Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Kwani Watanzania wanaendaga Dar tu?

Serikali ingepaswa kuwa na ofisi zake muhimu kwenye kanda, kama hawana mpaka hivi sasa.

Hiyo ni bonge la option.

Mtu wa Simiyu akitaka huduma flani flani basi anaenda Mwanza.

Wa Iringa akitaka huduma flani kama Iringa haipo basi anaenda Mbeya.

Lakini siyo kuhamisha serikali nzima iende Dodoma..
Wazo zuri ila ndio hivyo kama una tatizo Wizara labda ya maji lazima usafiri mpaka Dodoma ukaonane na maafisa wa wizara husika
 
Mwisho wa siku huoni tatizo lolote,

- Kurudiwa kwa chaguzi za kijinga kuwahi kutokea nchini,

- Tundu Lissu kupigwa risasi 38 bila hatia yoyote na kunyimwa haki zake.

- Mtu mmoja kuamua kununua ndege kwa gharama kubwa mara mbili ya bei halisi wala huoni tatizo.

- Mtu kuhubiri chukiii na migawanyiko huku akiwa-brand watu wengine uovu wala huoni tatizo.

Unachokifanya ni kuokoteza masuala machache kujaribu kudanganya watu kuwa uko neutral. Kumbe wala huoni tatizo lolote ..
Huyu Nyani Ngabu ni msukuma mwenzake hawezi kuona hilo
 
Ulikuwa ni mpango wa enzi hizo.

Miaka karibu 50 imepita.

Nchi ina changamoto nyingi mno kuliko wakati ule.

Kipaumbele sasa hivi kinapaswa kuwa ni kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa miaka yote hiyo nchi imeenda vizuri tu.

Mji mkuu uendelee kuwa Dar.
Sawa, ila pia changamoto zinaendelea kutatuliwa pia, miradi ya maji inaendelea, barabara zinajengwa, madaraja yanajengwa pia, madarasa yanaendelea kujengwa so mdogomdogo ndio mwendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho wa siku huoni tatizo lolote,

- Kurudiwa kwa chaguzi za kijinga kuwahi kutokea nchini,

- Tundu Lissu kupigwa risasi 38 bila hatia yoyote na kunyimwa haki zake.

- Mtu mmoja kuamua kununua ndege kwa gharama kubwa mara mbili ya bei halisi wala huoni tatizo.

- Mtu kuhubiri chukiii na migawanyiko huku akiwa-brand watu wengine uovu wala huoni tatizo.

Unachokifanya ni kuokoteza masuala machache kujaribu kudanganya watu kuwa uko neutral. Kumbe wala huoni tatizo lolote ..

Nani kasema sioni tatizo kuwa Lissu alijaribiwa kutolewa uhai wake? Nimeandika mada nyingi tu hapa nikiikosoa serikali juu ya uchunguzi wa huo uhalifu. FACT.

Nimemchana Magufuli hapa alipoendaga Mwanza na kusema wasivunjiwe nyumba zao huko kwa vile walimpa kura. FACT.

Nimemchana Magufuli hapa na kuombea ashindwe katika azma yake ya kutaka kuviminya vyombo vya habari. FACT.

Nimemchana Magufuli kwa kumpendelea Makonda. FACT.

Nimemchana Magufuli kwa mengi tu humu. FACT.

What rock has your ass been under?
 
Kitendo cha serikali kuhamia Dodoma manake miundombinu Kama barabara, majengo, maji umeme kuhimarika. Lakini vilevile miji ya jirani kukua kwa kasi kiuchumi.

Hili jambo liko wazi ndio maana unaona kukiwa na ujenzi wa makao makuu mapya ya wilaya au mkoa kunakuwa na ugomvi sana pajengwe wapi! Sababu ya wazi ni ile establishment tu ya ofisi inaleta sana maendeleo.

Sembuse makao makuu ya nchi? Au unataka iendelee kujengwa Dsm ambako kwa standard za kitanzania tunaona imeshajengwa sana ukilinganisha na sehemu nyingine. Na tumeshasoma malalamiko mengi humu humu jukwaani kwamba DSM inapendelewa na watu wanataka even distribution of growth.

Sababu za toka kipindi cha Nyerere bado ni valid. Lengo ilikuwa makao makuu iwe kati kati ya nchi ili krahisishwa maendeleo kwa maana ya mawasiliano, umbali mfupi kufika sehemu nyingine za Tanzania.

Najua kuna wengine watasema sababu ya kukua kwa sayansi na teknolojia hoja ya umbali haina umuhimu. Lakini ukweli wa wazi ambao tunahushuhudia mpaka leo njia za usafiri kuingia tu Dsm zilizidiwa. Over concentration ya magari na watu kuingia Dsm ilisababisha mji na infrastructures kuzidiwa sana na kusababisha gharama kubwa katika yote hayo. Kurekebisha miundo mbinu kumekuwa na gharama kubwa sana rejea tu upanuzi wa Morogoro road, gharama upande wa serikali kujenga barabara na gharama za wananchi kubomolewa nyumba zake.

Kwa lugha nyingine kasi ya ukuaji wa DSM Kama makao makuu hauendani kabisa na uwezo wa serikali na wananchi kurekebisha na kuundwa miundombinu(au miundo msingi, wataaalam wa lugha mtarekebisha). Tuwe wakweli Dsm ilikuwa tayari bomu linalosubiri kupasuka ikitokea mafuriko makubwa, tetemeko la ardhi, mlipuko mkubwa wa moto n.k

Kwa hiyo ukizungumzia gharama ya kujenga Dodoma linganisha na gharama ya kuirekebisha Dsm kwa kasi inayoendana na kasi ya ukuaji mji kama itaendelea kuwa makao makuu ya serikali.

Kwangu Mimi naona gharama ya Dsm ni kubwa zaidi. Lakini la pili kama nilivyosema bado tuna wajibu wa kuikuza Dodoma na Tanzania nzima. Ili linafanyika vizuri zaidi Kama Dodoma inakuwa Capital city. Kumbuka Dodoma imepangwa(planned) kwa asilimia kubwa, mji una barabara nyingi zilizojengwa kwa njia zote hivyo kutanuka kiurahisi bila kusahau kusimamia misingi ya mipango miji.
 
Wengine wanaweza kusema anaitaka ile sifa ya kuitwa rais aliyehamisha mji mkuu wa Tanzania.
Nyani Ngabu pamoja na hili la Dodoma pia kuna ile ya kuunga juhudi za Rais a k a kununua wapinzani na madege pia . Hivi havikutakiwa kuwa kipaumbele kwa nchi masikini kama hii !!.

Lakini haya yote yanafanyika kwa sababu maalum . Katiba ya nchi imemfanya Rais kuwa mungumutu anayefanya chochote na hakuna wa kuhoji.
Hii si kwa Maghufuli tu lah hasha. Ni kwa waliomtangulia na watakaomfuatia. Jibu ni moja KATIBA si nzuri.

Hebu imagine mtu kama Trump angetawala kwa katiba kama hii ya Tz . Inayo create miunguwatu. America na dunia ingekuwa Je ??!!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajenga daraja jipya la salendar kuelekea wanapokaa mabalozi halafu wakati huo huo unawapa hati mabalozi hao ili wakajenge ofisi zao mpya Dodoma!.

Nawaonea huruma watu wanaowekeza kwenye majengo mapya ya kupangisha, walifanya hivyo bila ya kutegemea hii hatua ya kuhamia Dodoma.

Unaliona jengo zuri pembeni ya Bagamoyo Road, lakini limepangishwa ile sehemu ya chini tu, ghorofa ya kwanza kwenda juu vioo vinajaa mavumbi kila kukicha.
 
Nyani Ngabu pamoja na hili la Dodoma pia kuna ile ya kuunga juhudi za Rais a k a kununua wapinzani na madege pia . Hivi havikutakiwa kuwa kipaumbele kwa nchi masikini kama hii !!.

Lakini haya yote yanafanyika kwa sababu maalum . Katiba ya nchi imemfanya Rais kuwa mungumutu anayefanya chochote na hakuna wa kuhoji.
Hii si kwa Maghufuli tu lah hasha. Ni kwa waliomtangulia na watakaomfuatia. Jibu ni moja KATIBA si nzuri.

Hebu imagine mtu kama Trump angetawala kwa katiba kama hii ya Tz . Inayo create miunguwatu. America na dunia ingekuwa Je ??!!.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiyo ya ndege nayo nimeshaikosoa humu.

FACT.
 
Back
Top Bottom