Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,486
- 3,408
Ni vigumu kuelewa Watanzania wengine akili zao wamewekeza wapi. Katiba ni waraka wa wananchi, siyo serikali. Wananchi wako juu ya Serikali, siyo kinyume chake. Serikali inawajibika kwa wananchi, siyo kinyue chake. Katiba inatoa uhuru kwa wananchi kupashana habari na kupeana taarifa, siyo kwa matakwa ya serikali. Sasa akina nyie mnataka serikali ikifanya maamuzi ya hovyo, na pengine maamuzi yanayohatarisha maisha ya wananchi (kwa mfano zigzag za COVID 19), wahanga waipigie magoti kuomba kuishauri serikali! Hopeless kabisa! Tabia hizi za maofisa wa serikali waliopo kazini na (the worst case scenario) wastaafu wa serikali, hazipaswi kuendekezwa na wananchi huru, katika taifa huru la kidemokrasia!Je, Katiba yetu tuliyonayo inaruhusu kutokuheshimu mamlaka iliyoko madarakani au kutokuwaheshimu wengine? Kukosoa Serikali bila staha kwa maana nyingine ni kudharau mamlaka iliyoko madarakani. Katiba yetu inaruhusu hilo?