Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Rais Magufuli; ubanaji matumizi; na kujichanganya [contradict]

Alipoingia madarakani aliingia kwa kasi na mbwembwe za kutaka kubana matumizi.

Akawakoromea wabunge kuhusu pesa za tafrija zao huko Dodoma, akaamuru kusiwepo na sherehe/ shamrashamra za sikukuu ya muungano, na kadhalika.

Baadhi yetu tukayaafiki hayo maamuzi. Tukaona ni mwanzo mzuri maana mabilioni ya pesa yalikuwa yakitumika kiholela tu kwa sherehe za masaa machache wakati kuna mambo mengine yaliyo ya muhimu ambapo hayo mabilioni yangeweza kutumika.

Baadaye kidogo akaja na hizi habari za serikali kuhamia Dodoma.

Sikuelewa! Nikajikuna kichwa.

Nikajiukiza, kama kweli mtu anayechukia mambo ya kutumia hovyo pesa za walipa kodi, inawezekanaje mtu huyo huyo ndo akawa mstari wa mbele katika kutaka kufanikisha jambo ambalo litagharimu mabilioni [kama siyo matrilioni] ya pesa za walipa kodi?

Nikajaribu kutafuta sababu iliyo ya lazima kuendelea na huo mpango wa kuifanya Dodoma ndo iwe mji mkuu, nikakosa!

Wazo lililokuwa na maana miaka ya 70 huko leo hii si lazima liwe na maana tena.

Leo hii sioni sababu ya kuingia migharama mikubwa kuhamisha makao makuu ya nchi.

Hapo ndipo napoona Rais Magufuli hayupo consistent kivile katika maamuzi mazuri ya matumizi ya pesa za walipa kodi.

Anabana matumizi huku lakini anaenda anatumia vibaya kule.

Mwisho wa siku inakuwa ni kazi bure tu! Inakuwa hujabana chochote!!

Ndo kujichanganya kwenyewe huko.

Heri ya 2019.

Wenu daima,

Nyani Ngabu au ukipenda, niite NN.
Ila mkuu unadhani ni matumizi mabaya kupeleka makao makuu dodoma, kama kitu kinafanyika kwa nchi ya tanzania si ndo kazi ya fedha ya mlipa kodi hiyo, asipofanya sahivi atafanya nani, ulikuwa ni mpango uliotakiwa kufanyika miaka ya zamani sana, ndo anafanya sahv, fair enough, labda uniambie matumizi mabaya yasiyo na manufaa kwa nchi ndo nikuelewe,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewahi kutembelea makao makuu tokea mikoani mfano Arusha ukilinganisha adha za safari kwenda Dodoma na kwenda Dar es Salaam ukaona tofauti yake?

Acha pesa zitumike tuu zinaingia kwene uchumi kupitia wakandarasi, wazalishaji na wauzaji wa vifaa vya ujenzi

Kutembelea kwa minajili ipi?
 
Alipoingia madarakani aliingia kwa kasi na mbwembwe za kutaka kubana matumizi.

Akawakoromea wabunge kuhusu pesa za tafrija zao huko Dodoma, akaamuru kusiwepo na sherehe/ shamrashamra za sikukuu ya muungano, na kadhalika.

Baadhi yetu tukayaafiki hayo maamuzi. Tukaona ni mwanzo mzuri maana mabilioni ya pesa yalikuwa yakitumika kiholela tu kwa sherehe za masaa machache wakati kuna mambo mengine yaliyo ya muhimu ambapo hayo mabilioni yangeweza kutumika.

Baadaye kidogo akaja na hizi habari za serikali kuhamia Dodoma.

Sikuelewa! Nikajikuna kichwa.

Nikajiukiza, kama kweli mtu anayechukia mambo ya kutumia hovyo pesa za walipa kodi, inawezekanaje mtu huyo huyo ndo akawa mstari wa mbele katika kutaka kufanikisha jambo ambalo litagharimu mabilioni [kama siyo matrilioni] ya pesa za walipa kodi?

Nikajaribu kutafuta sababu iliyo ya lazima kuendelea na huo mpango wa kuifanya Dodoma ndo iwe mji mkuu, nikakosa!

Wazo lililokuwa na maana miaka ya 70 huko leo hii si lazima liwe na maana tena.

Leo hii sioni sababu ya kuingia migharama mikubwa kuhamisha makao makuu ya nchi.

Hapo ndipo napoona Rais Magufuli hayupo consistent kivile katika maamuzi mazuri ya matumizi ya pesa za walipa kodi.

Anabana matumizi huku lakini anaenda anatumia vibaya kule.

Mwisho wa siku inakuwa ni kazi bure tu! Inakuwa hujabana chochote!!

Ndo kujichanganya kwenyewe huko.

Heri ya 2019.

Wenu daima,

Nyani Ngabu au ukipenda, niite NN.
Cha kushangaza kuhamia Dodoma ni moja ya mambo machache nampongeza. Nchi haiwezi kutegemea mji mmoja tu. Dar ni kero bora watu tugawane maendeleo na maeneo ya kuishi.
 
Ila mkuu unadhani ni matumizi mabaya kupeleka makao makuu dodoma, kama kitu kinafanyika kwa nchi ya tanzania si ndo kazi ya fedha ya mlipa kodi hiyo, asipofanya sahivi atafanya nani, ulikuwa ni mpango uliotakiwa kufanyika miaka ya zamani sana, ndo anafanya sahv, fair enough, labda uniambie matumizi mabaya yasiyo na manufaa kwa nchi ndo nikuelewe,

Sent using Jamii Forums mobile app

Mpango ulikuwa wa zamani.

Miaka karibu 50 imepita.

Hakuna tena sababu ya msingi ya kuhamia huko.
 
Mpango ulikuwa wa zamani.

Miaka karibu 50 imepita.

Hakuna tena sababu ya msingi ya kuhamia huko.
Tatizo tunajaribu kutafuta kila kitu kinachotufaa sisi binafsi ndo tuone cha maana, bunge kuwa dodoma kila mtu anakubali, historia ya nchi yetu inasema mji mkuu wa tanzania ni dodoma, nyerere alivision makao makuu ya nchi, hadi ikulu iwe dodoma tatizo alilolikumba yeye kipindi hicho nchi changa akafanikiwa kukuta bunge lipo dodoma akaishia hapo, waliofata hawakutaka kufuatilia hilo swala wakala bata zao wakamaliza majukumu yao fresh, sasa kaja huyu kaona mi nataka nimalize hili swala kabisa, sasa kila mtu anaona oooh huu ni upuuzi, how come wakati ilikua ndo moja ya plan ya nchi, kwangu mi naon kwakuwa ni mpango wa kuinufaisha nchi na dodoma ikiwa imejengwa itanufaisha tanzania nzima wala sioni matumizi mabaya yapo wapi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Serikali inatumia mabilioni bila sababu.
Kujenga ofisi za wizara na idara Dodoma wakati Dar es salaam kuna ofisi ,kwa nchi masikini hatukutakiwa kufanya hivyo.
Kufanya chaguzi ndogo za madiwani na wabunge bila sababu,Nina amini kabisa hakukuwa sababu za uchaguzi kama maendeleo hayana chama hakukuwa sababu ya kuwahonga wabunge na madiwani wa upinzani ili wahamie CCM.
Wakati yeye anamnanga Kikwete kwamba hela nyingi zilipotea kwa wapiga dili awamu ya nne,rais wa awamu ya sita atamnanga yeye kuwa hela nyingi zilipotea kwa kufanya chaguzi za hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewahi kujiuliza kwa miaka zaidi ya 30 tumetumia shs ngapi kwa ajili ya allowance ya watumishi wa umma waliokuwa wanaenda Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge?
 
Kusafiri kwenda Dodoma toka mikoani ni rahisi kuliko kutoka Mikoani kwenda Dar es Salaam

Kwani Watanzania wanaendaga Dar tu?

Serikali ingepaswa kuwa na ofisi zake muhimu kwenye kanda, kama hawana mpaka hivi sasa.

Hiyo ni bonge la option.

Mtu wa Simiyu akitaka huduma flani flani basi anaenda Mwanza.

Wa Iringa akitaka huduma flani kama Iringa haipo basi anaenda Mbeya.

Lakini siyo kuhamisha serikali nzima iende Dodoma..
 
Kazi kweli kweli... Dodoma imekua kero na catalyst ya kuvunja ndoa na chachu ya mifarakano ya familia, Wanataka wenzao waende Dodoma huku wao wako mjini kila siku na familia zao huku wenzao wakiwa wanaishi maisha ya big brother na kulala bar!

Ukiona maVX V8 ya viongozi waandamizi yanavyojiachia Dar unajiuliza sijui nani kaenda dodoma!
 
Mwisho wa siku huoni tatizo lolote,

- Kurudiwa kwa chaguzi za kijinga kuwahi kutokea nchini,

- Tundu Lissu kupigwa risasi 38 bila hatia yoyote na kunyimwa haki zake.

- Mtu mmoja kuamua kununua ndege kwa gharama kubwa mara mbili ya bei halisi wala huoni tatizo.

- Mtu kuhubiri chukiii na migawanyiko huku akiwa-brand watu wengine uovu wala huoni tatizo.

Unachokifanya ni kuokoteza masuala machache kujaribu kudanganya watu kuwa uko neutral. Kumbe wala huoni tatizo lolote ..
 
Mwenyewe na wengine wanasema tunaweza tusimuelewe sasahivi,kwamba tutamuelewa baadae.lkn kiukweli ukiacha hizo gharama za kuhamia dodoma kuna miundombinu iliyokuwa ikitumika hapa mjini imebaki magofu na baada ya miaka michache itakuwa haifai kwa matumizi,pili uwekezaji wa miundombinu hasa ya nyumba za makazi na ofisi imebaki kuwa hasara kwa wawekezaji na kwakweli sijui nini kifanyike kuokoa hiyo hali.
Hivi rais alishahamia Dodoma? Aliahidi kuhamia kabla ya Desemba 2018.
 
Tatizo tunajaribu kutafuta kila kitu kinachotufaa sisi binafsi ndo tuone cha maana, bunge kuwa dodoma kila mtu anakubali, historia ya nchi yetu inasema mji mkuu wa tanzania ni dodoma, nyerere alivision makao makuu ya nchi, hadi ikulu iwe dodoma tatizo alilolikumba yeye kipindi hicho nchi changa akafanikiwa kukuta bunge lipo dodoma akaishia hapo, waliofata hawakutaka kufuatilia hilo swala wakala bata zao wakamaliza majukumu yao fresh, sasa kaja huyu kaona mi nataka nimalize hili swala kabisa, sasa kila mtu anaona oooh huu ni upuuzi, how come wakati ilikua ndo moja ya plan ya nchi, kwangu mi naon kwakuwa ni mpango wa kuinufaisha nchi na dodoma ikiwa imejengwa itanufaisha tanzania nzima wala sioni matumizi mabaya yapo wapi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulikuwa ni mpango wa enzi hizo.

Miaka karibu 50 imepita.

Nchi ina changamoto nyingi mno kuliko wakati ule.

Kipaumbele sasa hivi kinapaswa kuwa ni kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa miaka yote hiyo nchi imeenda vizuri tu.

Mji mkuu uendelee kuwa Dar.
 
Back
Top Bottom