Rais Magufuli timiza ahadi yako ya kumpatia ajira Joshua Nassari

Rais Magufuli timiza ahadi yako ya kumpatia ajira Joshua Nassari

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,490
Reaction score
38,302
Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli wakati wa kipindi cha kampeni ulitoa ahadi ya kumpatia kazi kijana wetu mpendwa Joshua Nassari.

Muda unakwenda kasi sana tangu kampeni zimalizike na wewe kuibuka na ushindi wa kishindo.Kijana wetu wetu ana mtoto ambae anahitaji matunzo ya kiwango cha nafasi za juu za kiserekali kama Regional Commissioner au High Commissioner au Mkuu wa shirika lolote zuri la umma kama NSSF, PSPF, TANAPA, NCAA, CRDB, KADCO, TANESCO, TANROAD, UWASSA,TBC, na NK.

Kijana wetu Nassari alishiriki kikamilifu kampeni hadi ukapata ushindi wa kishindo,hata kama yule jamaa wa ubelgiji anasema kulikuwa na kosoro nyingi lakini wewe sasa ni Rais wa JMT.Kwa nafasi yako una nafasi kibao kuanzia serekali kuu,serekali za mitaa,mawizara kibao,nafasi za ubunge 10 jimbo la Ikulu.Najua una shughuli nyingi kiasi unaweza kusahau ebu tupia jicho kama ikishindikana basi mpatie nafasi ya RAS kijana asiteseke na kusahaulika.

Wasalamu Ngongo safarini Chato National Park.
 
Nassari ameapa kuwa kama hadi March mosi hajapewa kazi atahama nchi na akifika mbele ndiyo ataiumbua CCM na ataeleza yote yaliyo nyuma ya pazia kuanzia biashara ya kununua wabunge wa upinzani hadi hawa covid 19, na kwa jinsi anavyozungumza kwa hisia kali atafanya kweli.
 
Hivi bado kuna watu mnapangia dikteta cha kufanya.?
Dogo alishafyekwa mkia anashindwa hata kuchutama, dhambi ya 'usnitch' kwa wana Meru na Chadema inamtafuna boya huyo.

Afe na njaa.
Kama vile mwamba wa ufipa utampangia nani awemwenyekiti, nawakati yeye ndiye Alfa na omega??
 
bilashaka wee ndo Joshua Nassar, Kijana chapa kazi uchaguzi umepita.
 
Mh.Rais sidhani kama yupo tayari kutishwa eti huyo Nassari atatoboa siri na ieleweke hapangiwi cha kufanya...atakalolifanya analijuwa mwenyeweg.
Nassary dont try to fool nambari one and the citizens at large
 
Tukumbuke Kijana wetu aliunga mkono juhudi bila kile chama cha sera ya uhuru haki na maendelea kugundua.Isitoshe Silinde aliunga mkono juhudi siku za karibuni lakini kazawadiwa uNaibu Waziri huwezi kumlinganisha na Nassari aliunga mkono juhudi kisayansi zaidi.
 
Kwani lazima apewe teuzi ya umma?

Kama anagangania teuzi ni wazi ni mweupe kichwani.

Pia ni blackmail.
 
Back
Top Bottom