Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kudhalilisha mamlaka ya uteuzi ni kosa kubwa sana.
Unakuwa na mkuu wa wilaya ambae anajua fika anamamlaka kisheria ya kukamata mtu akifanya kosa ndani ya wilaya yake. Sheria inatamka wazi anatakiwa akikamata mtu amfikishe polisi kisha mahakamani na sheria ifuate mkondo.
Anakamata watu wanaotumia walemavu kama kitega uchumi,wanawachalaza bakora akiwa na waziri mdogo kama vile hawajui ibara ya 13 ya katiba ya JMT inasemaje juu ya usawa mbele ya sheria.
Mbali ya hayo vipi kuhusu haki ya kusikilizwa mtuhumiwa? Vipi kuhusu mamlaka ya kutoa adhabu?
Nini ambacho kinaendelea hapa Tanzania? Wateule wa rais ambao hawajui sheria za nchi? Mbona akina L Mrema walikamata bunduki,wakwepa kodi na wala rushwa hatukuona watu wakichapwa bakora?
Mkuu wa kaya safisha hawa wanaoharibu taswira ya utawala wako.