Hapo nyani umeongea haswa. Nianze na hili la "kufuta sherehe" kama za Muungano, na HATA SHEREHE ZA UHURU NA JAMHURI!!! Kuna mtu aliwahi kuhoji hata kile kitendo cha kuhamishia sherehe hizo DODOMA. hoja yake ilikuwa kwamba sherehe hizo zina historia yake, kwamba sherehe orijino ilifanyika "uwanja wa uhuru" na hiyo ni alama isiyohamishika. hivyo tunapofanya hapo sherehe hizo ina maana kubwa sana. Kwa Magufuli, mtu wa makalveti, madaraja na barabara, "such niceties" have no place, I suppose.
Sasa Magufuli hakuishia tu kuhamisha, lakini KUFUTA. Mwanzo alifuta ili KUFANYA USAFI. shida hapo ni kwamba usafi ni tabia inayoweza kujengwa, na iwe jambo la kawaida la kila siku. lakini kumbukumbu za UHURU WA NCHI ni kitu kingine kabisa. Angeweza KUBORESHA lakini siyo kufuta. Sasa nije kwenye hoja yako. Kafuta sherehe hizo muhimu, MUUNGANO, UHURU NA JAMHURI, lakini hebu angalia hizo "sherehe" za kupokea ndege, kwa mfano. ni kubwa kuliko ambavyo ingebidi iwe. ingetosha mara moja tu, nyingine ikawa ni zoezi la kawaida linalofanywa na wahusika. Nadhani ana lengo mahususi:
Kuhamia Dodoma ni hatua ya kuonesha kwamba NYERERE of all people alishindwa kwenda Dodoma, yeye kaweza. Sherehe za UHURU NA JAMHURI ni kusherehekea mafanikio ya Watanganyika wakiongozwa na Nyerere. sasa yeye hataki hiyo. anataka ATUKUZWE YEYE. so what about kuongoza shughuli za usafi? na yeye anapigwa picha? Hayo ni mafanikio yake yeye binafsi. Kupokea ndege? Hayo ni mafanikio ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Joseph Pombe Magufuli!! Tatizo ni EGO.
Lakini kama ambavyo wengine wamesema, hata Nyerere mwenyewe asingefurahia kuhamia Dodoma Leo hii. 1973 ilikuwa enzi za ANALOJIA. LEO NI DIGITALIA. Leo kuna dude linaitwa E-GOVERNMENT. Leo tunasema DUNIA NI KIJIJI. sasa maana gani kuhamia Dodoma? hata mambo ya security sasa ni tofauti kabisa na enzi hizo. Ni matumizi mabovu ya rasilimali za nchi, ili kuridhisha EGOTISTICAL ambitions za mtu mmoja