haraka kwenye mambo yatokanayo na CCM/serikali pekee? Ama kuna matatizo anayaona ni ya kisiasa na mengine si ya kisiasa? na kwani ni nani aliyekwenda kumwambia watu wanadai tetemeko limesababishwa na wewe/CCM? Mh. alikuwa ana defend nini katika hili? any way, the means justify the end.
 
Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Unafikiri hatujui alifanyaje mpaka akaupata urais? 2020 sio mbali panapo uhai
Ila watanzia weng walikua hawajui kua kura zao ndiyo mustakabil wa maisha yao 2020 ndo wanatajua umuhim wakufanya maamuz sahii na kuzitetea kula zao maana jamaa anawafundisha umuhim wa kura zao
 
Magufuli is very RIGHT. Maisha yanaendelea. Tusitegemee serikali kutumia rasilimali zake kuwajengea nyumba wahanga. In fact to me, Magufuli angetumia hiyo hela ya michango kukarabati mashule, hospitali na barabara zilizo athirika. Na ndo inapashwa kuwa hivo.

Hili janga ni funzo kwetu sote. Jamani katieni bima nyumba zenu na other valuable properties (by the way bima ya nyumba iko chini mno). Tatizo waswahili kila kitu tunakifanyia mzaha tukitumia visingizio lukuki. Lakini kwa mwenye akili dunia ya leo huwezi kujenga nyumba yako kwa hizi hela za kuokoteleza...ukashindwa kuikatia bima.

Najua wengi tutapiga kelele tukisingizia umasikini (this is a popular excuse so far in our country).......lakini ukweli unabaki. Dunia ya leo...haina msaada tena! Ni jukumu lako kufanya uwezalo kujikinga na haya majanga yasiyotabilika (umeme, mafuriko, tetemeko nk). Ndo maana utakuta wazungu hata akizeeka hawi mzigo kwa ndugu au serikali. Au hata akifa...ana bima yake ya kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele. They always work hard and save for the rainy day!

Leo hii baadhi ya waTanzania wenzetu walioko mambelezz (au hata hapa nyumbani) wanatangulia mbele ya haki...tunaanza kupitisha bakuli! (kusafirisha mwili). This is bad and we should correct this culture. Kateni bima za maisha kwa uhai wenu, nyumba zenu na mali nyinginezo. Tuache hii tabia ya kuishi kwa kutaka kuonewa huruma na binadamu wenzetu. Undugu au urafiki haina maana kwamba tuwe mizigo kwa wenzetu.

Maisha yako. Jukumu lako.

Masanja
 
Ndug zangu wabongo mnawafaham vizur? Mkuu anawafaham vizur sanai wabongo, tathimin inaendelea na wap watakaoambula mfuko wa cement tu huko, mtu ana nyufa tu anasubir msaada wa serikal, na kama angekurupuka kepeleka pesa daaah ingeishia kupigwa yote na wajanja, angekuwa mzee wangu JK fasta angereka mbele angerud na misaada kibao na nyote ingeishia DSM wangeishia kupigwa sound wahanga, mzee wangu alikuwa anajitoa sana ila ss watendaj wake daah walikuw shida anatafuta akiwakabidhi wanapiga yote. Kwaiyo kawaeleza ukwel hakuna shida
 
Mtu kapoteza ndugu wawili kwa pamoja, majeruhi watatu wapo hospital, nyumba yake iliyokua na kiduka chake nje zimeanguka, alaf unamwambia majibu ya kunya kama hayo hivi nyie magamba mlituletea aina gani ya binadamu huyu.
 
Tukiachana na cheap politics za CHADEMA and unethical conducts za viongozi wao; on a serious note tuna sheria luluki ambazo zinatoa framework jinsi ya ku approach national disaster na kuna body ambayo imeundwa na sheria 'disaster management act 2014' yenye majukumu ya kufanya research na kujua taratibu sahihi za kufanya intervention. Commonsense ni kujua kila disaster inakuja na changamoto gani, human resources zipi zinahitaji, skills za watu, mobilization, response time, contingency fund ya awali kabla ya misaada na mengine yote kuanzia early stage mpaka mwisho.

Hakuna anaekataa tetemeko la ardhi alifanyiwi na wanasiasa lakini kwakuwa serikari inatambua ya kuwa kuna hizo risks ndio maana ikatunga hiyo sheria. Sasa leo unajiuliza yuko huyu agency alietajwa na serikari ata kama jamii inatoa misaada si ni yeye ndiye alietakiwa kuwa anakusanya, kuwapa habari wananchi, pamoja na kuishauri serikari, wako hao ma expert wa haya mambo.

Serious Magufuli inabidi aingalie timu yake upya this is uncalled majuzi tumemaliza kupambana na kipindu kipindu hawa jamaa wanatakiwa wajue kwenye situation kama hizo mlipuko wa magonjwa ni risk nyingine, kuna watu bado wanashocks wanahitajia assurance to build their confidence sio lazima kupewa pesa, kuna watu wanamajonzi wamepoteza ndugu zao, kuna watu bado wako hospitali surely lazima lugha sahihi itumike na namna sahihi ya kuwapa faraja hawa wananchi sio lazima pesa ata empowerment to move forward.

I mean I can go on and on about this issues lakini ifike wakati waanze kukagua hizi Phd maana hawa ndio wanaopewa accountability kubwa na uwezo wao hafifu ndio unaopelekea kuzorota kwa sehemu nyingi; halafu mtu ukipekuwa kidogo kuangalia kama kuna tofauti na wengine wanavyofanya duniani unakutana na frameworks zile zile za dunia ya kwanza ila response and implementation zake toafauti sasa hawa wasomi walipitia modules tofauti au vipi (imagine tetemeko la ardhi linatokea on busy district si hatari).

Umeongea vema lakini unajikanyaga kiapproach. Kama pia una PhD pia basi una shida kwa kuwa huna approach sahihi ya kumaliza tatizo. Labda nikupe changamoto 2 au 3 za kuanzia siku.

1. Nini maana ya politiks?

2.How cheap are CHADEMAs politiks and probably how expensive are CCM politics.

3. Kwa nini siasa zinafanyika kwenye maafa na sio majukwaani.

4.kwa kupitia tukio hili tunajifunza nini kama taifa kutowachukia matajiri kama tunavyotambua uwepo wa masikini na kuchukua hatua mahususi kupromote wealth zao

5.tunajifunza nini kama taifa kujenga umoja upendo na mshikamano kwa dhati na sio kwa kutumia msuli? Je mshikamano na upendo wa dhati unajengwa vipi katika taifa?

6. Je ni nini nafasi ya viongozi wa dini na siasa katika taifa? Je wanapaswa kuheshimiwa au kupuuzwa?

7.je. tetemeko ni jaribu au sio jaribu?

Umeongea kitaalamu jinsi ya kukabili maafa...lakini je...bila kujibu maswali hayo hapo juu inawezekana kweli?

Ngoja niachie hapo wengine wataendelea.
 
Unatia aibu.... Ni hasara kwa familia yako maana hawana mlezi!

Maneno ya faraja yanasaidia nini sasa ikiwa ukweli watu wanahitaji kukarabati makazi yao?

Yani familia yako haina msosi alafu unawapa maneno ya faraja kwamba msijali chakula mtapata tu! Badala ya kuwambia jishughulisheni wewe unawaambia watandike mikeka wakae wasubiri kuletewa?

Hovyo kabisa
Hela zilizochangwa zinaenda wapi!?
 
Kufanya kazi siku hizi imekuwa fasheni.ni kazi gani ambazo wana kagera walikuwa hawazifanyi mnataka wazifanye ? Kauli zenye ukakasi namna hii kwa watu waliopata majanga hazivumiliki hata kidogo.watu wale wanahitaji kauli za faraja hakuna anayependa kulala nje wakati ana uwezo wa kuezeka kwa nyasi banda lake akajihifadhi na familia yake kwani hizo nyumba zilizopata madhara hapo mwanzo serikali ndiyo iliwajengea hao watu. Wana kagera na watanzania kwa ujumla tuna jambo la kujifunza hapa.
 
Back
Top Bottom