Abul Aaliyah
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 7,718
- 5,899
Hzo ni A.K.A ambapo ni kawaida tu pia ni majina yanayompendeza kwerkwer
Kwa nini mnamuita meko? Dikteta uchwara?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini mnamuita meko? Dikteta uchwara?
Sio ombi, lakini tumia lugha ya staha.
Rejea mchakato wa kupata katiba mpya wa Tume ya Jaji Warioba ulivyovurundwa.Wewe unadhani ilitokea kwa bahati mbaya?This is not true.
ningelikuwa mimi mtu anayekosoa kama anamkosoa mtoto wake apigwe bakora,hii ndio nidhamu.Rais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungumza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.
Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.
Unasema kwa nini huwa tunamwita Dikteta uchwara au Meko - sijui unamaanisha ni nani hao ambao huwa wanamwita hivyo.
Sidhani kama kuna kundi lolote kwa misingi ya aina yoyote, waliwahi kukaa na kukubaliana kuwa Rais Magufuli aitwe Meko au dikteta uchwara. Ndiyo maana hata ukiwatafuta wapinzani au wanaomkosoa Rais Magufuli, wengi sana hawajawahi kumwita kwa majina hayo.
Lakini pia hakujawahi kuwa ns mkutano wa kukubaliana kuwa wanaCCM waitwe mataga au wanaCHADEMA waitwe nyumbu. Lakini pia katika ushindani, jokes na vitimbwi, hunogesha mijadala na upinzani.
Ukiwa kiongozi, huwezi kukwepa majina bandia, mengine ni ya kukukejeli lakini yapo pia kwa nia ya kukusifu.
Mwalimu Nyerere alikuwa akiitwa Mchongameno na majina mengine, lakini la Mchongameno lilifahamika kwa watu wengi. Mwalimu hakuwahi kukataa wala kukubali, na wengine walidhani hajui. Lakini baadaye wapo walianza kumwita Musa, hapo ndipo Mwalimu alipokemea. Kwa maneno yake alisema, 'mmeniita majina mengi, nimekubali. Mnaweza kuendelea kuniita kwa hayo majina, mara mchongameno, na mengine. Lakini hili la kuitwa MUSA, nalikataa'. Mwalimu alijiona hamkaribii kwa namna yoyote ile nabii Musa, aliyewaongoza wana wa Israel kutoka Misri kuelekea nchi ya ahadi.
Mzee Mwinyi alikuwa akiitwa Mzee Ruksa. Wapo waliomwita hivyo kama namna ya kumsifu alileta demokrasia, lakini wapo waliomwita hivyo kumkejeli kama mtu aliyeruhusu mambo yote yafanyike holela. Lakini Mwinyi, siku moja alipohojiwa kuwa anajisikiaje anapoitwa Mzee Ruksa? Alijibu nafarijika sana. "Maana unapita sehemu unaitwa Mzee Ruksa, Mzee Ruksa. Nafarijika kwa sababu wakati ule tulisema watu wasibanwebanwe, wawe huru".
Magufuli aliwahi kutamka mwenyewe kuwa yeye ni Jiwe, wapo baada ya pale wanaomwita hivyo. Wengine kwa kutaka kuonesha ni mtu asiyeyumbishwa, lakini wapo wanaomwita hivyo, wakimaanisha mtu asiyepokea ushauri. Lakini Rais mwenyewe anapoitwa Jiwe, anajisikiaje, hakuna aliyewahi kumwuliza. Hatujui anafurahia au anachukizwa.
Lakini ukiacha hoja za hapo juu, Rais Magufuli huenda ndiye Rais atakayeongoza kwa kuitwa majina mengi bandia. Ukumbuke, mwanzoni mwa utawala wa Rais Magufuli, wapo waliomkosoa Rais Magufuli kwa kumwandika jina lake halisi yaani Rais Magufuli, baadhi ya watu hawa walikamatwa, baadhi waliokuwa na bahati walishtakiwa, wengine mateso waliyoyapitia wanayajua wao. Lakini ikumbukwe mmojawapo alishinda kesi mahakamani kwa vile alimwandika Rais Magufuli kama Magu. Alishinda kwa sababu kisheria Magu, hakuna uthibitisho kuwa ni Rais Magufuli. Hiyo iliongeza sana tabia ya watu kumwita Rais Magufuli kwa majina mbalimbali ili tu kisheria wasionekana wanayemsema ni Rais Magufuli.
Ukitaka jambo liondoke au lipungue, ni watu kuwaacha wawe huru. Anayekosea ashtakiwa kwa kosa alilolitenda na siyo kumbambikia makosa ambayo hakuyatenda. Mtu amemkashfu Rais, halafu anakamatwa, mahakamani anashtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi ili tu akae ndani asipate mdhamana. Mambo hayo yanazidisha chuki na kuongeza lugha zisizo na staha.
Tukubaki tu kuwa Rais kuna wakati, nadhani kwa ghadhabu, anatumia lugha zisizo na staha. Mfano kule Tunduma, mama anamweleza Rais kero ya maji, yeye akamjibu, aende akamwombe mume wake! Jibu kama hilo halijengi mazingira ya chuki na lugha zisizo na staha? Lakini huenda Rais naye, alikuwa tayari ameaudhiwa na mambo mengine, ndiyo maana ile hekima ya uvumilivu ilimwondoka.
Mimi nimewahi kushuhudia, watu wanamwuliza mkuu wa wilaya maswali, mkuu wa Wilaya badala ya kujibu, anaanza kuwatukana waliouliza maswali na kuwaita wapumbavu na kuamuru wawekwe ndani. Kiongozi wa namna hii, nani atamheshimu? Nani atatumia kugha ya heshuma dhidi yake?
Kama tunataka kuanza upya, kila mmoja kuna mahali na namna ya kujirekebisha. Viongozi wawe wa kwanza kuonesha njia kwa kujirekebisha, raia watafuata. Na wale wabishi, watashtakiwa kwa haki kwa mujibu wa sheria kwa makosa yao hakisi waliyoyatenda, na siyo ya kuwatengenezea.
Kuna wakati niliwahi kutamka kuwa, binafsi, kidhamira naweza kupuuza mengi ambayo nahisi viongozi wamekosea (maana nia wao ni binadamu, lazima kuna makosa watafabya), lakini siwezi kuouuza wala kusamehe mambo ya kuteka watu, kuwapoteza, kuwaua, kuwatesa au kuwabambikia kesi. Huo ni unyama na ushetani ambao haustahili kuwepo kabisa katila jamii ya watu waliostaarabika, tena ambao zaidi ya 80% ni watu wanaomjua Mungu kuoitia imani mbalimbali. Nashukuru sana, na ninafarijika sana, kuwa hayo mambo kwa kiasi kikubwa mengine yamekoma, na mengine yamepungua.
Usitafute justification,lugha za staha zipo mtu mzima hafundishi labda iwe wewe ulikulia mazingira ya wahuni wasiokuwa na akili wala ustaarabuJaribu kutengeneza maneno ya staha katika kukosoa?
Tatizo letu tunadhani watu wana ridhaa ya kukosolewa kwa dharau. Kukosoa siyo ombi, ila pia hakuna mtu aliye na maridhiano ya kudhrarauliwa na mtu mwingineTatizo lenu mnadhani kukosoa ni ombi?
Usitafute justification,lugha za staha zipo mtu mzima hafundishi labda iwe wewe ulikulia mazingira ya wahuni wasiokuwa na akili wala ustaarabu
Tatizo letu tunadhani watu wana ridhaa ya kukosolewa kwa dharau. Kukosoa siyo ombi, ila pia hakuna mtu aliye na maridhiano ya kudhrarauliwa na mtu mwingine
Mrudisheni wenye mamlaka. Sisi wengine tulizaliwa as powerless as a snail, kila kitu huwa tunakipishaYeye akiona shida arudi Chato hakuna aliyemuomba kuwa Rais
Mrudisheni wenye mamlaka. Sisi wengine tulizaliwa as powerless as a snail, kila kitu huwa tunakipisha
Hapo kwenye matokeo kuhojiwa mahakamani ongeza na kuondolewa kinga ya mashtaka utakuwa umeuliza kwa staha sana ila hautapata jibuKwa hiyo nikisema " Ndugu Rais kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu huu wa October 2021, (hamna haja ya kuzitaja zinajulikana kwa kila mtanzania mpiga kura) tunaomba kuanza mara moja kwa mchakato wa kuundwa kwa TUME HURU YA UCHAGUZI pamoja na mabadiliko yake ya KATIBA ambayo yataruhusu matokeo ya kura za URAIS yaweze kuhojiwa mahakamani kama kutakuwa na umuhimu huo kama zilivyo katiba za nchi karibia zote za Africa Mashariki (Majirani zetu)
Kama nikimwambia hivi nafikiri nitakuwa nimemshauri kwa staha.
The same reason inayomfanya yeye akaita watu wapumbavu...unless sheria inamruhusuKwa nini mnamuita meko? Dikteta uchwara?
Na yeye akikuita mpumbavu?kwenye katiba yapo tatizo hata katiba hamijui
Katiba inatamka wazi kuwa kila mtu anastahili heshima na kutovunjiwa utu wake sasa ukiongea na mtu maneno yasiyo na heshima unakuwa umevunja katiba na kumvunjia hshima utu wake
ina maana hata ukichora katuni ya kumdhalilisha umevunja katiba ya nchi
Wanaikosoa lini 'Silent society surrender public responsibility' kwasasa ni bora liende tu cha ajabu siku hazigandiRais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungumza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.
Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.
Hapa ni sawa kabisa, kwa hiyo usubiri, umwachie yeye. Kwa sasa kuna mambo mengi ambayo yamo kwenye ilani ya CCM ambayo yanatakiwa kutekelezwa!Kwa hiyo nikisema " Ndugu Rais kutokana na changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu huu wa October 2020, (hamna haja ya kuzitaja zinajulikana kwa kila mtanzania mpiga kura) tunaomba kuanza mara moja kwa mchakato wa kuundwa kwa TUME HURU YA UCHAGUZI pamoja na mabadiliko yake ya KATIBA ambayo yataruhusu matokeo ya kura za URAIS yaweze kuhojiwa mahakamani kama kutakuwa na umuhimu huo kama zilivyo katiba za nchi karibia zote za Africa Mashariki (Majirani zetu)
Kama nikimwambia hivi nafikiri nitakuwa nimemshauri kwa staha.
Mbona kila mtu Tanzania anujua huo ujumbe? - mpaka uliundiwa tume, wakati wa kampeni Lissu alizunguka nchi nzima ananadi hicho, mpaka akasahau hata kujiombea kura! Mwamakula, juzu juzi alikuwa anaongelea hayo! Sasa wewe unataka kwenda kufikisha ujumbe huo wapi! Hapo ndipo unaanza kupoteza staha na kuwakera watanzania.Sasa mkuu upuuzi wake ni upi? nia yangu ni njema kabisa kutaka kuufikisha ujumbe huo kwa wenzangu walio wengi au nakosea?
Rais wa JMT ameyasema hayo wakati akizungumza na watanzania kupitia hadhara iliyokusanyika jana viwanja vya mnazimmoja.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kwa sasa hapa Tanzania kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimepewa leseni za kufanyia kazi na hii ni ishara kuwa kuna uhuru mkubwa wa habari hapa Tanzania.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuona kuna upotoshaji mkubwa unaofaywa na baadhi ya vyombo vya habari. Mfano ni kuandika habari za uzushi juu ya vifo vya viongozi na kupotosha kuwa sasa kuna maambukizi makubwa ya Corona tofauti na hali halisi.
Hivyo ni wazi kuwa kama serikali inakubali kukosolewa ni jambo jema kutumia lugha nzuri kufikikisha ujumbe kwa viongozi wa serikali ili wajirekebishe.