Rais Magufuli: Wanaoikosoa serikali kwa staha hatuwachukii

ningelikuwa mimi mtu anayekosoa kama anamkosoa mtoto wake apigwe bakora,hii ndio nidhamu.

Hata kama raisi jukubaliani naye mitazamo basi unatakiwa umheshimu huku ukipinga mienendo yake kwa staha.
 
Well said,Ubarikiwe sana
 
Jaribu kutengeneza maneno ya staha katika kukosoa?
Usitafute justification,lugha za staha zipo mtu mzima hafundishi labda iwe wewe ulikulia mazingira ya wahuni wasiokuwa na akili wala ustaarabu
 
Tatizo lenu mnadhani kukosoa ni ombi?
Tatizo letu tunadhani watu wana ridhaa ya kukosolewa kwa dharau. Kukosoa siyo ombi, ila pia hakuna mtu aliye na maridhiano ya kudhrarauliwa na mtu mwingine
 
Usitafute justification,lugha za staha zipo mtu mzima hafundishi labda iwe wewe ulikulia mazingira ya wahuni wasiokuwa na akili wala ustaarabu



Kuna wakati nawaza watu kama nyinyi mtandaoni mnafanya nini? Maana hakuna mnachopata, serikali ya Magufuli hapendi ukweli hilo linajulikana!!

Ndio maana nilikuwa natumia mfano ya Gazeti ya UHURU na MUSIBA na watu wengi walilalamika kuhusu usemaji wao? Mfano Kinana, Mzee Makamba etc lakini hakuna aliyesema chochote akiwepo na Magufuli!

Pia alikuwa hana maneno ya staha, kwahyo yeye nani wa kuseme hiyo?

Kuwa mzalendo ni kuipenda nchi, sio lazima Serikali. Wakati mwingine Serikali hushikwa na kundi la waasi,wahuni au matapeli
 
Tatizo letu tunadhani watu wana ridhaa ya kukosolewa kwa dharau. Kukosoa siyo ombi, ila pia hakuna mtu aliye na maridhiano ya kudhrarauliwa na mtu mwingine

Yeye akiona shida arudi Chato hakuna aliyemuomba kuwa Rais
 
Hapo kwenye matokeo kuhojiwa mahakamani ongeza na kuondolewa kinga ya mashtaka utakuwa umeuliza kwa staha sana ila hautapata jibu
 
Na yeye akikuita mpumbavu?
 
Wanaikosoa lini 'Silent society surrender public responsibility' kwasasa ni bora liende tu cha ajabu siku hazigandi
 
Hapa ni sawa kabisa, kwa hiyo usubiri, umwachie yeye. Kwa sasa kuna mambo mengi ambayo yamo kwenye ilani ya CCM ambayo yanatakiwa kutekelezwa!
Hilo la katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi watu wengi wameisha liomba hivyo lisitukele. Tusubiri - sasa fikiria jingine.
 
Sasa mkuu upuuzi wake ni upi? nia yangu ni njema kabisa kutaka kuufikisha ujumbe huo kwa wenzangu walio wengi au nakosea?
Mbona kila mtu Tanzania anujua huo ujumbe? - mpaka uliundiwa tume, wakati wa kampeni Lissu alizunguka nchi nzima ananadi hicho, mpaka akasahau hata kujiombea kura! Mwamakula, juzu juzi alikuwa anaongelea hayo! Sasa wewe unataka kwenda kufikisha ujumbe huo wapi! Hapo ndipo unaanza kupoteza staha na kuwakera watanzania.
 

Watakua wamesifiwa sana mpaka wameanza kujishtukia....
 
Wao viongozi wanawastahi waTz? wananajisi kila kitu iweje watake staha. Turudi kwenye torati, Jino kwa jino. Halafu wanaogopa nini kukosolewa kwa maneno wakati wao wanawaharass wananchi kwa jeshi, mitutu, mahakama, kodi, n.k

Ni kweli wanaogopa maneno kiasi hicho au kuna ambacho hawakisemi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…