Rais Magufuli: Wanaoikosoa serikali kwa staha hatuwachukii

Rais Magufuli: Wanaoikosoa serikali kwa staha hatuwachukii

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Rais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungumza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.

Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.

Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.
 
Kwa hiyo nikisema " Ndugu Rais kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu huu wa October 2020, (hamna haja ya kuzitaja zinajulikana kwa kila mtanzania mpiga kura) tunaomba kuanza mara moja kwa mchakato wa kuundwa kwa TUME HURU YA UCHAGUZI pamoja na mabadiliko yake ya KATIBA ambayo yataruhusu matokeo ya kura za URAIS yaweze kuhojiwa mahakamani kama kutakuwa na umuhimu huo kama zilivyo katiba za nchi karibia zote za Africa Mashariki (Majirani zetu)

Kama nikimwambia hivi nafikiri nitakuwa nimemshauri kwa staha.
 
Kwa hiyo nikisema " Ndugu Rais kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu huu wa October 2021, (hamna haja ya kuzitaja zinajulikana kwa kila mtanzania mpiga kura) tunaomba kuanza mara moja kwa mchakato wa kuundwa kwa TUME HURU YA UCHAGUZI pamoja na mabadiliko yake ya KATIBA ambayo yataruhusu matokeo ya kura za URAIS yaweze kuhojiwa mahakamani kama kutakuwa na umuhimu huo kama zilivyo nchi karibia zote za Africa Mashariki (Majirani zetu)

Kama nikimwambia hivi nafikiri nitakuwa nimemshauri kwa staha.
Sawa kabisa.
 
Hayo maneno kwenye KATIBA hakuna!! Kama hawezi arudi chato mbona hatujamuomba kuwa Rais

Hapa yenyewe tunamsaidia kupata utajiri.
Je, Katiba yetu tuliyonayo inaruhusu kutokuheshimu mamlaka iliyoko madarakani au kutokuwaheshimu wengine? Kukosoa Serikali bila staha kwa maana nyingine ni kudharau mamlaka iliyoko madarakani. Katiba yetu inaruhusu hilo?
 
Hapana, Katiba hairuhusu kutoheshimu mamlaka na kutumia lugha zisizofaa.
 
Sawa kabisa.
asante, Sasa ili kusudio langu liweze kufanikiwa nahitaji kuufikisha ujumbe huo kwa watanzania walio wengi zaidi - sasa ili twende pamoja naomba ushairi wako ni njia gani nitumie ? ili nisije kujikuta nakosoa bila staha.
 
Swali la kipuuzi.
 
Mwana kulitafuta mwana kuli get.

Yani kwenye mkutano Wa hadhara uwagombeze wakurugenzi kuwa nawalipa mshahara na Gari afu utangaze mpinzani mshindi.

Chuki ya wananchi naserikali ilianzia hapo,maana wanalipwa kwa kodi zao.
Hela haitoki mfukoni kwa mwenyekiti.
 
Post yako inahusika vipi na kukosoa kwa staha?
 
Sasa mkuu upuuzi wake ni upi? nia yangu ni njema kabisa kutaka kuufikisha ujumbe huo kwa wenzangu walio wengi au nakosea?
Hujui ni njia gani utumie?
 
Back
Top Bottom