Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Staha ni subjective na inaweza kuwa perceived tofauti na watu tofautiKukosoa Serikali bila staha kwa maana nyingine ni kudharau mamlaka iliyoko madarakani. Katiba yetu inaruhusu hilo?
Madhaifu muyaeleze kwa lugha nzuri.
Kwa nini mnamuita meko? Dikteta uchwara?Mimi naamini kila binadamu ana uwezo wa kubadilika labda mwenyewe awe hataki.
Nadhani Rais Magufuli, tangu aingie madarakani, anatambua kuwa kuna maeneo hakufanya vizuri. Japo hawezi kusema moja kwa moja, sisi raia tunaweza kutambua kutokana na kauli na matendo yake ya sasa ukifananisha na ya hapo awali.
Kwa mfano, kama kauli hii ameitoa toka moyoni na kwa dhamira njema, ni jambo lenye manufaa kwa Taifa. Taifa hili, safari yake ya kufikia maendeleo ya kweli itakuwa rahisi zaidi kama tukitambua kuwa tupo watu wengi, wenye mawazo mengi yanayotofautiana, ujuzi wa aina mbalimbali, tabia za aina mbalimbali na mitazamo mingi inayotofautiana. Tukizikubali tofauti hizi, basi hugeuka kama maua au mapambo kwenye vazi lako, na utaona ni baraka. Lakini ukizikataa, utayaona kama ni madoa na uchafu katika vazi lako.
Rais kama ameyanena hayo, kama namna ya kubadilisha mtazamo, nadhani kila mwenye hekima hawezi kukosoa kwa kutukana. Lakini hiki linatakiwa liende mpaka chini. Kuna wasaidizi wake wengine wana lugha chafu na za kejeli. Yaani mtu akitofautiana tu mtazamo au akakosoa, basi huyo ni kibaraka anayetumiwa na mabeberu au hana uzalendo. Kwa mtu ambaye una uhakika huna mawasiliano yoyote na beberu na wala hujawahi kutumiwa na mtu wala chombo chochote, na unajua Tanzania ndiyo nchi yako pekee, mtu akikutolea kauli chafu kama hizo, sidhani kama naye atakujibu kwa staha maana wewe umepanda uchafu, aghalabu utavuna uchafu.
Rais tunakuomba uheshima fikra za wengine, utumie lughabya staha dhidi ya wengine, himiza hivyo hivyo kwa wasaidizi wako, nina hakika nawe na Serikali yako mtakosolewa kwa staha.
Japo ukweli ni kuwa uchaguzi wa 2020 ulikuwa ni aibu kubwa kwa Taifa letu, na Ulimwengu wa demokrasia.
Magufuli is a damn blasted liarRais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.
Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.
Kuna magazeti yanaendeshwa na serikali Kama Hari leo, tanzanite, Uhuru, mzalendo, na hoja huwa yanawakosoa na kuwaandika kwa staha chadema???Rais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.
Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.
Ni swali zuri, lakini katiba hiyo hiyo pamoja na mambo mengine inataka uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli za siasa bila kuingiliwa, je hayo yanazingatiwa?Je, Katiba yetu tuliyonayo inaruhusu kutokuheshimu mamlaka iliyoko madarakani au kutokuwaheshimu wengine? Kukosoa Serikali bila staha kwa maana nyingine ni kudharau mamlaka iliyoko madarakani. Katiba yetu inaruhusu hilo?
-Yako wapi hayo matusi?Katiba inataka mtumie matusi?
- meko-Yako wapi hayo matusi?
-Amejuwaje kuwa wanaokufa hawafi kwa korona wakati vipimo vya Corona havifanyiki?
-wingi wa vyombo vya habari unahusianaje na uhuru wa vyombo hivyo?
Hivi kusema jiwe ni dikteta na huku ushahidi wa wazi ukitamalaki ni matusi ?Katiba inataka mtumie matusi?
kwenye katiba yapo tatizo hata katiba hamijuiHayo maneno kwenye KATIBA hakuna!!
- meko
-dikteta uchwara
-aliyekuambia wanakufa kwa korona nani?
- kutoa leseni ni uthibisho tosha
Tujiulize Tanzania tuna vyombo vya Habari credible vyenye uwezo wa kukosoa serikali yake ikanyamaza, magazeti kama Mawio, MwanaHalisi, Tanzania Daima yalifungiwa na serikali, sasa hivi serikali inapata upinzania mkali sana kupitia social media ndiyo maana wamejitokeza mawaziri watatu Nchemba, Bashugwa na Ndungulile wote wanatoa matamko juu ya mitandao. Serikali ijuulize kwa nini wanapata upinzania huko, imekosea wapi? ndiyo itakuwa suluhisho.Mwana kulitafuta mwana kuli get.
Yani kwenye mkutano Wa hadhara uwagombeze wakurugenzi kuwa nawalipa mshahara na Gari afu utangaze mpinzani mshindi.
Chuki ya wananchi naserikali ilianzia hapo,maana wanalipwa kwa kodi zao.
Hela haitoki mfukoni kwa mwenyekiti.
Unasema kwa nini huwa tunamwita Dikteta uchwara au Meko - sijui unamaanisha ni nani hao ambao huwa wanamwita hivyo.Kwa nini mnamuita meko? Dikteta uchwara?