Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,008
- 17,480
Niko natembelea ndugu zangu walioko pembezoni mwa miji kadhaa ambao vijiji au tuviite vitongoji au mitaa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, cha kushangaza havina umeme.
Viongozi wengi wamekuja na kupiga uongo eti wanaletewa umeme wa REA awamu ya tatu ni mwaka wa tano hawajaletewa. Waziri wa Nishati anatoa takwimu za uongo kusema asilimia (%) ya vijiji vimeunganishwa na umeme kwa awamu ya kwanza na ya pili na sasa ya tatu ni uongo mtupu.
Hebu nikupe mfano wa kijiji/kitongoji/mtaa wa Makurunge ulioko kata ya Kiluvya tarafa ya Sungwi wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani. Kuna nguzo za umeme zimepita barabara ya kuanzia Zahanati ya Makurunge hadi Majumba sita. Kwa awamu zoote hizo za REA ni nyumba kadhaa na chache mno ndani ya mita 20 tu ndo zenye umeme.
Wenye pesa zao baada ya kusubiri Rea ya uongo ndo wanaingia gharama ya kulipia nguzo kuanzia milioni 3 hadi 5 ndio wamepelekewa umeme. Wananchi wengi wamejenga wana watoto wa shule wako gizani alafu waziri anakudanganya.
Kama kijiji cha Makurunge kilichopitiwa na umeme mkubwa wako gizani sembuse vijiji vya ndani ndani? Viongozi mliopewa dhamana muogopeni Mungu na acheni kusema uongo. Huo umeme wa REA haupo mnapeleka umeme mpaka mtu atoe hela na kuacha wananchi wenye kipato duni gizani wakati umeme wa REA ulikuwa kwa ajili ya kusaidia kaya masikini.
Nawasilisha