Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Kwani kuna mwananchi wa kagera ambaye aliomba tetemeko litokee? Au kuna mwanasias yeyote aliomba tetemeko litokee ili atumie hiyo nafasi kujinufaisha/kujitangaza kisiasa? Kauli ya kwamba tetemeko halikuletwa na serikali, kwa maoni yangu sidhani kama ni sahihi sana hasa katika wakati huu ambao watanzania wenzetu wa kagera wanahitaji msaada wa hali na mali, tunaamini ya kuwa serikali haiwezi kuwaacha watu wake waendelee kuteseka kutokana na janga lililosababishwa na tetemeko la ardhi, msaada utatolewa, lakini kwa nini wapewe msaada huo na maneno ya kuudhi kama hayo?
 
Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.
Umeonaaee !! Mswahili anasingiziwa aise duuuh .mpaka nimechafukwa na roho .Mungu atusaidie
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Ndio umesahau wa njombe kuwa magufuli kareta kupatwa kwa jua [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Tatizo waswahili tumezoea ahadi hewa za wanasiasa. Ndo maana tunadanganywa kila siku na tunakubali. Magufuli kaamua kuwa mkweli of what is on his mind. Go figure.

Hivi kweli kwa akili yako tukufu...serikali inaweza kuwajengea nyumba wahanga wote wa hili tetemeko? Get real bro!

Hivi Masanja unategemea nini wakati:Watu binafsi,makampuni Na nchi nyingi zimechangia kwenye hili janga la mtetemeko wa Ardhi.Mpaka Sasa karibu shilingi Bilion 5 zimekusanywa Pamoja Na saruji,mabati Na misumari.
Ina maana huu msaada unaenda wapi Kama sio Kwa waathirika.Halafu Kwa nini JWTZ lisishughulike Na ujenzi.Ngosha hana hekima kwenye hili janga.Waathiriwa wengi NI wakulima masikini.Wakafanye kazi wapi?Wengi wanataka kufarijiwa sio kubezwa Na kauli kali.
 
Endelea kufanya kampeni.
 
Wilaya ya Kyela ni mara nyingi .nyumba zao huharibiwa na mafuriko lakini huzijenga wenyewe.... hawajawai kusubiri serikali iwajengee,,,

Tuwasikitikie ndugu zetu lakini tusiwadanganye.
 
Wanawake ni viumbe wa ajabu sana,naamini Mungu aliwapa wanawake moyo wa kipekee sana,moyo wa uvumilivu na upendo.Wakati jamii inashangazwa na baadhi ya mienendo ya wanaume,mienendo ya ubabe na kutojali,wanaume hao wanaoonekana wa ajabu huku mitaani hutoka katika familia zao.

Pamoja na mitazamo hasi juu ya wababe hawa,nyuma yao kuna wanawake wavumilivu,waliowapenda jinsi walivyo na waliotayari hata kuhatarisha Maisha yao kwa kuwatetea.Laiti wanadamu wote wangeumbiwa moyo wa kike,naamini dunia ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.Hongereni Mama zetu,kwani wababe wote tunaowashangaa katika dunia hii,pamoja na ubabe wao bado mnamudu kuishi nao!!Kama haya ndiyo tunayashuhudia sisi tulio nje ya nyumba,Mama aliye ndani anashuhudia na kuona mangapi?Asanteni akina mama.
Asante sana mkuu.

Nyongeza: kuna mama mmoja wa ujerumani (Angela) pasipokujali athari za anachokifanya kisiasa,ameamua kuwapokea mamilioni ya wakimbizi toka mataifa yenye mapigano mashariki ya kati .

If only we could think why his wife was not with him during presidential campaign, MAY BE not just may be...may be people could have made a right decision
 
Hivi Masanja unategemea nini wakati:Watu binafsi,makampuni Na nchi nyingi zimechangia kwenye hili janga la mtetemeko wa Ardhi.Mpaka Sasa karibu shilingi Bilion 5 zimekusanywa Pamoja Na saruji,mabati Na misumari.
Ina maana huu msaada unaenda wapi Kama sio Kwa waathirika.Halafu Kwa nini JWTZ lisishughulike Na ujenzi.Ngosha hana hekima kwenye hili janga.Waathiriwa wengi NI wakulima masikini.Wakafanye kazi wapi?Wengi wanataka kufarijiwa sio kubezwa Na kauli kali.

Mkuu mimi nakupata. Ila all I am saying, ngosha anakuwa sincere na kile ambacho kimefanyika miaka mingi. Sema wanasiasa wengine walikuwa wanatudanganya na yeye anasema ukweli. Hebu Mkuu niambie ni wapi walipata majanga...serikali ikawasaidia kujenga nyumba upya? hata hapo Msimbazi the best the government could do was to get plots for these folks in Mabwepande! Lets be real.....
Huoni kujenga shule, zahanati, barabara ni muhimu kwa community welfare kuliko hizi ideas za kujengewa nyumba? Labda serikali iwape subsidy wakinunua building materials......otherwise kujengewa..ni ndoto za mchana.
 
Hivi Masanja unategemea nini wakati:Watu binafsi,makampuni Na nchi nyingi zimechangia kwenye hili janga la mtetemeko wa Ardhi.Mpaka Sasa karibu shilingi Bilion 5 zimekusanywa Pamoja Na saruji,mabati Na misumari.
Ina maana huu msaada unaenda wapi Kama sio Kwa waathirika.Halafu Kwa nini JWTZ lisishughulike Na ujenzi.Ngosha hana hekima kwenye hili janga.Waathiriwa wengi NI wakulima masikini.Wakafanye kazi wapi?Wengi wanataka kufarijiwa sio kubezwa Na kauli kali.
Waswahili bana,,, mnahusudu sana talalila,,,

Nawashauri msitangulize chuki
 
Hivi wewe aliyekwambia anataka kujengewa nyumba ni nani? Tangu nchi hii iumbwe ni serikali ipi iliwahi kuwajengea wananchi nyumba waliopatwa na majanga kama haya? Watu wanacho complain ni kauli zisizo na faraja zilizotolewa na mkuu wa nchi.hata kama wakiamuwa wasitoe chochote huwezi kuwambia wananchi msitegemee serikali fanyeni kazi kana kwamba wao hawafanyagi kazi au wamekaa tu kusubiri serikali. Haina shida ndugu zao wapo na watakaoguswa watawasaidia nakuwafariji. Sikutegemea kama rais angeweza kuongea kauli zile achilia mbali kwenda kuwatembelea wahanga wa tetemeko. Wana kagera hawana hiyana wataendelea kumuombea huku wakitambuwa sura siyo roho.

Siyo kumuombea tuu na kumpigia kura za kishindo! Welcome to the United Republic of Tanzania.
 
Mm majanga ni matukio ya asili yanapotokea huja bila taarifa .tujenge uzalendo wa kusaidiana pale inapobidi kule japan niliona rule mji wa Kumamoto ulipatwa Na tetemeko .serikali imeshajenga Nyumba Na tayar wale wahanga wamehamia .bila kuathiri masharti maisha yaendelee.
UNATAKA KUFANANISHA JAPAN NA TZ,AU HATA ITALY HAPO TETEMEKO LIMETOKEA JUZI TU HAPO WAMEJENGEWA.
MFUMO TULIONAO NA WA NCHI HIZO ZILIZOENDELEA NI TOFAUTI.WENZETU NYUMBA INAMILIKIWA NA SERIKALI IMEJENGWA NA SERIKALI.YEYE MMILIKI ANAHESABIKA KAMA MPANGAJI TU INGAWA ANAMILIKISHWA ASILIMIA KADHAA KWA KULIPIA KODI YA PANGO AU AKOPESHWE HELA NA BANK NDIO ALIPIE HIYO NYUMBA IWE YAKE,SASA INAPOTOKEA KUNA JANGA NYUMBA IMEDONDOKA AU KUPASUKA SERIKALI INACHUKUA JUKUMU LOTE KU REPAIR HIYO NYUMBA MPAKA IKAMILIKE.
 
Unawapa wahanga misaada huku unawasimanga! Hii inasikitisha sana, wenzetu hawakuomba wapate wapate hilo tetemeko, hawakuongea na Mungu ili awashushie gharika, hakutarajia kuishi kwao Kagera ni kujitakia balaa. Mwenye kaya hapa umenikwaza sana! Sikutarajia kauli kama hii kutoka kwa muungwana kama yeye.

Katika kipindi hiki ambacho wenzetu wanaishi kwa dhiki na hawaijui kesho itakucha vipi tunatakiwa kuchagua kauli za kiungwana kwa wenzetu walofikwa na maafa, hatutakiwi kuwasimanga kwani pia wao ni binaadamu na wana mioyo kama binaadamu wote tulivyo. Hawakupenda itokee na hawakupenda majanga ili wawe ombaomba.

Wengi wa waathirika wa tetemeko katika maisha yao hawajawahi kuwa ombaomba. Hawakutarajia kwamba wataishi katika ile kadhia, ni Mungu ndiye aliyewapangia. Kuna siku niliona mtangazaji wa BBC akionyenyesha nyumba aliyoangukiwa na jiwe kubwa. Ile nyumba imesawajika, masikini yule aliyejenga pale amekuwa hana eneo la kuishi, hana matarajio ya kutafuta pesa za kujengea sambamba na pesa ya kujikimu.

Hebu fikiri atajenga wapi makazi yake, ataishi wapi tena, atanunuaje ardhi nyingine. Kwa kweli inasikitisha huu sio wakati wa kutoa masimango, ni vyema tukajikita kuangalia namna njema ya kuwasaidia wenzetu. Na pia huu sio wakati wa kujitafutia umaarufu wala kjineemesha kubwa zaidi ni kuhakikisha kilicholetwa kinafikia walengwa kwa haraka zaidi.

Kusiwe na kasi ya konokono, au kufanya mzaha katika kufikisha misaada. Kunatakiwa kuwe na kasi nzuri ili kurejesha utu na kumfanya binaadamu wa Kagera arejee tena katika kulijenga taifa lake.Hii pia ni changamoto kwa wanaJF, yatupasa kutafuta namna ya kujihusisha na matukio kama haya. Hapa nazungumzia namna ya kuchangishana na kujitolea pindi yanapotokea majanga.

Natumai jopo la wahusika ni kipindi cha kukuna vichwa na kutafuta jawabu.
Pia kuna kale ka JF TV, hapa walitakiwa kutuhabarisha kwa kina. Vyombo vingi vya habari vilichelewa sana kutoa taarifa jadidu.
 
mbona serikali yake iliposifiwa kwa kuleta kupatwa kwa jua hakukataa?! au kwa kuwa ni ujiko?!
 
Back
Top Bottom