Kwani kuna mwananchi wa kagera ambaye aliomba tetemeko litokee? Au kuna mwanasias yeyote aliomba tetemeko litokee ili atumie hiyo nafasi kujinufaisha/kujitangaza kisiasa? Kauli ya kwamba tetemeko halikuletwa na serikali, kwa maoni yangu sidhani kama ni sahihi sana hasa katika wakati huu ambao watanzania wenzetu wa kagera wanahitaji msaada wa hali na mali, tunaamini ya kuwa serikali haiwezi kuwaacha watu wake waendelee kuteseka kutokana na janga lililosababishwa na tetemeko la ardhi, msaada utatolewa, lakini kwa nini wapewe msaada huo na maneno ya kuudhi kama hayo?