Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Mnataka press ya taifa ili iweje ..na utu uzima wako unaenda kunya unasubiri uambiwe utawaze au uchambe ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kila mtu mzima ana uelewa ulio nao wewe kuna wengine ni mtu nusu. press ya taifa ni muhimu itachangia kuleta attention kwa wengi wasio na uelewa wa hili jambo unadhani yule aliyepo "sitimbi" ana elimu yoyote kuhusu ili tatizo? Au hujui kiongozi mkuu ana influence na impact kubwa kwenye jamii?? Uwezo wako wa kuelewa jambo hauwezi kuwa sawa na yeyote yule bado inahitajika elimu kubwa kuhamasisha jamii kuhusu ili janga jombaa.
 
Ondoa hiyo chuki binafsi.
Kuna nchi ambayo imeshafanikiwa kuzuia maambukizi?

Hizo njia za kuzuia zilianza mwaka jana kipindi ambacho maambukizi kwa siku nzima yalikuwa hayazidi 1,000, kwa nini kama zinazuia Januari pamoja na kuendelea kutumia hizo njia kuna siku maambukizi yalikuwa mpaka 800,000 kwa siku?

Usitumie janga lililopo kueneza chuki binafsi kwa watu wote, hujazuiwa kufuata miongozo iliyopo, Vile vile umeongezewa mingine ya ziada. Hiyo Dodoma unayoisema watu wanaendelea na maisha kama kawaida na wengi hawana habari na hayo unayoyasema.

Punguza chuki binafsi zinakuumiza bure tu, toa ushauri kistaarabu na uje njia mbadala ambazo zitatusaidia katika hili janga.
Wajinga wako wengi. Tatizo ni kuwa hamjui english kama baba yenu na elimu yenu ni ya kuungaunga. Sikutegemea kuwa kuna kiongozi wa nchi mwenye level ya uelewa kama huyu. Na wajinga kama wewe mnahoji bila kujua hata mnachohoji. Unajua ilikuwa wafe watu wangapi kama nchi za Ulaya zisingechukuwa hatua? Unajua population ya wazee kule ni kiasi gani?
 
Numbe of fatalities caused by covid 19 in Italy? Kenya? Though lockdown and social distance measures were implemented.
Yaani wewe sijui kwann kichwa kigumu, Nchi hizo uluizotaja vifo vimepungua Sana baada ya Lockdown, social distancing. Sijui unatumia kamasi kufikiri.
 
Watanzania walikuwa wanasubiri kwa hamu kauli ya Amiri Jeshi Mkuu kuhusu uwepo wa Covid -19.

Wale waliokuwa wanaona soni kuvaa barakoa na kuji sanitize kwa kumuogopa namba moja, waanze mara moja, bila kusahau kuweka sanitize kwenye milango ya ofisi zenu.

Tukifanya kwa pamoja, tutapunguza athari zitokenazo na Covid -19.

Mungu ibariki Tanzania.
Mkuu, hao ndio tatizo kwa sababu ndio washauri wake. Wakisimama imara lazima tu na yeye abadilike. Angalia kanisa lilivyosimama imara na yeye kama muumuni ametambua.
Kisirisiri kuna kutoamini kama barakoa zinasaidia. Kuna haja gani kulinganisha ueezo wa barakoa na na uwezo wa Mungu.
Sayansi imetufunza mengi hata mpangilio wa kula. Mbona tunatumia dawa kwa kinga au kutibu kwani kwa kufanya hivyo tunsmpinga Mungu?
 
Maana yake serekali ilipaswa iwe imetoa miongozo kadhaa kuhusiana na kadhia hii ya Corona pamoja na kuisimamia kwa nguvu zote ila wao wanachofanya sasa hivi ni kuziponda barakoa,kuiponda social distancing na kuweka msisitizo katika maombi(Soma paragraph ya 5 katika waraka wao hapo juu).Yaani Tanzania imekuwa ni Taifa la maruwani linaloongozwa na viongozi maruwani!
Serikali ifanye kazi yake na Dini zifanye kazi yake.
Maisha ni kugawana majukumu.
 
Mkuu, nimesikiliza clip alichosema tofauti na kilichoandikwa naomba nenda kasikilize. Amewasifu wale ambao hawajavaa barakoa na kuwasifu waziri mkuu na makamu wa rais kutovaa barakoa kwa kuwa wanamuamini Mungu.

Amesema barakoa sawa ila tununue za hapa na kushonesha lakini walizozileta hizo barakoa anazosema kila leo zina corona ziliingia vipi nchini na madukani?

Hotuba ukiisikia kwa kweli ni ya kebehi kwa ugonjwa na wavaa barakoa. Naomba kamsikilize mwenyewe m, iko YouTube ni hotuba fulani hujui anataka kusema nini anaacha watu grey zone, hakuna message moja anauma na kupuliza. Inasikitisha kiongozi kuongea vile.

Kuna sehemu kasema “Hawa wasaidizi wangu hawajavaa barakoa na mimi sijavaa, kwani siogopi kifo? Wala sijui wamekutana na nani lakini naamini Mungu. Nchi nyingi waliovaa barakoa ndio wamekufa maelfu.” Sasa ni ujumbe gani kapeleka?

Hiyo statement wame soft baadhi ya maneno, kamsilize mwenyewe halafu uta comment.
Aliyeandika hiyo hotuba anaweza kutumbuliwa kwa kuandika tofauti na hisia za mwenye hotuba.
 
Mkuu, hao ndio tatizo kwa sababu ndio washauri wake. Wakisimama imara lazima tu na yeye abadilike. Angalia kanisa lilivyosimama imara na yeye kama muumuni ametambua.
Kisirisiri kuna kutoamini kama barakoa zinasaidia. Kuna haja gani kulinganisha ueezo wa barakoa na na uwezo wa Mungu.
Sayansi imetufunza mengi hata mpangilio wa kula. Mbona tunatumia dawa kwa kinga au kutibu kwani kwa kufanya hivyo tunsmpinga Mungu?
Afadhali amekiri uwepo wa Covid -19

Angeendelea kushupaza shingo angepigwa mapigo kama wa Ayubu hadi akiri kwa kinywa chake
 
Masikini Jaji Mihayo amekutana na Jiwe akavua kabarakoa kake. Siku akifa tunaambiwa kuwa wamekufa kidogo tuu ukilinganisha na huko duniani.
 
Toa elimu bila kueneza chuki zisizo na maana
Chuki gani? Anayesema barokoa zimewekwa virus ili tufe na anayesema tujikinge na virus ni nani anaeneza chuki? Anayesema hili suala la corona ni vita ya kiuchumi na mimi nayesema ni janga la dunia yote ni nani anaeneza chuki? Anayesema kuna watu walikwenda kuchanja wakarudi na corona ndiyo maana watu wanakufa na anayesema tujitahidi tupate chanjo ni nani anayeeneza chuki?
 
Hilo ndilo ninalotaka kusikia kwa kiongozi wa nchi.

Wananchi tupo tayari kusanehe yote yaliyopita, tuungane kwa nguvu zote, Raisi, viongozi was dini, taasisi zote na wananchi wote kupambana na Corona. Tushauriane, tuelekezane, lakini kwa lengo moja, kuyaokoa maisha yetu. Hata tusipofanikiwa kwa 100% lakini nina uhakika tutafanikiwa.

Kwenye tatizo hili hakuna mtu mmoja pekee yake mwenye jibu. Ni lazima tushirikiane sote, kuliko kuendesha Kila kitu kwa amri.
 
"Siku ina masaa 48"... Mwisho wa kunukuu.
Haa haa. Something is very wrong in upstairs. Hata hajui kuwa barakoa hazivaliwi muda wote mpaka unapokuwa umelala au uko nyumbani. Anajifanya hajui kuwa barakoa ni pale unapokuwa kwenye msongamano wa watu wengi tu.
 
Back
Top Bottom