Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Alipoingia madarakani aliingia kwa kasi na mbwembwe za kutaka kubana matumizi.
Akawakoromea wabunge kuhusu pesa za tafrija zao huko Dodoma, akaamuru kusiwepo na sherehe/ shamrashamra za sikukuu ya muungano, na kadhalika.
Baadhi yetu tukayaafiki hayo maamuzi. Tukaona ni mwanzo mzuri maana mabilioni ya pesa yalikuwa yakitumika kiholela tu kwa sherehe za masaa machache wakati kuna mambo mengine yaliyo ya muhimu ambapo hayo mabilioni yangeweza kutumika.
Baadaye kidogo akaja na hizi habari za serikali kuhamia Dodoma.
Sikuelewa! Nikajikuna kichwa.
Nikajiukiza, kama kweli mtu anayechukia mambo ya kutumia hovyo pesa za walipa kodi, inawezekanaje mtu huyo huyo ndo akawa mstari wa mbele katika kutaka kufanikisha jambo ambalo litagharimu mabilioni [kama siyo matrilioni] ya pesa za walipa kodi?
Nikajaribu kutafuta sababu iliyo ya lazima kuendelea na huo mpango wa kuifanya Dodoma ndo iwe mji mkuu, nikakosa!
Wazo lililokuwa na maana miaka ya 70 huko leo hii si lazima liwe na maana tena.
Leo hii sioni sababu ya kuingia migharama mikubwa kuhamisha makao makuu ya nchi.
Hapo ndipo napoona Rais Magufuli hayupo consistent kivile katika maamuzi mazuri ya matumizi ya pesa za walipa kodi.
Anabana matumizi huku lakini anaenda anatumia vibaya kule.
Mwisho wa siku inakuwa ni kazi bure tu! Inakuwa hujabana chochote!!
Ndo kujichanganya kwenyewe huko.
Heri ya 2019.
Wenu daima,
Nyani Ngabu au ukipenda, niite NN.