Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Kwani kuna mwananchi wa kagera ambaye aliomba tetemeko litokee? Au kuna mwanasias yeyote aliomba tetemeko litokee ili atumie hiyo nafasi kujinufaisha/kujitangaza kisiasa? Kauli ya kwamba tetemeko halikuletwa na serikali, kwa maoni yangu sidhani kama ni sahihi sana hasa katika wakati huu ambao watanzania wenzetu wa kagera wanahitaji msaada wa hali na mali, tunaamini ya kuwa serikali haiwezi kuwaacha watu wake waendelee kuteseka kutokana na janga lililosababishwa na tetemeko la ardhi, msaada utatolewa, lakini kwa nini wapewe msaada huo na maneno ya kuudhi kama hayo?
 
Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.
Umeonaaee !! Mswahili anasingiziwa aise duuuh .mpaka nimechafukwa na roho .Mungu atusaidie
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Ndio umesahau wa njombe kuwa magufuli kareta kupatwa kwa jua [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 

Hivi Masanja unategemea nini wakati:Watu binafsi,makampuni Na nchi nyingi zimechangia kwenye hili janga la mtetemeko wa Ardhi.Mpaka Sasa karibu shilingi Bilion 5 zimekusanywa Pamoja Na saruji,mabati Na misumari.
Ina maana huu msaada unaenda wapi Kama sio Kwa waathirika.Halafu Kwa nini JWTZ lisishughulike Na ujenzi.Ngosha hana hekima kwenye hili janga.Waathiriwa wengi NI wakulima masikini.Wakafanye kazi wapi?Wengi wanataka kufarijiwa sio kubezwa Na kauli kali.
 
Endelea kufanya kampeni.
 
Wilaya ya Kyela ni mara nyingi .nyumba zao huharibiwa na mafuriko lakini huzijenga wenyewe.... hawajawai kusubiri serikali iwajengee,,,


Tuwasikitikie ndugu zetu lakini tusiwadanganye.
 
Asante sana mkuu.

Nyongeza: kuna mama mmoja wa ujerumani (Angela) pasipokujali athari za anachokifanya kisiasa,ameamua kuwapokea mamilioni ya wakimbizi toka mataifa yenye mapigano mashariki ya kati .

If only we could think why his wife was not with him during presidential campaign, MAY BE not just may be...may be people could have made a right decision
 

Mkuu mimi nakupata. Ila all I am saying, ngosha anakuwa sincere na kile ambacho kimefanyika miaka mingi. Sema wanasiasa wengine walikuwa wanatudanganya na yeye anasema ukweli. Hebu Mkuu niambie ni wapi walipata majanga...serikali ikawasaidia kujenga nyumba upya? hata hapo Msimbazi the best the government could do was to get plots for these folks in Mabwepande! Lets be real.....
Huoni kujenga shule, zahanati, barabara ni muhimu kwa community welfare kuliko hizi ideas za kujengewa nyumba? Labda serikali iwape subsidy wakinunua building materials......otherwise kujengewa..ni ndoto za mchana.
 
Waswahili bana,,, mnahusudu sana talalila,,,

Nawashauri msitangulize chuki
 

Siyo kumuombea tuu na kumpigia kura za kishindo! Welcome to the United Republic of Tanzania.
 
UNATAKA KUFANANISHA JAPAN NA TZ,AU HATA ITALY HAPO TETEMEKO LIMETOKEA JUZI TU HAPO WAMEJENGEWA.
MFUMO TULIONAO NA WA NCHI HIZO ZILIZOENDELEA NI TOFAUTI.WENZETU NYUMBA INAMILIKIWA NA SERIKALI IMEJENGWA NA SERIKALI.YEYE MMILIKI ANAHESABIKA KAMA MPANGAJI TU INGAWA ANAMILIKISHWA ASILIMIA KADHAA KWA KULIPIA KODI YA PANGO AU AKOPESHWE HELA NA BANK NDIO ALIPIE HIYO NYUMBA IWE YAKE,SASA INAPOTOKEA KUNA JANGA NYUMBA IMEDONDOKA AU KUPASUKA SERIKALI INACHUKUA JUKUMU LOTE KU REPAIR HIYO NYUMBA MPAKA IKAMILIKE.
 
Unawapa wahanga misaada huku unawasimanga! Hii inasikitisha sana, wenzetu hawakuomba wapate wapate hilo tetemeko, hawakuongea na Mungu ili awashushie gharika, hakutarajia kuishi kwao Kagera ni kujitakia balaa. Mwenye kaya hapa umenikwaza sana! Sikutarajia kauli kama hii kutoka kwa muungwana kama yeye.

Katika kipindi hiki ambacho wenzetu wanaishi kwa dhiki na hawaijui kesho itakucha vipi tunatakiwa kuchagua kauli za kiungwana kwa wenzetu walofikwa na maafa, hatutakiwi kuwasimanga kwani pia wao ni binaadamu na wana mioyo kama binaadamu wote tulivyo. Hawakupenda itokee na hawakupenda majanga ili wawe ombaomba.

Wengi wa waathirika wa tetemeko katika maisha yao hawajawahi kuwa ombaomba. Hawakutarajia kwamba wataishi katika ile kadhia, ni Mungu ndiye aliyewapangia. Kuna siku niliona mtangazaji wa BBC akionyenyesha nyumba aliyoangukiwa na jiwe kubwa. Ile nyumba imesawajika, masikini yule aliyejenga pale amekuwa hana eneo la kuishi, hana matarajio ya kutafuta pesa za kujengea sambamba na pesa ya kujikimu.

Hebu fikiri atajenga wapi makazi yake, ataishi wapi tena, atanunuaje ardhi nyingine. Kwa kweli inasikitisha huu sio wakati wa kutoa masimango, ni vyema tukajikita kuangalia namna njema ya kuwasaidia wenzetu. Na pia huu sio wakati wa kujitafutia umaarufu wala kjineemesha kubwa zaidi ni kuhakikisha kilicholetwa kinafikia walengwa kwa haraka zaidi.

Kusiwe na kasi ya konokono, au kufanya mzaha katika kufikisha misaada. Kunatakiwa kuwe na kasi nzuri ili kurejesha utu na kumfanya binaadamu wa Kagera arejee tena katika kulijenga taifa lake.Hii pia ni changamoto kwa wanaJF, yatupasa kutafuta namna ya kujihusisha na matukio kama haya. Hapa nazungumzia namna ya kuchangishana na kujitolea pindi yanapotokea majanga.

Natumai jopo la wahusika ni kipindi cha kukuna vichwa na kutafuta jawabu.
Pia kuna kale ka JF TV, hapa walitakiwa kutuhabarisha kwa kina. Vyombo vingi vya habari vilichelewa sana kutoa taarifa jadidu.
 
mbona serikali yake iliposifiwa kwa kuleta kupatwa kwa jua hakukataa?! au kwa kuwa ni ujiko?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…