Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, ukishindwa uchaguzi uko tayari kukabidhi Ikulu?

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, ukishindwa uchaguzi uko tayari kukabidhi Ikulu?

JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea
Asishindwe yeye amekuwa Mungu? Mbona Kabuye alimshinda ubunge tena mara mbili
 
Rais Magufuli kama mgombea wa Chama tawala, anatakiwa kutoa tamko la kukubali matokeo kwa namna yoyote yatakavyokuwa. Itakuwa jambo la hekima kujitokeza hadharani na kuonesha msimamo wake.

Mpinzani wake mkuu, Lissu, ameshasema kuwa akishinda au kushindwa kwa haki, yupo tayari kukubali matokeo.

Wote hawa wanaamini watashinda, lakini je Magufuli ukishindwa utakubali?

TUNAOMBA MSIMAMO WAKO KWA HILI
Sidhani[emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Usijali kiongozi, kuanzia tarehe 02 hapo tutaanza kutafutana ila msizime simu tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahahaha Haina shida bwashe ......uchaguzi siyo ugomvi. Maisha lazima yaendelee kama jamii. Kwa kuwa mtashindwa mkubali ili tuendelee kuishi kama jamii moja!
 
Mara zote huwa napenda kuwakumbusha wakati wa uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

CCM ilihamasisha sana watu wake tofauti na nyie mlikuwa mnawaambia wagomee, tena wengine walikuwa wanapost picha mitandaoni kwa furaha kabisa kwamba vituoni hakuna watu na hilo ndio litawagharimu, msitegemee kupata ushindi eti kutoka kwa wana CCM wanaomchukia JPM
Hilo la picha kushangilia vituo tupu vya kujiandikisha nalikumbuka sana.
 
Hilo la picha kushangilia vituo tupu vya kujiandikisha nalikumbuka sana.
Sasa kama watu walishangilia vituo kukosa watu wa kujiandikisha ina maana kwamba wao hawakujiandikisha wala kurekebisha taarifa zao, kigezo kikubwa cha kukufanya upige kura ni taarifa zako kusomeka kwenye hilo daftari.........hesabu ni nyepesi sana ila watu wanajitoa ufahamu tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huko mbele tukishastaarabika tutakapoamua kufumua mifumo yetu ya uchaguzi tukumbuke kuongeza vitu viwili.

1. Kutakuwa na mdahalo isiyopungua miwili katika ngazi ya Urais itakayoratibiwa na tume kwa kushirikiana na vyombo vya habari na taasisi za kiraia.

2. Wagombea wote wa Urais watalazimika kila mmoja wao kutoa video siku tano kabla ya uchaguzi wakisoma statement ya Tume ya kukubali matokeo yoyote yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi.
 
Hahahahaha Haina shida bwashe ......uchaguzi siyo ugomvi. Maisha lazima yaendelee kama jamii. Kwa kuwa mtashindwa mkubali ili tuendelee kuishi kama jamii moja!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...........sawa mkuu twenda sawa zimebaki siku 10 tu
 
Muda mwingine tuwe wakweli, kabisaaa Tanzania inaongozwa na mtu aliyejipambanua wazi kabisa kuwa ni mtetezi wa Wezi na Wanyang'anyi wa Rasilimali zetu.
Huyo amegombea ili tu aingie kwenye orodha ya watu waliowahi kugombea Urais.
Kwa kifupi, JPM hana mpinzani.
 
JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea

Atakayeshinda kwa haki ndiye atangazwe hilo tu lakini uhuni kama ule wa Jecha safari hii hapana.
 
Najibu kichwa cha habari tu; hayo maelezo mengine sikuyasoma.

Sasa hilo nalo ni swali la kumuuliza yeye?

Kwani kuachia kiti ni hiari yake?

Elewa nimejibu swali kwa maswali hayo mawili.
 
Magufuli hata akishindwa uchaguzi na figisu zake zote ni king'ang'anizi hivyo ni ngumu sana kuwa tayari kuachia madaraka.

Kwa kipindi chake tu hiki cha kwanza cha miaka 5 ameonyesha kila dalili za kutaka kuwa Rais asiye na ukomo wa madaraka.

Watanzania tuamke Magufuli anaharibu nchi.
Trh 28 nafasi pekee tukicheza tu mwafaa.
Alijua upinzani umekufa atajipitisha tu bila kupingwa,hakutegemea ujio wa Lisu umemvuruga balaa, maana Lisu sio Lowasa.
 
Muda mwingine tuwe wakweli, kabisaaa Tanzania inaongozwa na mtu aliyejipambanua wazi kabisa kuwa ni mtetezi wa Wezi na Wanyang'anyi wa Rasilimali zetu.
Huyo amegombea ili tu aingie kwenye orodha ya watu waliowahi kugombea Urais.
Kwa kifupi, JPM hana mpinzani.
Wewe umechanganyikiwa kwelikweli, wala hujui unachoandika.
Na bado, subiri tu hiyo siku ya siku iwadie. Unaweza kujikuta unawehuka kabisa!
 
JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea
Angalia hizi bangi zinavyofanya kazi!
 
Hakuna Interview anayo ikubali Magufuli hapa ndio utajua kuwa jamaa ni muoga sana, kauli kama hizi maisha magufuli hawezi kutoa yeye anajua tu kuwa lazima aendelee kutawala kitu ambacho sio kabisa
Eti Magufuli ni muoga sana.

Ninyi watu mna mizaha sana.
 
Back
Top Bottom