Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Ni haki yako kuwa na mawazo kama hayo.

Rais katika hotuba yake, kwa lugha rahisi, ameeleza matumizi ya barakoa na madhara yake. Akatoa mifano ya nchi ambazo kuvaa barakoa ni sheria bado maambukizi yapo na wanakufa kwa wingi. Wataalam wa afya pia wanatoa angalizo la matumizi ya barakoa.

Hata vile amemwachia kila mtu kufanya uamuzi. Nawe rukhusa kufanya unaloona litakupitisha salama kwenye janga hili mradi huwi mmoja wa watakao ambukizwa au kuambukiza kwa sababu ya ujuaji na/au ujeuri
Nadhani hili linapotosha maana nzima ya uongozi, ikifika kipindi kila mtu aamue basi hakuna umuhimu tena wa kuwa na kiongozi ambaye ni jukumu lake kulinda wananchi kwa sera bora na kulinda taifa, ukiachia kila mtu kivyake basi isiwe katika hili hata na mengine ya kuamua kuandamana au kutoandamana kila mtu shauri yake, ukaimua kukimbia speed 100 au 50 juu yako utaona lipi bora kwako. Hakuna uongozi wa namna hiyo kuna mawili tu black and white, mambo ya shaurieni yenu kesho kitakuja kipindupindu tutasema shauri yako ukitaka kufanya usafi au hutaki juu yako japo usafi ni bora. Kiongozi ni dira kauli yako ndio mwelekeo...
 
Yeye kama kiongozi anatakiwa awe mfano kwa anaowaongoza kwa kuvaa barakoa ili kuonesha msisitizo.
Namshauri na yeye avae......huwezi kuleta kiburi kwenye Corona otherwise itamng'oa.
Imani yake ni kubwa kwa Mungu.sasa Kama ww ni muoga ,vaa balakoa,jifungie ndani n.k. na bado korona inauwezo wa kukuvabuwa hukohuko uliko.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Ni haki yako kuwa na mawazo kama hayo.

Rais katika hotuba yake, kwa lugha rahisi, ameeleza matumizi ya barakoa na madhara yake. Akatoa mifano ya nchi ambazo kuvaa barakoa ni sheria bado maambukizi yapo na wanakufa kwa wingi. Wataalam wa afya pia wanatoa angalizo la matumizi ya barakoa.

Hata vile amemwachia kila mtu kufanya uamuzi. Nawe rukhusa kufanya unaloona litakupitisha salama kwenye janga hili mradi huwi mmoja wa watakao ambukizwa au kuambukiza kwa sababu ya ujuaji na/au ujeuri
Ujuaji na mwenye hatari ya kuambukiza wengine ni yule asiyefuata ushauri wa madaktari na wataalamu. sasa nani asiyefuata? barakoa mbaya sasa nani aliyeziruhusu kuingia nchini? kuna watu wameenda kupigwa chanjo kuleta ugonjwa, hawa ni wauwaji kwanini usiwataje na kuwakamata?
 
Ameyasema hayo akiwa St. Peters katika Ibada alipopewa nafasi ya kutoa neno.

View attachment 1708018
View attachment 1708019

VIDEO:

Tatizo tulilo nalo kubwa ni kwamba, Magu amesha tuona Watanzania wote ni wapumbavu, mazwazwa na wachunga ng'ombe.
Kesha sema hakuna corona, hizo barakoa tuna vaa za nini???
Jamani hatuna rais hapa tuna comedian. Mara ndugu zangu wamekufa na corona, mara barakoa za nje ni mbaya, zikaingiaje Nchini????
Mungu humdaidia anae jisaidia. Kama ana amini Mungu hutenda mbona ana fanya kazi?
Angekaa nyumbani Mungu amlishe na kumvika..
Yaani kwa medani za kiaskari mkiwa vitani akifa askari mmoja lazima kiongozi wa kombania husikitika kumpoteza mpiganaji wake.
Inatia aibu na fedheha Rais alieapa kutulinda anapo sema tutakufa tuu. Yaani ni kinyaa, na hii ni wasaidizi wake kumuachia mike bila kumuandaa. Hapa Jpm haongozi nyumba yake bali analiongoza Taifa la Tanzania. Aweke interest zake mbali na dhamana aliyo kabidhiwa..
 
Mkuu waraka ni bora umeandikwa kiheshima kidogo kamsilize youtube kaponda kila kitu cha barakoa. wavaa barakoa hawaamini Mungu wasiovaa wanamuamini Mungu. kawatolea mfano masister wa tatu pale mbele wawili wamevaa mmoja hajavaa akasema namsifu huyu sister hajavaa inaonesha imani yake. akamsimamisha mama mmoja kuwa alikuwa na cancer akapona na barakoa hajavaa anamumini Mungu. alimjuaje huyu mama alikuwa na cancer, well staged drama
Kwani hujui kama jamaa anapenda sana kukamatia chini?
 
He is now coming to his sense.

Alikuwa anawasifia watu wasipovaa barakoa sasa akili inaanza kumrudia.

Alisema corona haipo sasa akili inamrudia kuwa huu msala upo na hauna utani.

Nimesikia sasa anakimbilia kwenye vita ya uchumi, eti hii ni vita ya uchumi, corona ni vita ya uchumi, uchumi gani?
Nilijua tu, Maana kwenu, Raisi akisema ni shida, akikaa kimya Bado ni shida
 
Itakuwa ile clip ya Ruwaichi imemuuma sana....anarudisha mashambulizi!?
 
kweni ww huamini Mungu yupo!!??

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
“Mwamini Mungu, lakini mfunge vizuri Ngamia wako”-Mtume Muhammad S.A.W

Mungu huwa halipi maombi bali hulipa jitihada!Kupiga maombi ya nguvu wakati hakuna mipango wala hatua(Actions) sahihi,stahiki na madhubuti za kupambana na Corona ni kumkejeli Mungu.Ukimkejeli Mungu tarajia mapigo saba ya ghadhabu ya Mungu.
 
Mkuu waraka ni bora umeandikwa kiheshima kidogo kamsilize youtube kaponda kila kitu cha barakoa. wavaa barakoa hawaamini Mungu wasiovaa wanamuamini Mungu. kawatolea mfano masister wa tatu pale mbele wawili wamevaa mmoja hajavaa akasema namsifu huyu sister hajavaa inaonesha imani yake. akamsimamisha mama mmoja kuwa alikuwa na cancer akapona na barakoa hajavaa anamumini Mungu. alimjuaje huyu mama alikuwa na cancer, well staged drama

Ni ajabu na kweli. Ametoa hotuba ya kukanganya kabisa (very controversial). Kwanza, ni kama anaona viongozi wa kanisa hawasisitizi vya kutosha umuhimu wa kumtegemea Mungu. Pili, kifo ni mpango wa Mungu; hakiepukiki! Tatu, serikali haijazuia kuvaa barakoa lakini barakoa, social distancing, lockdown hazisaidii kumaliza corona. Tena barakoa imported ni za hatari zaidi.

Nne kawasifu wasiovaa barakoa kwa ujasiri (kutokuwa na hofu); Tano, kawalaumu walioenda nje kuchanja kwa kuleta corona ya ajabu nchini. Tano kasisitiza kuwa tuko kwenye vita kubwa ya kiuchumi na kwamba “hawatupendi”!

Kwa kweli hii covid 19 ni changamoto. Naona inampa taabu sana Mheshimiwa.

Kifupi, bado hataki kusikia habari ya huu ugonjwa kuwepo nchini wala hatua za kukabiliana nao zilizokubaliwa chini ya WHO. Hivyo, tusitarajie kauli ya wazi (clarity) toka serikalini jinsi ya kupambana na covid 19. Ni juu ya kila mmoja kuamua cha kufanya.
 
Hivi huko kanisani ndio sehemu rasmi ya ku address janga kubwa na la kitaifa kama hili.

Alishindwa nini kufanya hotuba kama zile walizokua wanafanya watangulizi wake

Kipindi kile ukisikia rais anahutubia taifa basi station almost zote alikua anasikika live .
 
Sijasikia je kazungumzia na Nyungu hapo kanisani ama. Nipo Kimamba nalima nyanya Chungu hapa Rudewa.
Ndio amesema muendelee "kujifukizia" hata wasaidizi wake wameumwa na wamepona kwa "kujifukizia". Hata watoto wake wameumwa na wamepona kwa kujifukizia heheh! kumbe Rais ana dawa sisi tunahangaika tu!
 
Back
Top Bottom